Jeshi la wananchi Tanzania limetoa boti nne na askari kwa ajili ya ulinzi wa rasilimali za Ziwa Victoria

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512
boti.png


Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mara imepokea boti nne za kisasa kutoka kwa Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo kwa ajili kusaidia shughuli za doria katika Ziwa Victoria ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania dk John Pombe Magufuli katika kulinda rasilimali ndani ya ziwa hilo mkoni humo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi boti hizo kwa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mara,Mwakilishi wa mkuu huyo wa majeshi ya ulinzi nchini,kanali Ores Shawa,amesema jeshi la wananchi limeunda kikosi maalum cha ulinzi wa rasilimali katika ziwa hilo ikiwa ni pamoja na kupambana na uvuvi haramu na vitendo vya biashara ya magendo na uharamia ndani ya ziwa hilo.

Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Mara, na wilaya ya musoma,wakizungumza baada ya kupokea boti hizo na kikosi cha askari wa majini watakaotumika kufanya shughuli za doria na ulinzi wa rasilimali katika ziwa hilo,wamemshukuru mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini kwa kutekeleza agizo la rais kwa vitendo.

Chanzo: ITV
 
ila kupeleka meli za kubeba raia kutoka kisiwa ki1 kwenda kingine aah, wakerewe wanalia na nyehunge tu

nitakuunga mkono pale utakapoacha chuki, ubaguzi na visasi
 
Back
Top Bottom