JF Exclusive: CAG Report on IPTL/Tegeta Escrow Account

kakobe noma, hii ishu ya escrow siyo mchezo "the big brother is watching you"


Mimi hofu yangu ni juu ya sintofahamu au mtifuano utakao tokea bungeni...

Sitamani PM ajiuzulu maana itakuwa mzigo kwetu Bali hela iliyozidi irejeshwe....
 
Akishindwa kukuelewa basi usimueleweshe tena...

Watanzania wa namna yake ni wengi mno halafu ndio walalamishi nambari moja...

 
Akishindwa kukuelewa basi usimueleweshe tena...

Watanzania wa namna yake ni wengi mno halafu ndio walalamishi nambari moja...

Hawa ndio wanaochelewesha mabadiliko kuanzia ndani ya CCM na nje ya CCM...

Kukimaliza kizazi cha namna hii kisichoweza kufikiri nje ya kula na starehe itatugharimu miaka mingi....
 
Ni viambatanisho mkuu wangu. Basically tunavyo, na hata hizo pages mbili nilizoweka zimenyofolewa!

Hapa ninachotaka wafahamu ni kuwa, hatutaki kuingilia utendaji wa Bunge lakini wasihangaike na sarakasi zao; moto huu hauzimiki kwa kuumwagia petroli!

Invisible,

Kweli kuna moto lakini?

Ila, cha kushangaza. Tuseme hela ni za IPTL, inakuwakuwaje wanalipwa viongozi waandamizi wa serikali kwenye akauti zao? Kwa mfano, Tsh Bilioni 1.6 kwa Tibaijuka na Chenge? Hawa ni wa kuozea jela tu.
 
Tetesi zilizoko ni kuwa hio taarifa ya CAG imechakachuliwa kabla ya kuwasilishwa bungeni, hofu kubwa ya PM ni uwezekano wa kuibuliwa Original version !!! Nimrod Mkono inasemekana anayo uncut version !!! Mkuu Invisible ikiwezekana tuwekee na ile ya PCCB ili kukata mzizi wa fitna...
 


Yeah usemayo yanakaribiana na ukweli but kitu kikubwa kinachosumbua ni kwamba hakuna umoja....

hili suala limechukua sura mpya na ni mgogoro Wa kimaslahi lakini wenye kiini cha ukweli ( hapa namaanisha makosa yapo tena yakutisha ila wachezaji wameamua kuyaonesha ili kukomoana)

kauli ya Muhongo juu ya hasira za vitalu vya gesi na kunyimwa mikataba ni kweli but the question is that je? hicho wanachosimamia hao wanaokuwinda ni uzushi ama ukweli?

Hivi mbaya wako akikuona unaiba na vithibitisho anavyo atakuchekea?

"hamuwezi kuwa na umoja. kwenye uovu"****** JOB NDUGAI.
 
Thank you Jamiiforums na wale mnaoitakia mema Tanzania

Nimewaza sana kuanzia juzi, hasa hii tabia yetu ya "kuheshimu na kutukuza watu" bila tija nikasema IT CAN BE DONE, if we all say no, regardless of political affiliation, kila mwizi ataogopa bila kujali itikadi yake

IT IS TIME TO STAND UP AND BE COUNTED AS TANZANIANS - YES WE CAN!!
 
Invisible weka jalada lote kabla hujatolewa meno na mbavu! Pinda katoa maagizo kila mwenye kikaratasi cha CAG apigwe. Sasa saidia taifa kabla ya kutolewa meno
 
Asante JF hatimaye ni wewe tunayekufahamu,wewe ni Fagio la chuma ati.kwa kipande hiki tu tayari majanga makubwa.
 
Mkuu lusungo kwanza nakushukuru kwa kunitag kwenye huu uzi. Pole kwa vitisho ila kuwa makini Mkuu popote pale utakapokuwa hawa wahuni kuchukua uhai wa binadamu mwenzao kwao ni jambo dogo sana. Vitisho kweli vipo hata humu ndani vimo sana tu ambavyo mimi nimeamua kuvidharau lakini kuwa makini mno kwenye nyendo zangu za kila siku na nimeshabadili baadhi ya taratibu za nyendo zangu hasa ninapokuwa kwenye kadamnasi hivyo nawe kuwa muangalifu mno. Kumbuka ni juzi tu Nimrod Mkono alionywa awe muangalifu alipokuwa UK na bado wauaji waliweza kumpa sumu.

Ninakuheshimu sana pamoja na UCCM wako maana wewe ni tofauti na wengine hapa na siku zote umeamua kusimamia maslahi ya Tanzania na Watanzania, siku za mwanzo tulikwaruzana sana kule kwenye siasa lakini siku hizi tumekuwa mabest.

Haya Mkuu uwe na Jumapili njema.


 
Nakaa chini najiuliza huyu aliye nyuma ya huu ufisadi hasa ni nani? Siamini kabisa kama ni hawa wachache ambao nimekwisha wasikia. Huyu mwenye uwezo wa kuingia na kuchomoa nyaraka ofisi ya Bunge, ofisi ya CAG, kamati ya PAC. Tumesikia Mkono naye kalishwa sumu (anaaminika ndo kagawa details za ndani za escrow). Huyu si mtu mdogo anaye fanya hivi. Huu ufisadi bila shaka umejumuisha taasisi nyeti. Ni ipi? Ni CCM? Ni Ikulu?
 
Hii ishu bila wanaCCM kuwa against nayo isingefika hapa ilipo....

Think big.....
CCM wangekuwa against hii issue wangeivumbua mapema kwa sababu wana full access na mambo yanayofanyika, lakini walikaa kimya hadi pale issue ilipofunuliwa na mbunge wa upinzani sasa CCM nao wanajifanya kuamka! Hivi lusungo unataka kutuaminisha CCM hasa waandamizi wakuu hawakujua uwepo wa huu uharamia kabla ya mhe. Kafulila?
 
Last edited by a moderator:
Dah.........Ni around kumi na nusu alfajiri napata Nondo za kufa mtu.....kha......nimekumbuka Shule Ndio ilikuwa midas yangu ya kuamka na kuchangamsha akili....... Heshima nene kwa JF.
 

Yes against ukawa and no against mafisadi
 
thanks you Invisible hawa ccm wanafanya mambo ya kitoto kabisa ni wasomi lakini mambo yao ni hovyo kabisa/kwani kujiuzulu na kurejesha hizo fedha kuna ubaya gani?kuokoa muda na nchi ikarudi ktk mstari wake,wanaguard upuuzi na uchafu huu/mean WOTE NI WACHAFU NA HAWATUFAI
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…