Jeshi nchini Gabon lapindua Serikali ya Ali Bongo

SECRET AGENT

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2019
Posts
254
Reaction score
499
Jeshi nchini Gabon limetangaza kwamba limetekeleza mapinduzi ya serikali katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Wanajeshi wenye vifaru na magari ya kivita wanashika doria katika barabara za mji mkuu Libreville.

Amri ya kutotoka nje imetangazwa.

Tangazo kutoka kwa kundi la vijana wa umri wa makamo linatangazwa na kurudiwa katika kituo cha redio cha serikali nchini humo, ambapo wanasema kumekuwepo na wasiwasi kuhusu uwezo wa Rais Ali Bongo kuongoza nchi hiyo.

Wanakosoa pia viongozi wakuu wa jeshi nchini humo.

Bw Bongo amekuwa nje ya nchi hiyo kwa zaidi ya miezi miwili, akipokea matibabu nchini Morocco kutokana na maradhi ambayo hayajafichuliwa baada yake kuugua akiwa ziarani Saudi Arabia.

Familia ya Bongo imetawala taifa hilo kwa miaka 51 iliyopita, na imetuhumiwa kwa kujilimbikizia mali na utajiri mkubwa kutokana na rasilimali za taifa hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kundi la wanajeshi nchini Gabon limetangaza kwamba limetekeleza mapinduzi ya serikali katika taifa hilo la Afrika Magharibi.
Wanajeshi wenye vifaru na magari ya kivita wanashika doria katika barabara za mji mkuu Libreville. Shirika la habari la AFP inasema milio ya risasi imesikika jijini humo.
Amri ya kutotoka nje imetangazwa.
Tangazo kutoka kwa kundi la vijana wa umri wa makamo linatangazwa na kurudiwa katika kituo cha redio cha serikali nchini humo, ambapo wanasema kumekuwepo na wasiwasi kuhusu uwezo wa Rais Ali Bongo kuongoza nchi hiyo.
Wanajeshi hao wametangaza kwamba wanataka kuunda 'Baraza la Ufufuzi/Ukombozi'.

Wamekosoa hotuba ya Mwaka Mpya iliyotolewa na Rais Bongo mnamo 31 Desemba, na wanasema kwenye hotuba hiyo mawazo yake yalionekana kutotiririka na sauti yake ilikuwa dhaifu.
Bw Bongo amekuwa nje ya nchi hiyo kwa zaidi ya miezi miwili, akipokea matibabu nchini Morocco kutokana na maradhi ambayo hayajafichuliwa baada yake kuugua akiwa ziarani Saudi Arabia 24 Oktoba kuhudhuria mkutano mkubwa wa kiuchumi nchini humo.
Familia ya Bongo imetawala taifa hilo kwa miaka 51 iliyopita, na imetuhumiwa kwa kujilimbikizia mali na utajiri mkubwa kutokana na rasilimali za taifa hilo.

SOURCE: BBC SWAHILI
 
Jeshi nchini Gabon limetangaza kwamba limetekeleza mapinduzi ya serikali katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Wanajeshi wenye vifaru na magari ya kivita wanashika doria katika barabara za mji mkuu Libreville.

Amri ya kutotoka nje imetangazwa.

Tangazo kutoka kwa kundi la vijana wa umri wa makamo linatangazwa na kurudiwa katika kituo cha redio cha serikali nchini humo, ambapo wanasema kumekuwepo na wasiwasi kuhusu uwezo wa Rais Ali Bongo kuongoza nchi hiyo.

Wanakosoa pia viongozi wakuu wa jeshi nchini humo.

Bw Bongo amekuwa nje ya nchi hiyo kwa zaidi ya miezi miwili, akipokea matibabu nchini Morocco kutokana na maradhi ambayo hayajafichuliwa baada yake kuugua akiwa ziarani Saudi Arabia.

Familia ya Bongo imetawala taifa hilo kwa miaka 51 iliyopita, na imetuhumiwa kwa kujilimbikizia mali na utajiri mkubwa kutokana na rasilimali za taifa hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo matokeo y uongozi wakiimla

Fundisho kwa Jiwe

Be aware, when your neighbor is being......

Ni upuuzi sana kusubiria kuwa dictator atakuja kuwa na mwisho mbaya huko mbeleni wakati huo huowatu wanaendelea kuchapika
 
Back
Top Bottom