Jeshi la Zimbabwe lakanusha kufanya mapinduzi

Jeshi la Zimbabwe lakanusha kufanya mapinduzi

LENGISHO

Senior Member
Joined
Sep 15, 2017
Posts
169
Reaction score
265
Jeshi la Zimbabwe limekanusha madai kwamba mapinduzi ya kijeshi yamefanyika kuiondoa serekali, na kudai kwamba rais Robert Mugabe na familia yake wapo salama.

Katika taarifa iliyotolewa na jeshi kupitia televisheni ya taifa, imeelezwa kwamba jeshi linalenga wahalifu wanaosababisha shida za kijamii na kiuchumi na kuwafikisha mbele ya sheria.

Taarifa hiyo imetolewa baada ya mashuhuda kusema wamesikia takriban milipuko mitatu pamoja na milio ya risasi katika mji mkuu wa Harare, usiku wa kuamkia Jumatano.

Inaelezwa pia na mashuhuda magari ya jeshi na wanajeshi walikuwa katika mitaa mapema Jumatano hii saa kadhaa baada ya wanajeshi kushikilia chombo cha utangazaji cha serekali cha ZBC.

Wakazi wamesema kwamba tofauti na kuwepo kwa taarifa ya habari ya saa tano usiku, ZBC ilicheza muziki bila taarifa yoyote.

Msemaji wa ubalozi wa Marekani mjini Harare, alinukuliwa akisema kwamba mitaa ya Harare ilionekana kuwa tulivu usiku wa kuamkia leo, na hakuthibitisha kuona magari ya kijeshi. Msemaji huyo pia amesema hana taarifa ya milipuko yoyote kutokea kama ilivyoelezwa na baadhi ya wakazi wa Harare.

Hapo jana Jumanne, chama tawala nchini Zimbabwe ZANU-PF kilimshutumu mkuu wa majeshi kwa vitendo vya uhaini baada ya kutishia kuingilia kati mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo.

Taarifa ya ZANU-PF ilitolewa katikati ya wasiwasi uliotanda kwamba jeshi limechukuwa hatua ya kuchukuwa madaraka na kumuondoa rais wa muda mrefu wa Zimbabwe, Robert Mugabe.

Mashuhuda waliripoti kuona vifaru na maafisa wa jeshi wakiwa mitaani na kelekea nje ya mji licha ya Harare kuwa tulivu. Balozi za nchi mbalimbali nchini humo hazikutoa tahadhari kwa raia wake walioko nchini Zimbabwe kwa sasa.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani pia alinukuliwa akisema kwamba wanataarifa hizo na wanaendelea kufanya uangalizi.

Hali ya wasiwasi ya sasa ilizuka juma lililopita wakati rais Robert Mugabe alipomfukuza naibu wake Emmerson Mnangagwa na kumshutumu kwa kutomti na kupanga kutwaa madaraka.

Chanzo: UKOMBOZ BLOG
JESHI LA ZIMBABWE.jpg
 
Yale maneno yake kuntu mzee leo hayatamsaidia.hasa ile quote yake ya 'ukifutia taulo takoni leo kesho utafutia usoni'hahhaa
 
Hicho kibabu kingetulia kilee wajukumu kistaafu kwa heshima kuliko kwenda kufia jela, ataondoka ataiacha Zimbabwe kibishi kusoma alama za nyakati
 
Jeshi likisema limepindua litatengwa na jumuiya za kimataifa, hivyo njia nyepesi ni hiyo waliofanya then mzee atatangaza kujiuzulu bila ugomvi. Watapanga tarehe ya uchaguzi mambo yanaisha.
 
Kwa nini liseme jeshi lenyewe? Hakuna msemaji wa serikali? Think twice
siasa za zimbabwe ni ngumu kuzielewa kama sio mfuatiliaji na ndomana hadi leo Mugabe ni rais. jeshi la Zimbabwe asilimia 90 ni ZANU-PF wengi wanaongoza jeshi walipigania uhuru kipindi hiko,walichofanya jana nikuzima kinachoitwa vuguvugu la Aliyekuwa Vice President kwakuwa huyu mtu ananguvu sio tuu katika chama pia katika jeshi na taifa kwa ujumla.
 
