Jeshi la Polisi lapiga marufuku ‘tinted’ kwenye kioo cha mbele ya gari

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,075
17,237
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limepiga marufuku uwekaji wa ‘tinted’ katika kioo cha mbele huku likiwataka wamiliki wote kuondoa mara moja kabla ya kuanza operesheni kwa watakaokaidi agizo hilo.

Hayo yamezungumzwa na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga alipozungumza na Channel 10 na kusema uwekaji wa vioo vya tinted katika vioo vya mbele unawapa shida askari kutambua ni nani aliyepo katika gari husika kwa haraka huku akisema huchangia matukio ya uhalifu.

“Mimi tu niseme kuanzia sasa napiga marufuku wale wote walioweka tinted kwenye magari yao vioo vya mbele watoe mara moja, na sisi tutachukua hatua kali za kisheria kwa wale wote watakaokuwa wameweka tinted kwenye vioo vya mbele, hata pembeni hatuwezi sema lolote lakini naweza sema kwamba anaeweka tinted kioo cha mbele anaficha nini?

Alihoji, alisema Kamanda Mpinga huku akihoji. “Ikumbukwe kwamba sasa hivi yapo matukio kadhaa yanayotokea katika nchi yetu na kama unaweka tinted kwenye kioo cha mbele hivi unaficha nini?



Chanzo: Channel 10
 
Kuna wanaoweka tinted kwenye Wind Screen na Headlights hao ndio siwaelewagi kabisa ..sijui ni ushamba au utoto
 
Tinted ziwekwe nyuma tu kwa ajili ya kuzuia jua kwa abiria unaowabeba hasa wamama wenye watoto wachanga, jua hua linaumiza sana. Pia watu wengine hupenda privacy, unakuta mijitu yote macho kodo kutaka kujua nani anae endesha hiyo vogue, mtu hadi unajishtukia. Ila kwa vioo vya mbele ni kweli inachangia uhalifu, na pia ni chanzo cha ajali kwani side mirror huwa hazionekani vizuri hasa nyakati za usiku.
 
Tinted ziwekwe nyuma tu kwa ajili ya kuzuia jua kwa abiria unaowabeba hasa wamama wenye watoto wachanga, jua hua linaumiza sana. Pia watu wengine hupenda privacy, unakuta mijitu yote macho kodo kutaka kujua nani anae endesha hiyo vogue, mtu hadi unajishtukia. Ila kwa vioo vya mbele ni kweli inachangia uhalifu, na pia ni chanzo cha ajali kwani side mirror huwa hazionekani vizuri hasa nyakati za usiku.


Wee umeelewa KIOO CHA MBELE ni kipi? au unachanganya tu habari hapa..

Kuna Front side windows and WINDSCREEN..!! Wee umejua KIOO cha mbele ni kipi hapo..?
 
Wee umeelewa KIOO CHA MBELE ni kipi? au unachanganya tu habari hapa..

Kuna Front side windows and WINDSCREEN..!! Wee umejua KIOO cha mbele ni kipi hapo..?
Kwani kuna watu wanawekaga tinted kwenye windscreen?! Sikujua hili, mi nimeelewa vioo vya milango ya mbele
 
Sio muda tutapata na maelekezo ya madirisha na milango ya nyumba zetu


Hapa Polisi wanatafuta hela kwa nguvu sana, na wenye magari imeonekana ndio njia rahisi ya kupata mapato, yaani inakera sana

Mwenye gari analipia haya yote ila bado naona serikali hairidhiki

1: Road licence

2: Insurance

3: Driving licence

4: Mafuta, Oil, tyres, spare parts, anayonunua analipia kodi, imo ndani

5: SUMATRA

6: Fire.


Kuwa na gari imekuwa tatizo sana sasa, fine kidogo tu tshs. 30,000 hii ni adhabu kubwa sana sana hasa kwa hali ya maisha ilivyo, yaani ni mtindo wa kutegeana barabarani, yote ni kutafuta mapato kwa nguvu, hii ni mbaya sana sana, miaka yote sijawahi ona TRAFFIC POLICE INAKUWA CHANZO CHA MAPATO kwa nguvu hivi..!! Wenye magari tunaumizwa sana sana na hakuna hata mmoja anatetea.. Yafaa sasa iundwe CHOMBO CHA KUTETEA WENYE MAGARI HASA BINAFSI, NA UMOJA HUO UWE NA MFUKO WAKE WA KULIPIA KIDOGO KIDOGO KILA MWAKA, say tshs. 5,000 kwa mwaka na unakuwa mwanachama, na ukionewa upate kusaidiwa haraka sana, ili mmiliki wa gari binafsi apate haki yake ya kutetewa.. hali imekuwa mbaya sana, kuwa na gari binafsi imekuwa kero sbb ya Traffic, wanatafuta hela kwa nguvu mno mno.. na fine kwa kosa dogo ni kubwa sana tshs. 30,000 hii ni adhabu sana
 
hili tamko limekuja kwa kuchelewa sana unapojenga maadili yanaanzia chini hadi juu ,uwekaji wa tinted kioo cha mbele ilikuwa si sahihi kiusalama ,kimaadili ,pia anaweza kuwa kambeba hata mkeo na akapita ulipo na usione chochote ,napongeza tamko hili.
 
Sielewi kabisa windscreen ikiwekwa tinted inahusiana vipi na uhalifu. Au huo uhalifu unafanywa ndani ya gari? Askari unataka kumuuona aliyepo ndani ya gari si ulisimamishe na kumwambia dereva shusha kioo? au siku hizi wahalifu wanatambuliwa kutoka mbali? Police mnatumia binoculars? Otherwise mtamtambuaje mtu aliyepo ndani ya gari kutokea mbali bila kulisimamisha gari husika?
Nachojua mie. ..wizi mkubwa vitu vinavyoachwa ndani ya gari ndo sababu kubwa ya watu kuweka tinted kuepuka kuvutia wezi. Pia umbea wa uswahilini kutaka kujua kila aliyepo kwenye gari fulani linalopita ndo sababu ya kuweka tinted
 
Back
Top Bottom