Jeshi la Polisi Dar es Salaam RC Makonda asiwatumieni kama ngazi ya Kuhalalisha mapungufu yake yasiyotibika!

UTANGULIZI

Nianze Kwanza kutoa pongezi zangu za dhati kabisa kwa Wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam hasa wale wa Jimbo la Uchaguzi la Ukonga kwa kufanya Uchaguzi ambao kwa kiasi fulani umekwenda kwa amani japo kama kawaida mapungufu ya hapa na pale huwa hayakosekani na ni imani yangu Wahusika watakuwa wanayafanyia Kazi ili siku zijazo yasijitokeze.

Pia nichukue nafasi hii kuweza Kuwapongeza Wagombea wote Yule Mshindi wa CCM na yule wa CHADEMA ambaye Kura hazikutosha. Kwangu Mimi GENTAMYCINE wote hawa ni Washindi isipokuwa mmoja tu ndiyo amepewa dhamana kwa sasa hivyo huyo mwingine asikate tamaa na ajijenge zaidi ili mwaka 2020 iweze kuwa zamu yake kwani binafsi nimemfuatilia kwa umakini na nimeona ana uwezo mkubwa na mzuri tu.

SALAMU ZANGU KWA JESHI LA POLISI HASA KWA MKOA WA DAR ES SALAAM

Nawashukuruni sana kwa jitihada zenu za kila siku za kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa wana Dar es Salaam unakuwa mzuri na kiukweli mnajitahidi kulinganisha na huko nyuma japo bado kuna Kazi kubwa mbele yenu kwakuwa Wanadamu tunatofautiana na kila siku wanafanya Uhalifu wa aina mbalimbali hivyo nanyi mnapashwa mjidhatiti zaidi ili tuzidi kuwaamini na kuwapeni ushirikiano.

SINDANO YANGU YA GENTAMYCINE KWENU JESHI LA POLISI HASA KWA MKOA WA DAR ES SALAAM

Kama kawaida yangu huwa nikianza kwa Kusifu jua kuna ' dozi ' Kali na Kubwa inafuata na hapa nitawaombeni sana radhi Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kwani leo nimeamua kuwatoleeni Uvivu na nitatiririka na kuserereka nanyi ' Kunakotukuka ' ili hiki Kitendo cha ' Kipuuzi ' mlichokifanya msikirudie tena.

Nadhani kwa kilichotokea jana tayari Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam mmeshaingia katika Kundi la Watendaji wenye ' mapungufu ' makubwa ya Kimaadili na Kiuweledi hapa Duniani na nimeanza sasa kupata wasiwasi na aina ya Mafunzo yenu mnayopewa huko Chuoni Kwenu.

Kitendo cha Mapolisi tena wakiwa na Sare ( Uniforms ) zao Kushangilia barabarani huku wakiwa wanajimwagia Soda na kumbeba juu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwangu Mimi GENTAMYCINE naona ni ' Tusi ' kubwa sana kwa Taasisi muhimu kama hiyo ya Jeshi la Polisi.

Hivi kama nia yenu ilikuwa ni ' Kujipongeza ' mlishindwa nini Kujipanga tu na muende mkasheherekee pale Ukumbini Kwenu Police Officers Mess Masaki? Ni nani aliyewaambieni kwamba Kitendo mlichokifanya jana ndiyo kinawapeni Heshima kwa Jamii kubwa ya Wana Dar es Salaam?

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam acheni kufanywa ngazi ya Kupandia na Kujiimarisha Kiutendaji na Kinafasi na huyo mliyekuwa mnashangilia na mnambeba kwani ' Intellectually ' tu mlichokifanya jana ni ' absolutely Unethical and Unprofessional ' na kinastahili ' Kupingwa ' na kisijirudie tena kwakuwa ' Kimewadhalilisha ' mno.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam ni nani aliyewaambieni kwamba ule ' Utulivu ' uliotokea Ukonga umeletwa tu na uwepo wenu pale / kule? Hivi ni nyie tu peke yenu ambao ndiyo mnaratibu Ulinzi na Usalama wa Mkoa huu wa Dar es Salaam? Hivi ufanisi wenu unaweza kukamilika bila ushirikiano wa Sisi Raia wa kawaida na zile Taasisi zingine ' Nyeti ' zenye dhamana ya Ustawi wa Mkoa huu?

Haingii akilini Watu kama nyie mmetoka mtaani kushangilia kulinda Uchaguzi uende vyema huku mkiwa mmebeba Soda zenu mkiwa na Sare lakini wakati huo huo Mtaa wa nyuma yenu tu hapo Kuna Vibaka nao walikuwa wakiendelea Kutiririka na Kuserereka na Simu na Mikoba ya Watu.

