Jeshi la Polisi Manyara latawanya maandamano ya wanawake

Jeshi la Polisi Manyara latawanya maandamano ya wanawake

Huey freeman

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2013
Posts
593
Reaction score
248
babati.jpg

Jeshi la polisi mkoa wa Manyara limelazimika kutawanya maandamano ya zaidi ya wanawake miambili kutoka kata ya maisaka waliyoandamana kwenda ofisi ya mkuu wa wilaya ya Babati kwa madai ya kupinga hatua ya baadhi ya madiwani kuunga mkono mafisadi wa ardhi na kumfanyia fujo mbunge wa viti maalum mkoa wa Manyara Paulina Gekuru anayetetea ardhi ya wananchi iliyouzwa kwa wawekezaji kinyemera ili irudishwe kwa jamii.

Baada ya amri hiyo wanawake hao walilalamika kuwa awakutendewa haki kwani tabia ya baadhi ya madiwani kutetea wawekezaji katika ardhi imekuwa sugu na baadhi yao wanahusika katika kuuza ardhi lakini pia hata baada ya mbunge huyo kuvamiwa na kuchaniwa nguo alifikisha taarifa hiyo katika vyombo vinavyo husina na hakuna hatua inaliyochukuliwa ndiyo maana wameamua kupeleka kilio hicho serikalini.

Akizungumzia sakata ilo mbunge huyo wa viti maalum Chadema mkoa wa Manyara Paulina Gekuru amesema anasikitishwa na tabia ya baadhi ya viongozi wenzake kupinga utetezi wa ardhi ya umma kwani hiyo inaonesha jinsi gani watendaji wanavyo jali maslahi binafsi lakini yeye atoacha kutetea wanyonge hata kama wataendelea kumfanyia fujo.

Chanzo:ITV
 
Katika kile kinachoonyesha uelewa mdogo na taaluma ndogo ya uongozi, mbunge wa viti maalum manyara amedai kwamba kwa wadhifa wake wa kibunge basi hapashwi kupekuliwa mahali popote hata akiingia kwenye ndege!: amesema hayo ktk maandamano yaliyozuiliwa na polisi manyara. My take, mbunge huyu hajui haki na wajibu wake. pia haka kamtindo kwa kuandamana kijinga polisi wafanye kweli kwa hawa wenye kimbelembele
 
Kwa serikali ya ccm wawekezaji wanaowapa 10% wana haki kuliko wazawa wa nchi hii wananchi amkeni tuiondoe
ccm ili tupate haki zetu za kumiliki rasilimali zetu
 
Katika kile kinachoonyesha uelewa mdogo na taaluma ndogo ya uongozi, mbunge wa viti maalum manyara amedai kwamba kwa wadhifa wake wa kibunge basi hapashwi kupekuliwa mahali popote hata akiingia kwenye ndege!: amesema hayo ktk maandamano yaliyozuiliwa na polisi manyara. My take, mbunge huyu hajui haki na wajibu wake. pia haka kamtindo kwa kuandamana kijinga polisi wafanye kweli kwa hawa wenye kimbelembele

Labda ni uelewa mdogo au vinginevyo mi sijui sana. Ila tatizo hapo ni huo uwepo wa polisi at first place. Nadhani kunatatizo la kimaadili kwa polisi wetu. Nadhani pia kuna ushamba wa kutojua wajibu wao na mipaka ya kazi zao.

Katika hali ya kawaida, kazi ya polisi katika maandamano siyo kutawanya maandamano. Ni kuhakikisah maandamano yanafanyika kwa amani na hakuna uvunjifu wa amani wala sheria, hususan mali za kandoni mwa njia waandamanaji wanazopitia. Inashangaza kuwa pamoja na dunia yote kubadilika, pamoja na dunia yote kuhamia kwenye kuthamini uhai, maisha na haki za binadamu, pamoja na nchi yetu kujitia kimbelembele kusaini mikataba ya kimataifa ya kuridhia sheria za haki za binadamu, bado kila kukicha tunaamka na version za ujima kuhusu sheria zetu.

Ni lini tutaelewa kuwa maandamano ni haki ya msingi ya raia katika kupeleka ujumbe amabao anaamini haujawafikia walengwa ipasavyo? Ni kwa nini bado tunapenda kuongoza nchi kama tuko katika miaka ya machifu na watemi? Ni lini na nchi yangu itaacha ushamba huu wa kiuongozi ili watu wote wawe na fursa sawa za kusema, kusikilizwa na kusaidiwa? Na kwani haya mashetani yalitokea wapi na kwa nini bado tunayafuga?

Natoa wito tujifunze kutokana na makosa yetu. Sanduku la kura ni kila kitu, uhuru wetu na sauti yetu. Tulitumie wisely.
 
hao kina mama wameharibiwa na chadema kufanya maandamano.chadema ni wachochezi sana wamewachochea hawa kina mama.polisi manyara wachukue hatua dhidi ya chadema
 
Wanawake ndo wanakuwa mstari wa mbele kuichagu ccm haya ndo madhara yake...wajifunze sasa..!
 
hao kina mama wameharibiwa na chadema kufanya maandamano.chadema ni wachochezi sana wamewachochea hawa kina mama.polisi manyara wachukue hatua dhidi ya chadema

Wewe kweli umevurugwa, toka lini wewe una njaa harafu unachukua chakula unakigawa ili ulale na njaa pasipo sababu husika? Acha unafiki jisafishe mwenyewe kabla ya mwenzako
 
Ni dalili njema wanawake Lazima washiriki kuleta mabadiliko ya kweli.Haya sasa wale wanaosema kila siku chama fulani ni cha wanaume tu waseme tena
 
hao kina mama wameharibiwa na chadema kufanya maandamano.chadema ni wachochezi sana wamewachochea hawa kina mama.polisi manyara wachukue hatua dhidi ya chadema

Acha utahira wewe utawekwa unyumba,Yaani mtu akijitambua nakudai hakiyake nichadema imemtuma,wewe siku ukipata akiri timamu ukajitambua ni Chadema
 
Back
Top Bottom