figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Jeshi la Magereza nchini limeanza kuimarisha kujenga upya kiwanda chake cha viatu cha Karanga kilichopo wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro na kuanzisha kiwanda kipya cha sukari katika gereza la Mbigiri mkoani Morogoro.
Ili kufanikisha hilo tayari Shule ya Sekondari ya Bwawani inayomilikiwa na jeshi hilo iliyopo Chalinze,mkoani Pwani imeanzisha mtaala wa masomo ya sayansi ili kuandaa wa vijana wa kufanya kazi viwandani.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa MagerEZA, Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga amesema mikakati hiyo inalenga kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali kutilia mkazo ukuaji wa uchumi kupitia viwanda.
Chanzo: Mwananchi