Jeshi la Magereza: Taarifa inayosambaa kuwa ni ujumbe wa Lissu kutoka gerezani si sahihi, inapotosha umma

Jeshi la Magereza: Taarifa inayosambaa kuwa ni ujumbe wa Lissu kutoka gerezani si sahihi, inapotosha umma

Hiyo haitoshi. Weka nyingine mpaka uchoke.
Screenshot_20251212-173144~2.png
 
TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la Magereza Tanzania linapenda kuujulisha umma kuwa, zipo taratibu za mawasiliano kwa wale wote waliopo gerezani kwa mujibu wa sheria ambazo hupaswa kusimamiwa na kuthibitishwa iwapo maudhui ya mawasiliano hayo hayakiuki taratibu zilizopo wala kuathiri suala zima la usalama kabla ya kutoka au kuingia gerezani.

Hivyo, taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni ujumbe wa Ndugu Tundu Antipasi Lisu ikidai kwamba ujumbe huo umetoka gerezani sio sahihi bali ni yenye kupotosha umma. Jeshi linawasisitiza wananchi kuacha kutoa taarifa za Jeshi au wale wanaohifadhiwa gerezani zenye mwelekeo wa kupotosha umma.

Pia Soma: Mjumbe maalum wa Tundu Lissu katika msiba wa mzee Mtei

Mwisho wa ubaya ni aibu! Na mwisho huu u karibu mno.
 
Halafu kwani lissu kasema umeandikwa na magereza au kaundika yeye akiwa magereza? Ndio maana sisi waislam tunaambiwa siku ya hukumu kutakuwa na Hakimu wa mahakimu yaani Allah atahukumu kesi zote zilizotokea duniani kwani anajua binaadam tunavyofanyiana hapa duniani
Duniani hapa hamna haki! Tunapeana moyo tu ila ukweli ndiyo huo. Idai, ipambanie na uwe tayari kufa kwa ajili ya haki yako, bila hivyo sahau!
 
Back
Top Bottom