Jeshi la Sungusungu limeishia wapi?

Muyobhyo

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
8,149
6,544
Hivi jeshi la Sungusungu liliishia wapi? Nakumbuka nikiwa Mwanza kulikuwa na jeshi la Sungusungu la Kasamwa, lilikuwa ni moto wa kuotea mbali. Lilikuwa linafanya kazi kwa weledi sana. Ni nini kilifanya mpaka Sungusungu ipotee, manake walisaidia sana Kanda ya Ziwa kuzima uhalifu.
 
Hahah eti jeshi la singusungu.
Hivi nataka kujua Tanzania kuna majeshi mangapi?
Maana mara JESHI LA MGAMBO mara JESHI LA WOKOVU kama hivo jeshi la sungusungu...
Yani wanatuchanganya
 
Hahah eti jeshi la singusungu.
Hivi nataka kujua Tanzania kuna majeshi mangapi?
Maana mara JESHI LA MGAMBO mara JESHI LA WOKOVU kama hivo jeshi la sungusungu...
Yani wanatuchanganya
hili jeshi lilikuwa ni hatari sana, liliweza kufanya kazi kuliko hao polisi wa chama na jamii, liliweza kuzuia ujambazi kanda ya ziwa, nakumbuka nilikuwa mtoto miaka hiyo ya 80's
 
hili jeshi lilikuwa ni hatari sana, liliweza kufanya kazi kuliko hao polisi wa chama na jamii, liliweza kuzuia ujambazi kanda ya ziwa, nakumbuka nilikuwa mtoto miaka hiyo ya 80's
Na jeshi la mgambo ni lipi? Sungusungu walipugwa marufuku kipindi fulani eti kwa uonevu
 
Back
Top Bottom