Amefeli vipi kwani yy ndo amewapa silaha na kuwafunza hao alshabib?Hao polisi wanaomlilia Mangu, wamezungumzia na kufel kwake kwenye mauaji ya polisi wenzao na mauaji ya kila siku uko mkuranga? au ni kwa sababu ya 'maslahi yao'
Utadumu waambie wananafuki haoAcheni unafiki watanzania...... una uhakika polisi hawajafurahia yeye kutolewa
Nimemjibu aliyesema mauaji ya polisi ndio chanzoMkuu wamesema issue ni mauaji ya polisi?
HUU NI UONGOHuyu Sirro ni mchumia tumbo fulani hivi. Hazingatii kanuni na taratibu za kazi yake bali hutekeleza kila anachoagizwa na Magufuli hata kama kitakuwa hakiendani na maadili ya kazi yake.
Huwa hatujielewi na tukisemwa tunalialiaNimejifunza kuwa Watanzania tuna sifa ya kuwapenda Viongozi legelege ambao wanaweza kutuvumilai tukifanya vyovyote vile, na kuwachukia Viongozi wachapa kazi.
Bora legelege mwenye haki kuliko mkakamavu asiye na haki. Moyo mwororo wa mtu ni amana ya maisha yake ya duniani na mbinguni.Nimejifunza kuwa Watanzania tuna sifa ya kuwapenda Viongozi legelege ambao wanaweza kutuvumilai tukifanya vyovyote vile, na kuwachukia Viongozi wachapa kazi.
[emoji23]Matamshi haya ya kifedhuli yalitolewa na Magufuli wakti wa kamatakamata ya Watuhumiwa wa Madawa ya kulevya baada ya Wafuasi wa Gwajima na Manji walipokuwa wakiimba mapambio na kusukuma gari!!!
Magufuli alitoa maelekezo ya utata kuwa kama yeye angelikuwa IGP basi gari la Manji lingewekwa rokapu na wale Wanakwaya wote wa Gwajima wangelipelekwa Segerea wakaimbie mapambio huko!!!!!
Haya hayawezi kuchukuliwa kama ni matamshi ya Kiongozi wa nchi mwenye busara baali matamshi ya Mtawala fulani aliye lewa madaraka na aliyejaa kibri na chembechembe za Udiktet!!!
Huyu Sirro ni mchumia tumbo fulani hivi. Hazingatii kanuni na taratibu za kazi yake bali hutekeleza kila anachoagizwa na Magufuli hata kama kitakuwa hakiendani na maadili ya kazi yake.
Nimeicopy kama ilivyo kutoka mtamboni......
Baada ya kufanya mahojiano na askari polisi maeneo mbalimbali ya nchi hii kwa njia ya simu kwa wale wa mbali na wale wa karibu kuongea nao ana kwa ana hasa baada ya utenguaji na uteuzi wa mkuu mpya wa polisi IGP , askari wengi ambao niwazoefu na wamefanya kazi na viongozi hawa wote wana kiri kwamba utenguzi huo umewashtua na wengi umewaumiza sana
Wanadai kwamba Mangu alikuwa mtetezi wao mkubwa sana na amewatetea askari wake walio chini yake kwa nguvu kubwa sana ikiwa ni pamoja na kuihimiza serikali kuwaboreshea maslahi yao na mahitaji yao mbalimbali, ingawa kuna baadhi serikali ilikuwa ikilega lega kuyatimiza lakini Mangu alijitahidi sana kufuatilia.
Lakin pia wamedai Mangu ni mtu mwenye misimamo dhabiti na anayejua vema kusimamia maadili na miongozo ya kazi yake kikamilifu, asiye yumbishwa , asiye ingiza siasa katika kazi au yupo radhi akae kimya na asiwe muongeaji kabisa pale anapo ona kuna mbinu zinazo kiuka madili ya kazi yake na kama mbinu hizo zipo juu ya uwezo wake kimaamuzi
"Unajua kaka huyu jamaa kwakweli sisi kama askari tulikuwa tunampenda sana maana ni kiongozi aliye kuwa akitujali sana na ametupigania sana serikalini ili tupate baadhi ya stahiki zetu kwakweli jamaa ametufaa sana ila ni basi tu kaka maana huyu mwingine kisha ingizwa kwenye siasa yaani daah sijui lakin ila nimeumia sana lakin sisi hatuna tatizo kaka sisi ni punda tu yeyote anaye kabidhiwa mjeredi kutuongoza sie tutavuta mzigo tu hahaaaa" alisikika afande mmoja akitoa yake ya moyoni huku akimalizia na kicheko
Lakin pia walio wengi wamemuongelea Sirro kuwa hana shida katika utekelezaji wa majukumu yake lakini huwa si mtu anae weza kusimamia misimamo ya kazi yake na kwa sasa amepoteza ule u Sirro aliokuwa nao hapo zamani, wamemuingiza kwenye siasa kinguvu,, ila naye si mbaya ingawa hatujui akipewa madaraka makubwa hayo atakuwaje lakin kwa hali ilivyo sasa na utawala huu wa sasa askari wengi wame hofia kufanya kazi kisiasa zaid kuliko kuzingatia kanuni ,taratibu, miiko na weledi wa kazi yako
Mleta mada anasingizia wenzake, kumbe yeye ndo analia. Sasa tochi za vichakani marufuku. Mangu alikuwa kama picha tu. Kila siku utasikia Siro na Mpinga kama wao ndo walikuwa Jeshi la Polisi. Magu anaona hadi kwenye soksi.Acha uongo,mbona mi nimepita makao yao makuu leo sijaona polisi yeyote akilia?
Ni maslahi tu kwa sasa, uzuri/thamani ya mtu au kiongozi si kwa anavyotii kiapo alichoapa na wajibu alioukubali bali kwa namna anayosimamia maslahi na hasa ya kifedha ya anaowaongoza. Kiongozi tulipofikia hapimwi kwa wajibu wake ni kwa maslahi binafsi ya anaowaongoza. Tunaliona hili mahospitalini,serikalini na hata kwenye sehemu za kutulea kiroho. Ni kitu kibaya sana na kinapelekea watu kutafuta popularity kwa kupitia watu wachache huku wakiwaumiza na kuwasaliti wengi zaidi.Hao polisi wanaomlilia Mangu, wamezungumzia na kufel kwake kwenye mauaji ya polisi wenzao na mauaji ya kila siku uko mkuranga? au ni kwa sababu ya 'maslahi yao'