Ninachojua tu ni kwamba Polisi hawapashwi Kujipongeza wala Kujisifu kwa lolote lile kwakuwa Uhalifu kokote pale Duniani huwa haumaliziki bali huwa unapungua tu hivyo ' Upuuzi ' wenu wa jana umetulazimisha wenye akili / upeo tuanze ' Kuwadharau ' na msipobadilika ' tutawadharau ' zaidi.

KWAKO MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL CHRISTIAN MAKONDA

Unaweza ukadhani na najua hivi sasa unajua kuwa Mimi GENTAMYCINE nakuchukia ila leo nikuambie ukweli kwamba kama kuna Kijana ambaye namkubali hasa katika Utendaji wake hasa pale akisimamia jambo lake ni Wewe ila una mapungufu ya ' Kipuuzi ' sana ambayo nadhani nimeshawahi Kukuandikia humu / hapa JamiiForums mara kwa mara lakini naona bado hujabadilika. Na isitoshe nakukubali pia kwakuwa Wewe pia ni Simba Sports Club Mwenzangu na pia ni mwana CCM mwenzangu japo Wewe ni Mwanachama na Mimi ni Mshabiki ' tukuka ' kabisa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Makonda unataka GENTAMYCINE nikuseme na nikurekebishe mara ngapi labda uweze Kubadilika? Kwanini unakuwa Kichwa ngumu Kijana mwenzangu? Hizi Sifa / Kiki za ' Kipopoma ' ambazo unazipenda na unaziendekeza zinakusaidia nini? Umerogwa na nani labda kiasi kwamba hushauriki na umekuwa kama Sikio la Kufa lisilosikia dawa?

Ulianza ' Kuwahadaa ' Walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam ili uweze Kufanikisha ' Agenda ' yako na mara baada ya jambo lako la Makontena yako yale ' Kubumba / Kushindwa ' na Walimu nao ' Kukutosa ' Kiaina ukaahana nao na sasa umeamua kuhamishia ' Agenda ' yako na kuanza kutaka Kujenga ukaribu wako na Jeshi la Polisi la Mkoa wa Dar es Salaam ili baadae uwatumie kama ngazi yako katika yale ambayo Wewe kama Mwenyekiti wao wa Kamati ya Ulinzi na Usalama utakuwa unayataka.

Hivi Makonda unaona ni sahihi kabisa kwa dhamana kubwa ya Mkoa uliyonayo ulistahili kubebwa na kushangiliwa vile na wale Mapolisi / Mandata wako jana? Ni kweli Makonda unataka kutuambia kwamba ubora wa Jeshi la Polisi kwa Mkoa wa Dar es Salaam unathaminika au unaonekana tu pale ambapo wamesimamia vyema Uchaguzi katika Mkoa wako lakini siyo kuweza Kukabiliana na Uhalifu mbalimbali ambao kila uchao unatokea hapa Jijini?

Ni lini labda utaiga Uongozi wa Kimaadili, Kiumakini na Kiunyenyekevu wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka? Hivi Makonda ingekuwa ndiyo Wewe umemwagiwa / umepewa zile Sifa alizopewa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mtaka na Mheshimiwa Rais leo hii sisi tungekunywa hata maji hapa Dar es Salaam? Wewe una matatizo gani Makonda?

HITIMISHO

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam nahitimisha kwa kuwaachieni ile Kauli ' Fikirishi ' ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambayo nainukuu hapa...." Ukiona Mtu Mpumbavu anakuja Kwako huku akijua kuwa Wewe una Akili halafu akakuambia ufanye nae jambo la Kipumbavu na Wewe ukamsikiliza na kulifanya basi jua ya kwamba si tu amekuona Mpumbavu zaidi yake bali pia amekudharau mno ".

Siwazuii ' Kunichukia ' ila nawaombeni tu yafanyieni Kazi ' mawazo ' yangu.

Akhsanteni

Nawasilisha.

Mfikishieni tafadhali kwani kiukweli Makonda ' anaboa ' to the extent na bahati mbaya wengine tumeumbwa na mioyo ya kutovumilia na kufumbia macho ' Upopoma / Upumbavu ' ambao kwa bahati mbaya sana badala ya Kupungua sasa ndiyo unazidi tu Kuongezeka kila siku. Kwanini habadiliki? Mbona Wakuu wa Mikoa wengine Mikoani Kazi zao zinaonekana na wala hawana Sifa,Ujivuni na Kimbelembele kama Yeye?

