Ni uwanja mzuri kwa werevu,
Ni uwanja mzuri iwapo nia ni kujadili, kueleweshana na kukosoana pasipo ukali wa maneno,
Ni uwanja mzuri iwapo tu wachangiaji hawana uegemeo hata waeleweshwapo,
Ni uwanja mzuri sana tena sana kwa wenye nia njema ya kuchangia na kubadilishana kwa hoja, na si malumbano yasiyo na tija,
Ni uwanja mzuri kama sote tunaipenda na kuithamini JF yetu kama sehemu muhimu ktk jamii yetu ya kiTanzania kwa kuelimishana kiustaarabu.