SI KWELI Jeshi la Marekani limetangaza kifo cha Benjamin Netanyahu

SI KWELI Jeshi la Marekani limetangaza kifo cha Benjamin Netanyahu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
1773904926399.jpeg
 
Tunachokijua
Karibuni kumekuwepo na taarifa nyingi zisizo za kweli zinazosambazwa mtandaoni zikidai Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amefariki dunia. Mfano rejea taarifa hii iliyohakikiwa na JamiiCheck ikiwa na madai kama hayo lakini ilibainika kuwa ni uzushi.

Ukurasa wa Kanyamala media umechapisha taarifa ukinukuu ukurasa iliodai kuwa ni wa Jeshi la Marekani kuwa umetangaza kifo cha Benjamin Netanyahu kupitia mtandao wa X.


Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia nyenzo za kidigitali umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani haijatolewa na jeshi la Marekani.

Aidha ukurasa ulionukuliwa kutoka mtandao wa X si ukurasa rasmi wa jeshi la Marekani. Kupitia kurasa zake jeshi hilo halijachapisha taarifa yoyote kuthibitisha kifo cha Netanyahu.

Aidha ukurasa huo umetengenezwa mwezi Machi 2026 tofauti na ukurasa rasmi ambao umekuwepo katika mtandao wa X tangu mwezi Septemba 2007.


Aidha X inatumia ishara za utambulisho wa picha kama vile vibandiko na alama za tiki kwenye wasifu wa akaunti ili kutoa maelezo zaidi kuhusu — na kusaidia kutofautisha — aina mbalimbali za akaunti. Baadhi ya viashiria hivi huwekwa na X, huku vingine vikichochewa na hatua za mtumiaji.

Alama Zinazowekwa na X

Alama ya Bluu
(Blue checkmark): Inaonyesha mtu au shirika limejisajili kwenye X Premium. Inamaanisha wamelipia huduma hiyo.

Alama ya Dhahabu (Gold checkmark and square profile picture): Ni maalum kwa makampuni na mashirika rasmi.

Alama ya Kijivu (Grey checkmark): Inatumiwa na serikali, viongozi wa nchi, au mashirika ya kimataifa (kama UN).

Beji ya Uhusiano (Affiliation badges): Picha ndogo pembeni ya jina inayoonyesha kuwa akaunti hiyo imeunganishwa na kampuni fulani kubwa.

Kibandiko cha "Automated" (Automated account labels): Huonyesha kuwa akaunti hiyo inajiendesha yenyewe (bot) na si binadamu anayeposti.

Alama Unazojiamulia Mwenyewe

Kejeli na Mashabiki (Parody/Fan and Commentary labels): Lazima uweke alama hii ikiwa akaunti yako inatumia jina la mtu maarufu kwa ajili ya utani au ushabiki, ili usiwadanganye watu.

Kategoria ya Kazi (Professional category labels): Ukibadilisha akaunti kuwa ya "Kitaalamu", unaweza kuchagua maelezo ya kazi yako (kama vile: Mwanamuziki, Mwanasayansi, au Mfanyabiashara).​
Huyo mwamba hao Iran hawamwezi
Atawapiga kadri atavojisikia
 
Habari ya uwongo.
Hivi wanaotengeneza hizo habari za uwongo zinawasaidia nini? Kwanza hakuna account inayoitwa US Military.

it is not true that the US military or any credible authority has announced the death of Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu.
 
Habari ya uwongo.
Hivi wanaotengeneza hizo habari za uwongo zinawasaidia nini? Kwanza hakuna account inayoitwa US Military.

it is not true that the US military or any credible authority has announced the death of Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu.
Japo tangu ikulu yake isambaratishwe tar 2March, hajaonekana tena, hewani
Wengine wanasema alipelekwa Ujerumani kwa matibabu..
Israel wametoa video clip FEKI za kuzugia watu, ila mwenyewe hajaonekana...
 
Back
Top Bottom