JF Member wengi hawana hela ila wanajiita Great Thinkers, Kivipi?

JF Member wengi hawana hela ila wanajiita Great Thinkers, Kivipi?

Huu uzi ukiingia kichwa kichwa utaishia kuwa na hasira halafu utatoka bila bila

Ila ukiwa makini utatoka na kitu hapa

Nimeweka huu uzi baada ya Juzi kuweka tangazo langu la kuuza ac na vitu vingi tu tokea kitambo ila nikaja kugundua jf member wengi humu ni pangu pakavu tia mchuzi hela hamna

Mara nyingi watu wa jf huwaona watu wa istagram na facebook kama watu watoto ma wasiojielewa ila cha kushangaza Matajri wengi wapo instagram mimi nikiwa shahidi

Nilianza biashara viatu 2020 nikaanza kutangaza humu ila niliishia kupata hela ya kula tu na watu wachache sana, ila kuna mtu akanishauri nikatangaze facebook na instagram nilivyoelekea kule ndani ya miaka 3 tu instagram ilinipa wateja wengi nikafungua na duka yaani ilinileta kwenye maisha ya ndoto zangu ila nikajiuliza kwa nini jf ni pagumu kutoka kibiashara?

Juzi niliweka Ac hapa tena nlikuwa nauza kwa bei chee tu sh 690000 kama kawaida watu humu wengi wana zarau na hela hawana nikaishia kuona blaa blaa na masihara mara mtu anacoment laki 4 ipo mfuko wa shati mwingine ananiita mimi winga siku 3 sikupata mteja hapa

Basi nikaingia instagram nikalipia tangazo 5400 dola mbili nikatangaza kuwa nauza ac na vigezo vyake yaani ndani ya masaa machechs watu walikuwa wanagombania tangazo nililiweka usiku asubuhi saa 12 mteja akadamkia kwangu akatest akalipa akasepa nayo chap tu na wengine bado sim zikawa zinaita yaani instagram watu wana hela

Nilishawahi kuweka tangazo hapa jf Gari inauzwa bei chee tu crown no E KWA Milioni 13 tu ilikuwa inahitajika hela ya haraka ila kama kawaida watu hapa pesa ni ya mawazo ila kuja kutangaza insta ni chap niliuza nikaswma why jf?

Inatagram weka hata Range rover unauza milioni 300 shida chuma kiwe kizima na bei sio ya tamaa masaa 12 mengi unauza yaani watu wa kule pesa ipo sio ya kitoto na matajiri wengi hawatumii jf sijui ni kwa nini

Sasa how Come Great thinkers wengi humu hamna hela?

Jf kwa ushauri wa vilinge vya waganga wa kienyeji na mambo ya ushirikina tu wataalam wapo kama wote ,magonjwa watu wa msaada utawapata hapo napaheshimu ila michongo ya hela humu hapana

Jamii forum member wengi wana roho za kimaskini na wajuaji yaani utakuta umeweka tangazo lako maybe unahza ist yako nzuri tu mtu anakuja anasema gari mbovu , mwingine sio bei yake yaani ilimradi mtu aharibu muwe wote maskini

Ukitaka utoke chap kimaisha tangaza biashara yako instagram au fb hutojutia kule.
Wewe kauze vitu vyako hukohuko Tik Tok/Instagram/FB lakini humu hakuna mtu wa kujiingiza kwenye mtego wa panya, Melo mwenyewe yuko mafichoni mnataka kumuua.
 
Labda una CV ya upuuzi , kwa miaka takribani mi 5 iliyopita hapajatokea mpuuzi Jf kuzidi kiwango chako.

Sio kunihalibia ❌ = Kuniharibia ✅

Sasa kama kuandika kiswahili na kutofautisha kati ya L na R huwezi Kuna haja ya kubishana na wewe ?

Hapo si tayari umeshathibitisha kuwa wewe ni mjinga ?
Kohozi nimekutema, ole wako nikuone siku nyingine unakatiza pua yako mbele yangu.
 
Humu Jf tumejaa majobless ambao tupo fake fake fake. Kila mtu anajikuta ana hela na kazi nzuri, gari kali ila kwa ground hakuna kitu. Ukitaka kupoteza muda njoo JF ila ukiwa serious na biashara nenda mitandao mingine ya kijamii.

NB: JF tumejaa watu fake na waongo waongo tunaoishi kwenye maisha ya kufikirika.
Hio research umefanya wapi mkuu?
 
Hio research umefanya wapi mkuu?
Humu humu JF mkuu ingawa sio wote ila asilimia kubwa sana. Members wengi wa zamani walikuwa magreat thinkers kweli wenye vigezo vyote, ukiwa biashara unafanya, ushauri wanatoa wa kueleweka na hata misaada pia.

Then ikaja hii jf ya magen z ndio imejaza memba wenye sifa nilizozotaja hapo juu na wakafanya wenye michango chanya wengi wapotee humu
 
Jf ni dark site ndo maana watu hawatumii majina yao bali wanafake inawapa uhuru wa kuongea kiuwazi au kukosoa.

Usishangae hawajitokez hadharan wanahofia huenda ukawa mtego.

Taarifa za wanajf zinalindwa mno na wasimamizi wa jf.
 
Back
Top Bottom