Soulbrother
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 405
- 17
Hakuna kitu inaitwa soo,tena ukinichanganya nitakupa ndoo
kughani hakuna veterani,kughani ni kipaji ulichonacho
unaweza kujiona veterani,kumbe watu anakuona tu bishow
i am always top of the top,na ndomaaana kila siku napata shows
mi ni mkalizaidi ya taisoni,na kwenye hili gemu nitatoa somo
Oyaaa wana tulizeni mizuka basi
Nyie wote mnacheza
Hamna lolote mnalosema
.............................................
(hapo ndo nimefikia kikomo wallahi hii aibu tupu niwaachie wenye fani zao za free style lol)
naona umekuwa mdogo,kama mistari yako ilivyo midogoNaona unakuja, lakini bado umbali
uso wako umekunja, vipi umekuwa mwanamwali
mpigie magoti jah, kabla kujibu swali
watakuja washikaji, hospitali kukujulia hali
naona umekuwa mdogo,kama mistari yako ilivyo midogo
unaishia kutoa matuci,ni dalili ya kuishiwa mavoko
jicho umelirembua utadhani mtarimbo umelala doro
jicho limekutoka,kwasababu ya bange na gongo
kwenye hii fani mi mkali,kwasababu natumia ubongo
yeeahh!yeeaahh!Oyaaa wana tulizeni mizuka basi
Nyie wote mnacheza
Hamna lolote mnalosema
.............................................
(hapo ndo nimefikia kikomo wallahi hii aibu tupu niwaachie wenye fani zao za free style lol)
aaah Nguli, hii swaafii!😉Battling is the basis for all rap music. The battle is the truest essence of rap and where rap music started. The object of a rap battle is to come up with insulting rap lyrics on the spot (not pre-written or pre-meditated) and rap them towards an opponent. The rapper with the best delivery, lyrics, and crowd response usually wins.
Learn to accept that it's only a vocal battle and there is no chance of you actually losing your life, surviving a rap battle is easier than it seems and happens to both contenders almost always unless a less traditional type of rap is performed, involving physical contact or firearms
Mfano tu....
Title yenyewe inajieleza namaanisha nini
Naanza na wewe uliyefulia kijana kloroquin
Mwanzoni nilihisi wewe mkali ka vile quinin
Kwa mashairi yako nimegundua sio makini
Ulijigamba ww ni tajiri wa vina na sio masikini
Nakusubiri kwenye next reply nione wako umakini.
Radical na Burn mko wapi kwenye yetu hii fani
Tuendeleee...
DISCLAIMER: MASHAIRI YOTE YATAKAYOPOSTIWA HAPA YATABAKIA MALI YA JAMII FORUM. COM.
bora ugeuke na uangalie mbali,huu ni moto wa tipaNageuka naangalia kando,naipa mistari yako kisogo
nisije nikajirusha mbali, nibaki hapa hapa bongo
unaninyoshea kidole, jichoni mwako kuna gogo
kama mimi nimetusi,ya kwako nini; na usiwe muongo
mistari yote si ubongo, sijui ulitoa wapi gongo
doro, mavoko na gongo, unatafuta vina dogo?
usitafute sana dogo, kwenye gemu usiwe na usongo
ndo maana naona simple, nikikwambia tulia dogo
yeeeeeehhh!Mzuka wakuu.
yeeeeeehhh!
mzuka
wamepata shock wamepigwa na butwaa
hawakutegema sasa wanachechemea
wamepigwa tobo hawana lakuongea
wanajiumauma hawalewi ni wapi pa kutokea
vichwa vinawauma,wameshachanganyikiwa
nitasema nao,mpaka leo kunakucha
nimekuja kikazimsijaja kutaniana
ninashusha vocal mpaka kitaeleweka
Mkuu pongezi kwa oustanding nyingi japo vina vinadunda
mc lazima apashe misuli moto na sio kula nyama na mrunda
Sometimes unategemea ushauri wa dr ukutoe na kukufunda
Najikubali noma na sio lazma niende kitunda ndio nile matunda
yeeeeeehhh!
mzuka
wamepata shock wamepigwa na butwaa
hawakutegema sasa wanachechemea
wamepigwa tobo hawana lakuongea
wanajiumauma hawalewi ni wapi pa kutokea
vichwa vinawauma,wameshachanganyikiwa
nitasema nao,mpaka leo kunakucha
nimekuja kikazimsijaja kutaniana
ninashusha vocal mpaka kitaeleweka
yeeeeaahh!Wacha spidi, usije ukafikia changanyikeni
tunaendelea spidi ile ile, kama sala aimen
kujiuma hatuwezi tumesimama wima hatupigi pembeni
mistari vina, hata na album mkitaka lingine semeni
vipi mbona kimya, hapa hamna brazameni
hili letu, kazi zetu, itikeni tena aimen
aaah Nguli, hii swaafii!😉
Great Thinkers naona wengi yenu butu mistari imejaa kutu
Wengine vina chuku hoja ukasuku mtatoka tupu
Bantugbro ngoja niwapeni somo ki-Tumbuktu
Thubutu acha ukuku freestyle battle makini iko huku
Tazama mwana ntaKu-Cabinda ki-Togo kwa mitutu ya Mobutu
Zamani kabla ya luku tulichana mitaa flani ilikuwa fani halafu ikajaa upupu
Tukaenda ughaibuni majaribuni uzayuni maisha ya kipopo tunakula fufu
Yeaah, sikia kengele inalia saa imefika wakulu sasa ni shifi ya usiku
wakuu nimewakubali
kwa vyenu vina vikali
kwa kuwa mnaona mbali
Ninyi nyote ni majabali
Mmechuana vikali
kuonyesha mnajali
hakika Jf ina marijali
Kila mmoja anawakubali
Yoyoyooo yeah yeah
Mazee kwa wote mliorhyme mnatisha
SoulBrother n Bantgbrother karibu kuwakilsha
Salamu kutoka kwa Naniliu na JS nimezifikisha
Burn Leo pumzi kapandisha lakini zimemkwsha
yes! Yes! nabadilisha mada natafuta engo ya uhakika,
leo hii ma rhymer nawahakikishia nikipewa urasi wa Africa,
nitafaanya maajabu nitachoma silaha zote na zenu avatar,
bara hili limejaa vita kila kona hata wachezaji togo kughafilika,
wakuu nimewakubali
kwa vyenu vina vikali
kwa kuwa mnaona mbali
ninyi nyote ni majabali
mmechuana vikali
kuonyesha mnajali
hakika jf ina marijali
kila mmoja anawakubali
yoyoyooo yeah yeah