Duuu hii inatoa Funzo kwa Viongozi wengine wa Kiafrika ambao wakishapata Madaraka hawataki Kung'atuka na wakitaka Kung'atuka wanataka Kufanya ikulu Kuwa za Familia zao...... Mugabe alisaidia sana Afrika na Zimbabwe kwa Ujumla ila uroho wake wa madaraka umempeleka pabaya ... ilifikia sehemu akajiona ni Mungu Mtu wa Zimbabwe...
 
Zimbabwe military's statement after seizing power

Reuters Staff

4 MIN READ

HARARE (Reuters) - Following is the text of an address made by Zimbabwe Major General SB Moyo, Chief of Staff Logistics, on national television after the military seized power:


Soldiers stand beside military vehicles just outside Harare, Zimbabwe November 14, 2017. REUTERS/Philimon Bulawayo
”Following the address we made on November 13, 2017, which we believe our main broadcaster, the Zimbabwe Broadcasting Corporation and The Herald were directed not to publicize, the situation in our country has moved to another level. Firstly, we wish to assure the nation that His Excellency the President of the Republic of Zimbabwe, and commander-in-chief of Zimbabwe Defence Forces, Comrade RG Mugabe, and his family are safe and sound and their security is guaranteed.

”We are only targeting criminals around him who are committing crimes that are causing social and economic suffering in the country in order to bring them to justice.


”As soon as we have accomplished our mission, we expect that the situation will return to normalcy. To the civil servants, as you are aware, there is a plan by the same individuals to influence the current purging that is taking place in the political sphere to the civil service. We are against that act of injustice and we intend to protect every one of you against that.

”To the judiciary, the measures underway are intended to assure that as an independent arm of the state you are able to exercise your independent authority without fear of being obstructed as has been the case with this group of individuals.


”To our members of parliament, your legislative role is of paramount importance for peace and stability in this country and it is our desire that a dispensation is created that allows you to serve your respective political constituencies according to democratic tenets.

”To the generality of the people of Zimbabwe we urge you to remain calm and limit unnecessary movement. However, we encourage those who are employed and those with essential business in the city to continue their normal activities usual. Our wish is that you enjoy your rights and freedoms and that we return our country to a dispensation that allows for investment, development and prosperity that we all fought for and for which many of our citizens paid the supreme sacrifice.

”To political parties we urge you to discourage your members from engaging in violent behavior.

”To the youth we call upon you to realize that the future of this country is yours. Do not be enticed with dirty coins of silver. Be disciplined and remain committed to the ethos and values of this great nation.

”To all churches and religious organizations in Zimbabwe we call upon you and your congregations to pray for our country and preach the gospel of love, peace, unity and development.

”To both our people and the world beyond our borders, we wish to make it abundantly clear that this is not a military takeover of government. What the Zimbabwe Defence Forces is actually doing is to pacify a degenerating political, social and economic situation in our country, which if not addressed may result in a violent conflict.

”We call upon all the war veterans to play positive in ensuring peace, stability and unity in the country.

”To members of the defense forces, all leave is canceled and you all to return to your barracks with immediate effect.

”To our respected traditional leaders, you are our custodians of our culture, customs, traditions and heritage and we request you to provide leadership and direction to your communities for the sake of unity and development in our country.


”To the other Security Services: We urge you to cooperate for the good of our country. Let it be clear that we intend to address the human security threats in our country. Therefore any provocation will be met with an appropriate response.

”To the media; we urge you report fairly and responsibly.

“Thank you”

Zimbabwe military's statement after seizing power
 
siasa za zimbabwe ni ngumu kuzielewa kama sio mfuatiliaji na ndomana hadi leo Mugabe ni rais. jeshi la Zimbabwe asilimia 90 ni ZANU-PF wengi wanaongoza jeshi walipigania uhuru kipindi hiko,walichofanya jana nikuzima kinachoitwa vuguvugu la Aliyekuwa Vice President kwakuwa huyu mtu ananguvu sio tuu katika chama pia katika jeshi na taifa kwa ujumla.
Mugabe chali na taarifa kutoka afrika kusini zinasema muda wowote atatangaza kuachia madaraka, I am sure atapewa hidadhi huko.
Watu wamechoshwa na Grace kuongoza nchi kwa kivuli cha mumewe na sasa anataka ashuke usukani kabisa
 
Back
Top Bottom