Jeshi la Polisi limesema linamtaka dereva wa Lissu ili liendelee na uchunguzi wa shambulizi la Lissu

Wadau wa cdm pamoja na Mwenyekiti wenu mkimaliza mbwembwe zenu Mtuletee Yule Dereva aliyeshuhudia Tukio.
Tumieni huu muda vizuri kadri muwezavyo lakini lazima Huyo dereva arudi Tanzania aisadie Police katika Uchunguzi.
Msisahau na vielelezo vya kuthibitisha matumizi ya fedha za Michango ya Mgonjwa.
Jeshi limeingiliwa lime kuwa mdebwedo yaani wanataka kufanyiwa uchunguzi na chadema da musije mukakenuwa wakiwatolea uchunguzi wao hamchelewi kusema ni taarifa si ushahidi
 
Kwanza niseme polisi wetu wamenishangaza sana kwamba hawakumhoji dereva siku ile ile ya tukio. Pale dereva alikuwa anakumbuka kila kitu vizuri sana.

Na hata kama alikuwa anahusika na njama za kumuua Lissu angekuwa hajapata nafasi ya kutunga hadithi nyingine baada ya ule uhalifu kutokufanikiwa. Angetoa taarifa ambazo hazijachujwa na kuzongwa na kumbukumbu baada ya muda kupita.

Lakini hali ndivyo ilivyo hivi sasa. Katika upelelezi wa makosa ya jinai, mtu wa karibu kabisa ndie anaekuwa mshukiwa namba moja.

Mfano, kama mume ameuawa nyumbani au sehemu yoyote ile basi lazima mkewe, marafiki zake wa karibu wahojiwe kwanza na kujiridhisha hawahusiki wakati uchunguzi unapanuka kutafuta washukiwa wengine.

Dereva ndie mtu wa mwisho kuwa na Lissu kabla hajashambuliwa na ana taarifa nzuri za watu na magari yaliyokuwa yanawafuatilia. Pia dereva alisema aliwaona nyuso zao waliompiga risasi Lissu. Hizi ni taarifa za muhimu sana katika huu upelelezi.

Kwa kuwa dereva ana ushahidi mzito kama huu, kumuweka Nairobi na kuzuia mahojiano na polisi ni kuzuia haki itendeke (obstruction of justice).

Kuna watu wanauliza eti kwa nini polisi hawaendi Nairobi kumhoji. Hii hoja haina mantiki. Wanaomhoji shahidi sio mtu mmoja. Ni timu yenye wataalamu wa maeneo mengi.
* Kuna wanaomhoji moja kwa moja.

* Kuna asiowaona lakini wanapima kiasi gani anasema ukweli au anadanganya.

*Kuna wengine watakaomuuliza maswali yatakayopima usahihi wa majibu yake.

*Anaweza kuhojiwa leo halafu akaambiwa arudi baada ya wiki na mtu mwengine akamhoji kivingine kuhakikisha kama kumbukumbu yake ni nzuri.

Huwezi kutegemea hii timu yote ya upelelezi ihamie Nairobi na vifaa vyote wanavyohitaji kufanya haya mahojiano. Kwa hiyo wanaosema kwa nini polisi hawaendi Nairobi kumhoji ni kwamba hawajui nini kinafanyika katika kuutafuta ukweli mtu anapohojiwa.

Kwa kweli wanaomzuia huyu dereva huko Nairobi watakuwa watu wazito sana hapa TZ. Ingekuwa mtu hohe hahe kama mimi saa hizi ningekuwa ndani kwa kuzuia upelelezi (obstruction of justice).
makonda mpaka unakufa hili unalo
 
Back
Top Bottom