Wewe umewahi kuona wapi duniani Askari Polisi wanashangilia hovyo hovyo kama vile jana? Kile Kitendo kimewadhalilisha mno tu Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam japo wao wanaweza wasiligundue hilo haraka.
Well said, as if ndio waliompigia kura na katangazwa mshindi.Huwezi amini kama kweli hawa walikuwa neutral wanasimamia haki Only in Tanzania
 
Naona kama vile tumerudi nyuma miaka 60 iliyopita, huwezi kuamini kuwa hawa ni walinda amani wa nchi wakiwa na kiongozi wa kiserikali.!!
 
Kwanza kitendo cha kumbeba na kumwagia soda ni kitendo cha utovu wa nidhamu, kuna askari pale anayeweza mbeba sirro au mabeyo na kushangilia kwa kummwagia soda?
Kumbe zile walikua wanammwagia ni soda? Mi nilijua ni mkojo....
 
Kwakweli hata mimi pamoja na mahaba makubwa kwa Polisi lakini kitendo kile kimenikwaza naamini kuna mtu amewapotosha natambua upweke walionao polisi najua wakipata mtu wa kuwafariji huwa wanafarijika sana lkn ni muhimu zaidi kutokufungana na upande wowote.
 
Hata msemeje habadiliki ng’oo , maana kila sakata linalomkuta anakingiwa kifua. Anashida gani !
 
Najiuliza polisi ni wajinga kiasi gani wa kujivunia amani kwenye uchaguzi uliokosa ushindani kiasi kile? Uchaguzi ule hata kama usingekuwa na walinzi wowote ungekuwa na utulivu kwani haukuwa na hamasa baada ya wananchi wengi kupuuza huo uchaguzi. Alichofanya Makonda ni kuwatumia hao mapolisi wasiojitambua kushangalia jambo ambalo hata wasingekuwepo amani ingekuwepo. Yaani ni sawa na polisi kwenda nje ya kanisa siku ya ibada, halafu baada ya ibada wajitokeze kushangalia wamelinda amani!
 
M
UTANGULIZI

Nianze Kwanza kutoa pongezi zangu za dhati kabisa kwa Wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam hasa wale wa Jimbo la Uchaguzi la Ukonga kwa kufanya Uchaguzi ambao kwa kiasi fulani umekwenda kwa amani japo kama kawaida mapungufu ya hapa na pale huwa hayakosekani na ni imani yangu Wahusika watakuwa wanayafanyia Kazi ili siku zijazo yasijitokeze.

Pia nichukue nafasi hii kuweza Kuwapongeza Wagombea wote Yule Mshindi wa CCM na yule wa CHADEMA ambaye Kura hazikutosha. Kwangu Mimi GENTAMYCINE wote hawa ni Washindi isipokuwa mmoja tu ndiyo amepewa dhamana kwa sasa hivyo huyo mwingine asikate tamaa na ajijenge zaidi ili mwaka 2020 iweze kuwa zamu yake kwani binafsi nimemfuatilia kwa umakini na nimeona ana uwezo mkubwa na mzuri tu.

SALAMU ZANGU KWA JESHI LA POLISI HASA KWA MKOA WA DAR ES SALAAM

Nawashukuruni sana kwa jitihada zenu za kila siku za kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa wana Dar es Salaam unakuwa mzuri na kiukweli mnajitahidi kulinganisha na huko nyuma japo bado kuna Kazi kubwa mbele yenu kwakuwa Wanadamu tunatofautiana na kila siku wanafanya Uhalifu wa aina mbalimbali hivyo nanyi mnapashwa mjidhatiti zaidi ili tuzidi kuwaamini na kuwapeni ushirikiano.

SINDANO YANGU YA GENTAMYCINE KWENU JESHI LA POLISI HASA KWA MKOA WA DAR ES SALAAM

Kama kawaida yangu huwa nikianza kwa Kusifu jua kuna ' dozi ' Kali na Kubwa inafuata na hapa nitawaombeni sana radhi Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kwani leo nimeamua kuwatoleeni Uvivu na nitatiririka na kuserereka nanyi ' Kunakotukuka ' ili hiki Kitendo cha ' Kipuuzi ' mlichokifanya msikirudie tena.

Nadhani kwa kilichotokea jana tayari Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam mmeshaingia katika Kundi la Watendaji wenye ' mapungufu ' makubwa ya Kimaadili na Kiuweledi hapa Duniani na nimeanza sasa kupata wasiwasi na aina ya Mafunzo yenu mnayopewa huko Chuoni Kwenu.

