Jeshi la police linahitaji semina juu ya wanawake la sivyo askari wetu watakwisha

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,551
22,097
INTELIJENSIA YA POLICE inahitaji kupatiwa ITELIJENSIA YA MAPENZI ili kuwanusuru askari wetu.
Naomba IGP asipuuzie kuwapa vijana wake semina juu ya mahusiano!
Mahusiano hayaepukiki, lakini yanahitaji elimu ya saikolojia!
Upande Wa JWT kuna sheria maalumu ya kuzuia maafisa kuoa au kuolewa Kwa mda maalum.
Kwa upande Wa jeshi la police kuna tatizo kubwa sana kuhusu "ngono!
Siku moja nilishuhudia askari walimkamata bodaboda aliyekuwa kambeba msichana mrembo, yule bodaboda walimpeleka kituoni fasta, yule Dada wakawa wanamgombania kila askari akawa anataka Namba ya simu! Kwa ahadi ya kumsaidia!
Ipo mifano mingi sana, Dada zetu wanaokamatwa watashuhudia;
Kwa maana hiyo;
Naomba elimu itolewe Kwa hawa askari ili kifo cha mapenzi Kwa askari tusisikie tena!
Kwanza kiinteligensia, wanawake wanaweza tumika kuwapoteza uhai askari wetu endapo maadui wakiamua; jaribu kufikilia kama adui ataamua kumpoteza mkuu Wa kituo furani Kwa kutumia mwanamke atashindwa kweli? It's too easier! Ni kitendo cha kupakiwa dawa kwenye chuchu huku mtu akiwa na kanga moja!!
Nachukizwa sana kuona askari wetu anakufa kizembe namna hii!
Yaani askari aliyepambana na UKUTA, askari aliyeuwa jambazi, askari aliye fuzu mafunzo ya ukakamavu, Leo hii unasikia kafa kwa kanga? Yaani natamani IGP anipe fursa niwape semina hawa vijana.
Tembea mtaani utaona wanavo wabeba makahaba pasipo usalama! Halafu ukipeleleza utasikia huyo Dada anatembea na mkuu Wa................... Kila saa difender linakuja hapo!
****************************
Mbali na mauaji, Kuna visasi, bifu juu ya mapenzi pia kuna jambo kubwa sana la Gonjwa la ukimwi!
HILO JAMBO LA ASKARI KUFA KWA MAPENZI LISHUGHULIKIWE MAPEMA KWA VIJANA WAPEWE SEMINA.
********************************
ASIYE KUPENDA HATAKUSHAURI KAMWE! NALIPENDA SANA JESHI LA POLICE! NI VYEMA KUBADILI TABIA
 
Hilo kweli mkuu maana nakumbuka karibia na njia ya kwenda chuo kikuu udsm kuna grosary moja sasa kulikua na kadada kazuri ikifika saa moja trafiki wanajazana kwamba wemekuja kunywa supublakini shida yao wala sii supu, yaani ipikua kama wale wanyama walinzi wanaolundikana kumsarandia jike 1
 
Wewe uko salama kiasi gani kuwasemea wenzako? Kwani unaonekana kama unatafuta tenda ya kutoa semina elekezi! Mapenzi ni mtu na akili zake zinavyomtuma! By the way ni private business
 
Kule arusha Mwenzao aliamua kubaka, kule tanga mwenzao akauawa na askari mpelelez mwenzake; tabora kajinyonga, songea kanywa sumu, mpwapwa kafumaniwa, katavi kapigwa, ruvuma kajinyonga, kigoma kajiua, Singida kafa kwa maladhi, mbeya kauwawa daaaaaaaaaaaah hawa jama noma sana
 
Nina rafiki zangu watatu maaskari, sijui ni nan anamzidi mwenzie kwa kupiga show. Priority yao ni wanawake...bila shaka huko depo wanachanjiwa jasho la uchi wa mwanamke.
 
INTELIJENSIA YA POLICE inahitaji kupatiwa ITELIJENSIA YA MAPENZI ili kuwanusuru askari wetu.
Naomba IGP asipuuzie kuwapa vijana wake semina juu ya mahusiano!
Mahusiano hayaepukiki, lakini yanahitaji elimu ya saikolojia!
Upande Wa JWT kuna sheria maalumu ya kuzuia maafisa kuoa au kuolewa Kwa mda maalum.
Kwa upande Wa jeshi la police kuna tatizo kubwa sana kuhusu "ngono!
Siku moja nilishuhudia askari walimkamata bodaboda aliyekuwa kambeba msichana mrembo, yule bodaboda walimpeleka kituoni fasta, yule Dada wakawa wanamgombania kila askari akawa anataka Namba ya simu! Kwa ahadi ya kumsaidia!
Ipo mifano mingi sana, Dada zetu wanaokamatwa watashuhudia;
Kwa maana hiyo;
Naomba elimu itolewe Kwa hawa askari ili kifo cha mapenzi Kwa askari tusisikie tena!
Kwanza kiinteligensia, wanawake wanaweza tumika kuwapoteza uhai askari wetu endapo maadui wakiamua; jaribu kufikilia kama adui ataamua kumpoteza mkuu Wa kituo furani Kwa kutumia mwanamke atashindwa kweli? It's too easier! Ni kitendo cha kupakiwa dawa kwenye chuchu huku mtu akiwa na kanga moja!!
Nachukizwa sana kuona askari wetu anakufa kizembe namna hii!
Yaani askari aliyepambana na UKUTA, askari aliyeuwa jambazi, askari aliye fuzu mafunzo ya ukakamavu, Leo hii unasikia kafa kwa kanga? Yaani natamani IGP anipe fursa niwape semina hawa vijana.
Tembea mtaani utaona wanavo wabeba makahaba pasipo usalama! Halafu ukipeleleza utasikia huyo Dada anatembea na mkuu Wa................... Kila saa difender linakuja hapo!
****************************
Mbali na mauaji, Kuna visasi, bifu juu ya mapenzi pia kuna jambo kubwa sana la Gonjwa la ukimwi!
HILO JAMBO LA ASKARI KUFA KWA MAPENZI LISHUGHULIKIWE MAPEMA KWA VIJANA WAPEWE SEMINA.
********************************
ASIYE KUPENDA HATAKUSHAURI KAMWE! NALIPENDA SANA JESHI LA POLICE! NI VYEMA KUBADILI TABIA
pengine Mungu ameonelea alisafishe jeshi letu kwa njia hiyo ili tubakiwe na askari wanaotenda haki kwa raia wote pasipokujali itikadi zozote.
 
Juzi nilikuwa naongea na wadada wanaouza miili yao barabarani wana sema wakikamatwa na Police ili waachiwe na Police wasiowaaminifu fasta wengine wanatoa penzi fasta.

Issue ni condom sasa unakuta hakuna na afande anataka afanye ngono hivyo hivyo bila condom

Wadada wanasema wengine wanakubali na kutoka lockup fasta na wasiokubali basi utabaki under custody hata siku mbili tatu mpaka ndugu zako waje kukudhamini kabla hujapelekwa Mahakamani.

Sasa hapo tunaweza kuwapoteza vijana wetu wengi in case kama kuna issue ya maambukizi ya HIV kwa Jeshi letu la Police.

Kitengo cha elimu kwa jamii kuhusu mahusiano ndani ya Jeshi la Police kiwasaidie vijana wake ktk mahusiano kupunguza vifo lakini na kujikinga na HIV.
 
Back
Top Bottom