Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 33,612
- 40,158
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linaendelea na Upelelezi wa tukio la kupotea kwa Padre Camillus Nikata wa Jimbo kuu Songea ambaye pia ni Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) Mwanza.
Akiongea Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamisha Msaidizi Mwandanizi wa Polisi (SACP) Marco G. Chilya amesema kuwa Padri Nikata alifika Songea tarehe 03.10.2025 akitokea Dodoma huku akiwa na mhadhili mwenzake ambaye ni Padre wa Jimbo la Songea na kufikia katika nyumba ya Mapadre, St. Shanney, Ilipofika tarehe 07.10.2025 majira ya jioni Father Nikata alionwa na padre mwenzake huko Mtaa wa Kanisani akiwa na kibegi kidogo Mkononi akielekea Stendi ya zamani ya Mabasi Mfaranyaki ambapo tokea tarehe hiyo hakuweza kurudi mahali alipofikia jimboni.
Hata hivyo uongozi wa Kanisa hilo na Mapadre wenzake waliendelea na Juhudi za Kumtafuta sehemu tofautitofauti ambazo walisadiki kuwa atakuwepo lakini hawakufanikisha kumpata ndipo ilipofika tarehe 09.10.2025 waliweza kutoa taarifa ya kutoonekana kwa Father Nikata tangu tarehe 07.10.2025.
Pia Soma: Kanisa Katoliki latoa taarifa ya "kutoonekana" kwa Padre Camillus Nikata wa Jimbo Kuu la Songea