Kitendo cha Mapolisi tena wakiwa na Sare ( Uniforms ) zao Kushangilia barabarani huku wakiwa wanajimwagia Soda na kumbeba juu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwangu Mimi GENTAMYCINE naona ni ' Tusi ' kubwa sana kwa Taasisi muhimu kama hiyo ya Jeshi la Polisi.

Hivi kama nia yenu ilikuwa ni ' Kujipongeza ' mlishindwa nini Kujipanga tu na muende mkasheherekee pale Ukumbini Kwenu Police Officers Mess Masaki? Ni nani aliyewaambieni kwamba Kitendo mlichokifanya jana ndiyo kinawapeni Heshima kwa Jamii kubwa ya Wana Dar es Salaam?

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam acheni kufanywa ngazi ya Kupandia na Kujiimarisha Kiutendaji na Kinafasi na huyo mliyekuwa mnashangilia na mnambeba kwani ' Intellectually ' tu mlichokifanya jana ni ' absolutely Unethical and Unprofessional ' na kinastahili ' Kupingwa ' na kisijirudie tena kwakuwa ' Kimewadhalilisha ' mno.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam ni nani aliyewaambieni kwamba ule ' Utulivu ' uliotokea Ukonga umeletwa tu na uwepo wenu pale / kule? Hivi ni nyie tu peke yenu ambao ndiyo mnaratibu Ulinzi na Usalama wa Mkoa huu wa Dar es Salaam? Hivi ufanisi wenu unaweza kukamilika bila ushirikiano wa Sisi Raia wa kawaida na zile Taasisi zingine ' Nyeti ' zenye dhamana ya Ustawi wa Mkoa huu?

Haingii akilini Watu kama nyie mmetoka mtaani kushangilia kulinda Uchaguzi uende vyema huku mkiwa mmebeba Soda zenu mkiwa na Sare lakini wakati huo huo Mtaa wa nyuma yenu tu hapo Kuna Vibaka nao walikuwa wakiendelea Kutiririka na Kuserereka na Simu na Mikoba ya Watu.

Ninachojua tu ni kwamba Polisi hawapashwi Kujipongeza wala Kujisifu kwa lolote lile kwakuwa Uhalifu kokote pale Duniani huwa haumaliziki bali huwa unapungua tu hivyo ' Upuuzi ' wenu wa jana umetulazimisha wenye akili / upeo tuanze ' Kuwadharau ' na msipobadilika ' tutawadharau ' zaidi.

KWAKO MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL CHRISTIAN MAKONDA

Unaweza ukadhani na najua hivi sasa unajua kuwa Mimi GENTAMYCINE nakuchukia ila leo nikuambie ukweli kwamba kama kuna Kijana ambaye namkubali hasa katika Utendaji wake hasa pale akisimamia jambo lake ni Wewe ila una mapungufu ya ' Kipuuzi ' sana ambayo nadhani nimeshawahi Kukuandikia humu / hapa JamiiForums mara kwa mara lakini naona bado hujabadilika. Na isitoshe nakukubali pia kwakuwa Wewe pia ni Simba Sports Club Mwenzangu na pia ni mwana CCM mwenzangu japo Wewe ni Mwanachama na Mimi ni Mshabiki ' tukuka ' kabisa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Makonda unataka GENTAMYCINE nikuseme na nikurekebishe mara ngapi labda uweze Kubadilika? Kwanini unakuwa Kichwa ngumu Kijana mwenzangu? Hizi Sifa / Kiki za ' Kipopoma ' ambazo unazipenda na unaziendekeza zinakusaidia nini? Umerogwa na nani labda kiasi kwamba hushauriki na umekuwa kama Sikio la Kufa lisilosikia dawa?

Ulianza ' Kuwahadaa ' Walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam ili uweze Kufanikisha ' Agenda ' yako na mara baada ya jambo lako la Makontena yako yale ' Kubumba / Kushindwa ' na Walimu nao ' Kukutosa ' Kiaina ukaahana nao na sasa umeamua kuhamishia ' Agenda ' yako na kuanza kutaka Kujenga ukaribu wako na Jeshi la Polisi la Mkoa wa Dar es Salaam ili baadae uwatumie kama ngazi yako katika yale ambayo Wewe kama Mwenyekiti wao wa Kamati ya Ulinzi na Usalama utakuwa unayataka.

