Jeshi la Yemen latungua ndege ya Marekani

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Jeshi la Yemen latungua ndege ya Marekani

Jeshi la Yemen limetangaza kuwa limefanikiwa kutungua ndege ya kijasusi ya Jeshi la Marekani katika anga ya mkoa wa Ma'rib.

Msemaji wa Jeshi la Yemen Yahya Saree aesema ndege hiyo isiyo na rubani au drone iliyotunguliwa ni aina ya Scan-Eagle na ilitunguliwa wakati ikiwa inapaa katika anga ya eneo la Mashjah mkoani Ma'rib.

Ameongeza kuwa drone hiyo ya kisasa kabisa imetunguliwa na wanajeshi wa Yemen waliokuwa wakitumia kombora la nchi kavu kuelekea angani.

Msemajji huyo wa Jeshi la Yemen amesisitiza kuwa, wanajeshi wa Yemen hawatasita hata kidogo katika kutekeleza majukumu yao ya kuilinda anga ya nchi hiyo ili kuzima hujuma za wavamizi.

[https://media]Msemaji wa Jeshi la Yemen Yahya Saree

Ndege kadhaa zisizo na rubani za Jeshi la Marekani zimetunguliwa na Jeshi la Yemen linaloshirikiana na kamati za wanachi za kujitolea vitani tangu Saudi Arabia ilipoanzisha uvamizi dhidi ya Yemen mwaka 2015.

Saudi Arabia inaungwa mkono kijeshi na Marekani katika uvamizi wake unaoendelea dhidi ya Yemen na ambao umepelekea makumu ya maelfu ya Wayemen kupoteza maisha wengi wakiwa ni wanawake na watoto wasio na hatia.

4by21a267939e41w730_800C450.jpg
 
Umetushitua mkuu.kumbe ni drone ndiyo imetungulia na siy ilibeba abiria.
 
sema drone . watu mna mbwembwe na ushabiki maandazi
 
Huu ni ushabiki wa kitoto sana! kutungua drone unasema kutungua ndege na je ingetunguliwa ndege si mngefanya public holiday kusherekea! Naftali Benet kashika hatamu sasa, mtamkoma huko middle east.mnapenda sana kuandamana sasa sio tuu kuandamana bali pia mtafanya charity za vilio!
 
Kwa ujinga wao wataende wakachukue mabaki ya hiyo drone na kuipeleka kambini ndipo watajua wameji-expose?
 
inawezekanaje drone ya maarekani ikatunguliwa kirahi ivyo?au m ndio sijaelewa .
 
Huu ni ushabiki wa kitoto sana! kutungua drone unasema kutungua ndege na je ingetunguliwa ndege si mngefanya public holiday kusherekea! Naftali Benet kashika hatamu sasa, mtamkoma huko middle east.mnapenda sana kuandamana sasa sio tuu kuandamana bali pia mtafanya charity za vilio!
Drone yenyewe ni zile za kuulia nzige
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom