Jeshi la Polisi lawakamata makahaba 287 na wateja wao

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata jumla ya watu 287 ambao ni dada poa pamoja na kaka poa katika operation maalum iliyofanyika maneo mbalimbali ya Jiji hilo.

Operation hiyo ilitangazwa na kamishna wa kanda maalum mnamo Tarehe 7 mwezi wa 3 na kuazimia kuwakamata madada poa na makaka poa pamoja na wateja wao ambao watakutwa wakiwanunua.

Katika mkoa wa kipolisi wa ilala operation hii imefanikiwa kuwakamata jumla ya madada poa 51 kutoka katika maeneo mbalimbali yakiwemo msimbazi,Buguruni,na stakishari,pia imewakamata jumla ya makaka poa 12 ambapo 11 wanatokea Buguruni na mmoja kutoka msimbazi.

Mkoa wa kipolisi wa temeke umefanikiwa kuwakamata jumla ya madada poa 22,ambapo changombe walipatikana 12,na mbagala walipatikana madada poa 10.

Aidha katika mkoa wa kipolisi wa kinondoni operation hiyo imefanikiwa kuwakamata madada poa 76 kutoka maeneo ya osyterbay madada poa 49,magomeni 23,na kawe madada poa 4,pamoja na makaka poa 4.

Akizungumza na wanahabari jana makao makuu ya polisi kanda maalum ya Dar es salaam ,Kamishna wa kanda hiyo CP Simon Sirro aliwataka watu wenye tabia kama hizo kuacha mara moja kwani ni kinyume na mila na desturi za mtanzania ambapo amewataka kutafuta biashara nyingine halali za kufanya.
 
Ndio maana mtu wangu hayupoo nimepita kwake nimekuta kufuli daaah nawaonea wivu polisi wale wenzangu na mm watawagonga saaana kipindi hiki daaah wamepunguziwa safari za kutangatanga polisi vijana na wazee wapenda mizigo.huwa tunakutana mipenyoni
 
Hizi Ni Mbinu Za kutafuta rushwa Za kiurahisi, dada poa akitakiwa atoe 50000 atoke huwa hawachelewi kutoka.

Nchi yetu inamatatizo ya kiusalama zaidi kuliko hao dada poa lkn haya pewi kipaumbele. Wengetafuta jinsi gani ya kuzuia ajali zinazopoteza roho nying Za Watz. Majambazi kila kona hawa wangewatumia Kama Ni njia ya kupata taarifa Za kiujambazi Na wakaweza kusajiliwa Na kupatiwa leseni ya kazi yake.
 
mbagala wamekamata 10 tu. / ajabu sana / Mbagala ilitakiwa wakamatwe 500.,kimboka 70.,buguruni hapo stand penye hayo mabaa yenye best kwa ndani 100.,kinondoni 500.,× faini nazo ziongezwe zisiwe 10000. ziwe 250,000/- @.,kama ipo dhamira ya ukweli.
 
Hii mada imekosa kabisa watu wa kulipongeza jeshi la polisi kwa hiyo oparesheni yao. Naona wachangiaji wote wamepaniki vilivyo na kumlaani kamanda siro bila shaka kwa kuwazibia riziki na starehe zao.

Mimi nimeona nibakie neutral bila shaka kwa kuamini kuwa baadhi ya hao wadada wanafanya hiyo biashara kutokana tu hulka na wengine ni shida na changamoto mbalimbali za maisha wanazopitia.

Nina imani aina ya watu wanaofanya hiyo biashara kwa shinikizo tu la maisha, wakipewa ushauri nasaha,elimu ya saikolojia, na wakiwezeshwa na serikali au NGO's ktk vikundi au mtu mmoja mmoja wanaweza kubadilika na kuacha kabisa.

ila hawa wanaofanya kama hulka nadhani ni vigumu sana kubadilika na watabakia daima kwenye jamii zetu maana tangu enzi na enzi walikuwepo(hata kwenye biblia wanaongelewa) na baadhi unaweza ukakuta wanatokea familia zinazojiweza kabisa lakini ndio hivyo tena.
 
Back
Top Bottom