JF ichangiwe kwa ulazima sasa...Tunachokipata humu ni kikubwa sana!

Plan Of Action

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
462
381
Habari za Jioni wadau?

Naomba tuungane hapa kwa mustakabali wa kuiendeleza JF yetu.

Hapa pamekuwa nyumbani sasa, kila kitu twakipata hapa.. habari za kila namna kwa kweli bila shaka mnajionea wenyewe!

Mimi kwa upande wangu na kwa mustakabali wa JF, ningependa Moderator na viongozi wengine wa JF waliangalie hili.

JF sasa ichangiwe kila mwezi walau Tshs 200 kwa kila member!

Kama kweli tupo 390,000 na kuendelea, ina maana JF itaweza kuingiza kiasi cha pesa 78million monthly!

Ifikie wakati tujali huduma itolewayo na mtandao huu.

Tunakabiliwa na kesi mbalimbali mahakamani, Je hizo kesi zinaendeshwaje kama si kupitia sisi?

Maoni yenu tafadhali..

cc Maxence Melo
 
Excellent. Ni wazo zuri kabisa. Hakuna atakayeshindwa kutoa sh. 500 kwa mwezi. Mbona watu wakienda bar wanaacha maelefu lakini wakirudi JF wanakutana na post zinazowachekesha mpaka mioyo inasuuzika? Na kuna mambo mengi sana tunajifunza humu.
mkuu nimeona niwashirikishe japo kwa haka ka wazo kangu
nawaona viongozi wa JF katika matatizo makubwa sana mahakamani,
najiuliza gharama za kuendesha kesi wanatoa wapi?
lazima tutoke jasho sasa japo kwa mia 2 kwa mwezi.
cc Paw Invisible Fang Maxence Melo na wengineo
hii hoja iwekwe mezani ijadiliwe kwa kina
 
nashangaa wadau wanapita kimya kimya
halafu wanalalamika sana wapoona mtandao unafungiwa ama viongozi kupelekwa mahakamani
mambo kama haya yabidi yapewe kipaumbele katika mambo ya fedha ili kesi zijiendeshe
 
Habari za Jioni wadau?
Naomba tuungane hapa kwa mustakabali wa kuiendeleza JF yetu..
Hapa pamekuwa nyumbani sasa, kila kitu twakipata hapa.. habari za kila namna kwa kweli bila shaka mnajionea wenyewe!
Mimi kwa upande wangu na kwa mustakabali wa JF, ningependa Moderator na viongozi wengine wa JF waliangalie hili.
JF sasa ichangiwe kila mwezi walau Tshs 200 kwa kila member!
Kama kweli tupo 390,000 na kuendelea, ina maana JF itaweza kuingiza kiasi cha pesa 78million monthly!
Ifikie wakati tujali huduma itolewayo na mtandao huu..
Tunakabiliwa na kesi mbalimbali mahakamani, Je hizo kesi zinaendeshwaje kama si kupitia sisi?
Maoni yenu tafadhali..

cc Maxence Melo Invisible
Wazo murua hili, kuchangia muhimu kama wakiitaji msaada kutoka kwetu, nitachangia kile nitakachokua nacho,,,
 
Hahaha, ni nafikiri wanaotakiwa kuchangia ni wale wanaoleta matangazo madogo madogo, hata 500/= itatosha, ukitaka tuchangie wote unataka kuuwa mtandao wako,
 
Wazo murua hili, kuchangia muhimu kama wakiitaji msaada kutoka kwetu, nitachangia kile nitakachokua nacho,,,
Naombea sana hili wazo lipite hata kwa ni kwa Tshs 100/= kwa mwezi.
Kama Real members wakiwa 150,000 basi itaongeza pato la JF..
Vile vile hata wenzetu wanapopata matatizo inakuwa rahisi kusaidia kama mtandao
mfano halisi ni mwenzetu PakaJimmy kapatwa na matatizo ajali ya Karatu kule mwanae kaaga,
Huwezi jua financial standing yake ikoje, ni vyema sasa Maxence Melo aweke hili kimkakati zaidi,
watu wachange monthly na tuoneshwe pato kila mwezi
Ikiwezekana kama hujachanga usiweze kuiaccess JF..
 
Excellent. Ni wazo zuri kabisa. Hakuna atakayeshindwa kutoa sh. 500 kwa mwezi. Mbona watu wakienda bar wanaacha maelefu lakini wakirudi JF wanakutana na post zinazowachekesha mpaka mioyo inasuuzika? Na kuna mambo mengi sana tunajifunza humu.
Karibu ungechangia kijanja ila ulipoingiza habari ya bar umeharibu lengo. Bar kuna nyama choma, pombe na wanawake wazuri hasa ukishautwika mzigo, unaweza kushika kalio bila vurugu, bar kuna starehe bana acha tu.
 
nao hawapati info muhimu humu jf?
tunategemeana sana mkuu
Sawa, sasa kama tunategemeana kwa nini tulipane mkuu, mtaji wako ni sisi member bac, tena kaka kuna member wanaingia fj kila siku kuwafuatilia watu flani wamepost nini, hawa wakiondoka ni shida
 
Back
Top Bottom