Jeshi kufanya mazoezi ya kivita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi kufanya mazoezi ya kivita

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kaitaba, Jul 15, 2009.

 1. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kuna tetesi kuwa jeshi linatarajia kufanya mazoezi ya kivita mkoani pwani wiki ijayo,

  Pia inasemekana kuwa yatakuwa niya usiku na mchana, kwa wiki nzima,

  Pia wavuvi wametakiwa kutovua ktk siku hizo zote, familia sijui zitaishi vipi,

  Wenye data zaidi watujulishe, hayo mazoezi ya kivita ni ya nini kwa wiki nzima?
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Du!
  Labda ni kuharibu mabomu zaidi yanayokaribia kuekspaya!
  Si Unajua nchi yetu inaendeshwa na matukio mzee...Ishu ya Mbagala ndo imetuamsha usingizini.
  Acha wafanye bana kuliko kutuulia ndugu zetu na kuharibu majumba yetu.
   
 3. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,810
  Likes Received: 2,514
  Trophy Points: 280
  Yaani kama itakuwa kweli basi wanataka kuteketeza silaha zilizokuwa zimeexpire.

  Verry good idea nahisi wanajipanga na mahakama ya Kadhi
   
 4. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #4
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Kuna waheshimiwa nimewapigia simu muda si mrefu wamenambia watanifahamisha ukweli wa habari hii. Sintosita kuwafahamisha kama ni tetesi ama ni kweli kwani ni vema jamii kuwa na taarifa ya tukio kama hili.

  Regards,

  Maxence
   
 5. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Kwanini wayafanyie Pwani badala ya Tarime na Rorya!(jokes)
   
 6. araway

  araway JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2009
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 498
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  hivi punde nimeona ndege za kivita zikipiga jaramba katika anga la morogoro, sina hakika kama nazo zinahusika katika mazoezi hayo!
   
 7. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Habari ya Morogoro Mkuu?

  Hapa katika kambi ya Kaboya kuna pilikapilika za hapa na pale!
   
 8. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Ni kawaida JWTZ kufanya mazoezi ya kivita kila mwaka(kutegemea na bajeti ya jeshi) yakihusiha commands zote, hii nafikiri ni lile la kila mwaka wandugu. Na tangu nimefahamu kwa infantry wanafanyia Msata mkoa wa Pwani kila mwaka. Na mazoezi ya kila command nayo hufanyika kila mwaka na kila command inapanga yenyewe ifanyie mkoa gani.
   
 9. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hapa tatizo ni njaa itakayowapata wavuvi kwa wiki nzima, kwanini wasifanye siku moja moja badala ya kufanya mfululizo?
   
Loading...