Hivi Makonda unaona ni sahihi kabisa kwa dhamana kubwa ya Mkoa uliyonayo ulistahili kubebwa na kushangiliwa vile na wale Mapolisi / Mandata wako jana? Ni kweli Makonda unataka kutuambia kwamba ubora wa Jeshi la Polisi kwa Mkoa wa Dar es Salaam unathaminika au unaonekana tu pale ambapo wamesimamia vyema Uchaguzi katika Mkoa wako lakini siyo kuweza Kukabiliana na Uhalifu mbalimbali ambao kila uchao unatokea hapa Jijini?

Ni lini labda utaiga Uongozi wa Kimaadili, Kiumakini na Kiunyenyekevu wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka? Hivi Makonda ingekuwa ndiyo Wewe umemwagiwa / umepewa zile Sifa alizopewa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mtaka na Mheshimiwa Rais leo hii sisi tungekunywa hata maji hapa Dar es Salaam? Wewe una matatizo gani Makonda?

HITIMISHO

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam nahitimisha kwa kuwaachieni ile Kauli ' Fikirishi ' ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambayo nainukuu hapa...." Ukiona Mtu Mpumbavu anakuja Kwako huku akijua kuwa Wewe una Akili halafu akakuambia ufanye nae jambo la Kipumbavu na Wewe ukamsikiliza na kulifanya basi jua ya kwamba si tu amekuona Mpumbavu zaidi yake bali pia amekudharau mno ".

Siwazuii ' Kunichukia ' ila nawaombeni tu yafanyieni Kazi ' mawazo ' yangu.

Akhsanteni

Nawasilisha.
Mkuu umesimamia kwenye ukweli halisi.Maadili ya Jeshi la Polisi hapa nchini yamehamishiwa kwenye bongo fleva.Huyu mambosasa ndiye ameamua kuisigina PGO kwa kiwango hiki na mkubwa wake wa kazi naye ameridhika kabisa.Mkuu wa mkoa ni mjumbe wa kamati ya siasa ya ccm mkoa hivyo aliwashirikisha polisi kusherehekea ushindi wa ccm kwa kutumia kigezo cha kupongeza kazi.Polisi wameharibu haiba yao.
 
Haya ni miongoni mwa maajabu ya dunia yanayoonekana Tiziiiii... Yajayo yanafedhehesha... Pale unapotaka kujisafisha kwa kujipaka lami....
 
Mfikishieni tafadhali kwani kiukweli Makonda ' anaboa ' to the extent na bahati mbaya wengine tumeumbwa na mioyo ya kutovumilia na kufumbia macho ' Upopoma / Upumbavu ' ambao kwa bahati mbaya sana badala ya Kupungua sasa ndiyo unazidi tu Kuongezeka kila siku. Kwanini habadiliki? Mbona Wakuu wa Mikoa wengine Mikoani Kazi zao zinaonekana na wala hawana Sifa,Ujivuni na Kimbelembele kama Yeye?

Wewe umewahi kuona wapi duniani Askari Polisi wanashangilia hovyo hovyo kama vile jana? Kile Kitendo kimewadhalilisha mno tu Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam japo wao wanaweza wasiligundue hilo haraka.
Kusikia kwa kwenge lazima damu zimtoke kwanza sikioni.
FB_IMG_1537263812374.jpg
 
Sababu mojawapo ya DAB kuwa RC wa Dar ni ku demoralise upinzani.
Siasa za kweli zipo Zanzibar, naielewa vizuri misimamo ya kina Maalim Seif na naiheshimu

Unaposhiriki haramu na kuibariki haram na wewe ni haram tu.

Katika mazingira haya utashangaa kesho Chadema wanashiriki uchaguzi mwingine huku wakitegemea matokeo tofauti, that is insanity.

Siasa zipo Zanzibar tu, huku Tanganyika kuna magenge tu ya wasaka fursa.
 
Inabidi tuendelee kukusanya ushahidi jinsi maonevu yanavyoendelea ili hata tukianza kuchoma matairi barabarani dunia ijue sababu na chanzo
 
Kwanza alianza kuwadhalilisha wababa wa dar, kwa kuwaitA pale ofisini kuwa hawalei familia akasahau kuwa, wanawake hata uwape mamilioni hawatosheki na ndo walivyoumbwa, matokea yake kawaachia wamama maumivu makubwa huku, maana mambo Yameharibika zaidi
Hapa sio sahihi mm ni dume ila wanawake wengi tumewatupia mizigo ya kulea.wanaume tuna tamaa sana ya chini.we need to change.naanza mm
 
Back
Top Bottom