Uchaguzi 2020 Jeshi la polisi wilayani Mvomero Mkoani Morogoro wamesimamisha msafara wa mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba

CUF Habari

Verified Member
Dec 12, 2019
221
250
Screenshot_20200911-160849.png
IMG_20200911_160714_382.jpg


Jeshi la polisi wilayani Mvomero Mkoani Morogoro wamesimamisha msafara wa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba ukitokea kata ya Kimamba kuelekea Kilosa kwajili ya kufanya mikutano yake ya kampeni.

Kufuatia hali hiyo mgombea urais huyo anasikitishwa na kitendo cha Jeshi la Polisi kuendelea kutumika na chama cha CCM na kueleza kuwa hali hiyo ni wazi kuwa panakuzuiliwa kufanya shughuli za kisiasa wilayani Kilosa kwani hata mgombea wao wa ubunge wa jimbo hilo aliwekewa pingamizi na kuondolewa na kubambikiziwa kesi ya kumtishia msimamizi wa uchaguzi.

Profesa Lipumba amesema ni wazi kabisa hakuna demokrasia ya kweli Nchini ikiwa hivi karibuni wakati wakiwa Dodoma na Rais Magufuli alisema kipindi hiki cha kampeni waache vyama vya kisiasa vifanye kampeni bila matatizo na kuwabugudhi ili viweze kurahisisha ufanyaji wao wa kampeni.

''Tulipokuwa tukizindua jengo la uchaguzi Dodoma Rais Magufuli alisema vyombo vya dola visibugudhi vyama vya aiasa kufanya kampeni zake tunashangaa hali hii bado inaendelea

Amesema watawaeleza tume hali ilivyo pamoja na IGP Simon Sirro sababu ratiba zao za kufanya kampeni zinaharibika hivyo watachukua hatua ya kuijulisha tume kwamba ratiba yao inabugudhiwa na kuharibiwa hivyo waweze kuwaelimisha jeshi la polisi waweze kutenda haki.

Mgombea urais huyo amesema tokea ameanza kampeni zake amefanya vizuri tatizo limejitokeza maeneo hayo ya Morogoro Mvomero na Kilosa.

Amesema tume inapaswa kuonyesha makali yake kwa wasimamizi wa uchaguzi na kutolea mfano kuwa wagombea Morogoro wamepita bila kupingwa hivyo lazima tume ionyeshe kuwa inafanya uchaguzi huru na wa haki.

Kwa upande meneja kampeni wa mgombea urais huyo amesema hali hiyo ni ukiukwaji wa haki za vyama vya kisiasa hivyo jeshi lapolisi linapaswa kuacha kutumika na kukandamiza vyama vya upinzani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom