Jeshi la Polisi Tarime latoa msaada wa chakula na maji kwa familia ya mbunge wa Tarime John Heche

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Tarime. Siku chache baada ya mkazi wa Tarime, Suguta Chacha kufariki dunia akiwa mikononi mwa polisi, familia yake imekataa kupokea msaada wa chakula kilichotolewa na ofisi ya kamanda wa polisi, Kanda Malumu ya Tarime/Rorya.

Chakula hicho kilitolewa na jeshi hilo kwa ajili ya shughuli za msiba wa Suguta ambaye ni ndugu wa Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche aliyefariki Aprili 27 akiwa mikononi mwa polisi.

Msaada huo wa kilo 100 za mchele, unga kilo 100, maji ya kunywa katoni 20 pamoja na sukari uliwasilishwa msibani hapo jana na Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Henry Mwaibambe lakini ulikataliwa.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo Kamanda Mwaibambe alisema: “Tuliache kwa sababu halina maana tena na tunapenda liishe salama.”

Katibu wa ukoo wa Suguta, Chacha Heche alisema familia hiyo iko tayari kupokea msaada wa Kamanda Mwaibambe kama mtu binafsi kutokana na jinsi alivyoshirikiana nao tangu mauaji hayo yatokee, lakini haitapokea msaada wa polisi kama taasisi.

“Tutapokea msaada kutoka kwa yeyote mwenye mapenzi mema lakini siyo taasisi ya Jeshi la Polisi. Tayari tumechanga zaidi ya Sh5 milioni kati ya Sh8 milioni zinazohitajika kugharamia mazishi ya ndugu yetu,” alisema Heche.

Alisema familia inaheshimu na kutambua jinsi Kamanda Mwaibambe anavyoshughulikia tukio hilo na itashirikiana naye na kumkaribisha katika mazishi kama mtu binafsi na siyo kwa kofia ya polisi.

Katibu huyo wa ukoo wa Suguta, alisema marehemu atazikwa kesho baada ya ndugu kujiridhisha na hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi.

Suguta anadaiwa kufariki dunia baada ya kuchomwa visu na askari polisi, William Marwa (50).

Marwa alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime juzi na kusomewa shtaka la mauaji.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Mwani Mrisho alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Aprili 27 ambako alimuua Suguta (27) kwa kumchoma na kisu.

Tukio hilo lilitokea usiku wa siku hiyo baada ya Suguta na mmiliki wa baa kukamatwa na polisi waliokuwa doria. Hata hivyo, ndugu wa Suguta walipokwenda kumuangalia siku inayofuata waliambiwa amefariki na mwili upo mochwari.
MCL
 
Jamani wakati mwingine tuache ushamba kosa katenda mjinga flani na yuko under custody!! Unakataa msaada Wa nia njema tu!
Nadhani unakumbuka sakata la Akwilina (R.I.P), kama unakumbuka mpaka lilivyoisha utafuta hii comment yako. Usishangae hata huyo aliyepo custody akaachiwa huru siku za usoni, au wewe ni mgeni nchi hii?
 
Hawanaga aibu hawa,wakiua tu wanajifanya kimbelembels kuhudumia msiba..I am sure marehenu anazikwa na hicho kinyongo,maana angekuwa inaweza kuamka akasema jambo angewafukuza
 
Mimi sijawahi kuona mkurya anayeendeshwa na tumbo kama huyu Kichonge. Siku zote ni mtu wa kuimba nyimbo za sifa na mapambio kwa serikali hata pale isipostahili.

Kichonge unapaswa kutambua familia, nchi ama dunia haiwez kuendelea kwa watu kusifia tu. Pia angalia muktadha wa tukio kama hili unapotosha ilhali kuna watu wenye majonz ya kupotez mpendwa wao. Nani kakunyang'anya hekima ndogo tu za ubinadam kuwa msiba hauchangaman na siasa?
 
