Jiandae kisaikolojia na kuachwa wakati wowote

Jiandae kisaikolojia na kuachwa wakati wowote

timetoloveyourself

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2015
Posts
206
Reaction score
206
Wanajukwaa,kama heading inavyojieleza,
wimbi la kuachwa na kuachwa limekuwa kubwa likiathiri pande zote za jinsi(ke na me), wenyewe husema hakuna maumivu mabaya kama ya mapenzi,yawezekana ikawa kweli.

Mimi niwashauri wale wote ambao safari zao za kupata wenzi hazijafika kikomo,wakati wakiendelea na safari wazingatie ya kwamba kuna kuachwa,nazungumzia sana kuachwa kwa kuwa ndipo haswa maumivu yalipo,sina uhakika kama muachaj huumia sana kama muachwa,
sasa ili kupunguza maumivu ya roho na kuvunjika moyo wewe senior bachelor ukiingia kwenye mahusiano mapya jitahidi kuueleza ubongo wako kuwa kuna kuachwa kwa namna yoyote wakati wowote ili ikitokea uwe unatabasamu tu kama mgeni uliemtarajia.

Kukaa bachelor kwa muda ukijipa nafasi si mbaya pia, lakini ikumbukwe pia katika kuacha na kuachwa isiwe issue ya kuifurahikia sana kwa maana ya kubadilisha wapenzi kila wakati nayo si nzuri sana hivyo basi uvumilivu wakati mwingine panapo wezekana tusiruhusu kuachanaachana huku tunauma rohoni.
Salamu zenu ma senior bachelor, siku yenu ya ninyi pia kuwa double kitandani itafika tu endeleeni kuomba kwa imani.ila tabia za usingle tuzimalize kabla ya kuingia ndoani.
 
Kimsingi tegemea lolote, kwa sababu binadamu yeyote anaweza kufanya chochote wakati wowote bila kujali chochote!

Na mtu aliyezoea kuacha acha, haimchukui muda kuacha ni kitu rahisi tu kwa vile amezoea.
 
Yeah but ni shida kwa waliopenda na kuzama bila ya kuwa na mawazo that whenever there's a positivity so does Negativity stays..? Havn a plan "B" its a cure
 
Kuachwa kunauma endapo kwa wakati huo there's nothing else unachowaza zaidi ya mapenzi but if you wanted it to be just among other parts of your ordinary life, walaa... unaendelea na maisha kama kawaida, unaanzia pale ulipoachia... ni kama ambavyo ulikusudia kuweka pilipili kwenye mboga... ikakosekana, mitonge inaenda kama kawaida coz' it's just pili pili na sio chumvi!
 
Mada nzuri, ni kweli wanaoumia zaidi ni wale wanaoingia wakiwa hawajui kuwa kuachana kupo, wanajiona wamefika siku bomu likibust ni balaa, asante kwa kunikumbusha tena
 
Kimsingi tegemea lolote, kwa sababu binadamu yeyote anaweza kufanya chochote wakati wowote bila kujali chochote!

Na mtu aliyezoea kuacha acha, haimchukui muda kuacha ni kitu rahisi tu kwa vile amezoea.

wanandoa wenyewe huachana sembuse ninyi ambao hamjaoana.weka akili yako teyari kwa lolote esp pale unapoona mwenzio bado anaendelea na safari yake mapenzi
 
Back
Top Bottom