funaku
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 38,534
- 31,198
Hii ni ishara kuwa bado kutakuwa na safari ndefu ya mkanganyiko ndani ya Venezuela. Jeshi tiifu kwa Maduro. Wapinzani hawakubaliki na wananchi
Makamu wa Rais anakosa nguvu za kisheria kufanya makubaliano yoyote.
Yaani ni kama Kongo nyingine hivi.
-------------------
Jeshi la Kitaifa la Venezuela limetoa tamko rasmi likilaani vikali kile ilichokitaja kuwa utekaji nyara wa rais Nicolás Maduro Moros na mke wake Cilia Flores, tukio lililodaiwa kutokea Januari 3, 2026, na kuhusisha mauaji ya walinzi wake, wanajeshi na raia wasiokuwa na hatia.
Katika tamko hilo, Wizara ya Ulinzi imesema Mahakama ya Juu ya Katiba imemteua makamu wa rais Delcy Rodríguez kuwa rais wa mpito, huku serikali ikitangaza hali ya hatari ya usalama wa nje nchini kote.
Jeshi limesema litaendelea kuhakikisha utawala wa nchi, kulinda amani, kudumisha usalama wa ndani na kukabiliana na kile ilichokiita uchokozi wa kibeberu, likisisitiza kuwa lipo tayari kwa ulinzi wa taifa, uhuru na mamlaka ya Venezuela.