Tarime. Siku chache baada ya mkazi wa Tarime, Suguta Chacha kufariki dunia akiwa mikononi mwa polisi, familia yake imekataa kupokea msaada wa chakula kilichotolewa na ofisi ya kamanda wa polisi, Kanda Malumu ya Tarime/Rorya.

Chakula hicho kilitolewa na jeshi hilo kwa ajili ya shughuli za msiba wa Suguta ambaye ni ndugu wa Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche aliyefariki Aprili 27 akiwa mikononi mwa polisi.

Msaada huo wa kilo 100 za mchele, unga kilo 100, maji ya kunywa katoni 20 pamoja na sukari uliwasilishwa msibani hapo jana na Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Henry Mwaibambe lakini ulikataliwa.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo Kamanda Mwaibambe alisema: “Tuliache kwa sababu halina maana tena na tunapenda liishe salama.”

Katibu wa ukoo wa Suguta, Chacha Heche alisema familia hiyo iko tayari kupokea msaada wa Kamanda Mwaibambe kama mtu binafsi kutokana na jinsi alivyoshirikiana nao tangu mauaji hayo yatokee, lakini haitapokea msaada wa polisi kama taasisi.

“Tutapokea msaada kutoka kwa yeyote mwenye mapenzi mema lakini siyo taasisi ya Jeshi la Polisi. Tayari tumechanga zaidi ya Sh5 milioni kati ya Sh8 milioni zinazohitajika kugharamia mazishi ya ndugu yetu,” alisema Heche.

Alisema familia inaheshimu na kutambua jinsi Kamanda Mwaibambe anavyoshughulikia tukio hilo na itashirikiana naye na kumkaribisha katika mazishi kama mtu binafsi na siyo kwa kofia ya polisi.

Katibu huyo wa ukoo wa Suguta, alisema marehemu atazikwa kesho baada ya ndugu kujiridhisha na hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi.

Suguta anadaiwa kufariki dunia baada ya kuchomwa visu na askari polisi, William Marwa (50).

Marwa alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime juzi na kusomewa shtaka la mauaji.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Mwani Mrisho alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Aprili 27 ambako alimuua Suguta (27) kwa kumchoma na kisu.

Tukio hilo lilitokea usiku wa siku hiyo baada ya Suguta na mmiliki wa baa kukamatwa na polisi waliokuwa doria. Hata hivyo, ndugu wa Suguta walipokwenda kumuangalia siku inayofuata waliambiwa amefariki na mwili upo mochwari.
MCL
RPC Mwaibambe ni mtu makini anafaa kwa nafasi za juu zaidi siku za usoni!
 
Hiki ndio polisi wa tanzania na serikali kwa ujumla wanachoweza kufanya kama kupunguza aibu yao pale wanapokuwa wamefanya mauaji ya wazi bila kificho.

Huu ni udharirishaji wa hali ya juu kabisa, kama kweli huyo kijana alikuwa ni muarifu basi hapakuwepo na haja ya wao kujipendekeza kwenye familia ya wafiwa, lakini kwa sababu wanafahamu kabisa walimuua mtu asiyekuwa na hatia basi ndio maana wana jikosha kosha kwa wafiwa.

Cha ajabu baada ya wao kufanya hivi hakuna indictment yoyote itakayofuata kwa hao polisi wauaji na wakati hiki kitendo tu cha wao kujari mazishi kinaonesha yule kijana alionewa.
 
Jamani wakati mwingine tuache ushamba kosa katenda mjinga flani na yuko under custody!! Unakataa msaada Wa nia njema tu!
Kwani wamesema wanataka msaada wao?
warudishe roho ya marehemu.
KUTOA MSAADA NI DHARAU.
 
Taarifa nilizozithitibisha familia imekataa msaada wowote kutoka kwa Polisi kupitia RPC wao.

Achana na hizi propaganda uchwara.
Propaganda zipi hapa? Mbona kilichosema ndo na wewe umerudia japo kwa ufupi?
 
Hakika tutavuna tunachopanda.Uchama,ukanda,ubabe,hofu,dhuluma,dharau,biashara haramu ya binadamu nk.
 
Back
Top Bottom