Mhere Mwita
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 235
- 1,275
[HASHTAG]#Nchi[/HASHTAG] imekosa misaada mingi na kusababisha bajeti kukwama kutokana na ukosefu wa utawala bora. Mwaka jana Bodi ya MCC ilitangaza kufuta msaada wa $463m kutokana na kushindwa kwa vigezo vya utawala bora. hiki ni kiasi kikubwa sana, Ni takribani shilingi trilioni1. Kiasi hiki ni kkikubwa sana kuweza kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo nchini.
# Bajeti ya 2016/17 leo tunajadili imetekelezwa kwa kiwango cha asilimia 34% ya miradi ya maendeleo, kiasi cha chini sana. lakini sababu kubwa ni Waziri katembea Ulaya yote kutafuta mikopo na misaada bila mafanikio kwasababu wanaotoa mikopo hiyo wanazingatia kigezo cha utawala wa sheria, kitu ambacho kinavunjwa kila siku katika utawala huu. Leo miradi imekwama kwasababu nchi inaendeshwa na serikali isiohwshimu utawala wa sheria.
[HASHTAG]#Hata[/HASHTAG] wawekezaji na wafanyabiashara wanakimbia kwasababu hakuna mwekezaji makini anayeweza kuleta mitaji kwenye nchi ambayo mkataba unaweza kuvunjwa jukwaani. biashara zinakufa, uwekezaji unazidi kukwama kwasababu wenye mitaji wanaogopa risk ya kuwekeza mitaji yao kwenye nchi ambayo serikali inaweza kuvunja sheria wakati wowote.Hii inaathiri biashara na mwenendo wa uchumi kwa ujumla.
[HASHTAG]#Kibaya[/HASHTAG] zaidi hata vita ya Ufisadi, bado kuna maeneo Rais anaonesha double standards, kuna watu wanavunja sheria wanatumbuliwa, na wengine wanavunja sheria lakini wapo akina Bashite wanalindwa tena kwa vyombo vya dola.
[HASHTAG]#Mkutano[/HASHTAG] uliopita niligusia hapa kuhusu kuvunjwa kwa sheria Finance Act 2012, kifungu cha 29, kinachosisitiza uhamishaji wa shares usifanyike bila malipo ya kodi ya ongezeko la mtaji( capital gain tax), lakini kampuni ya shell imekwepa kodi ya zaidi ya $500m, kiasi ambacho ni zaidi ya trilioni1. hiki ni kiasi kikubwa kinachoweza kujenga reli hiyo ya kisasa kutoka Dar mpaka Moro lakini kwasababu ya vigogo wasiogusika TRA, FCC na serikali kwa ujumla, nchi inapoteza fedha hizo. Huu ni ufisadi mkubwa na sintomwelewa JPM kwa kuachia mamlaka husika bila kuzichukulia hatua kwa kosa la kuruhusu umamishaji wa sheres kabla ya malipo ya kodi hiyo kufanyika kinyume cha sheria ya fedha ya 2012,kifungu cha 29.
[HASHTAG]#Nasema[/HASHTAG] haya kwasababu kampuni hii ya Shell ni very corrupt, juzi hapa imetajwa kwenye majarida makubwa duniani ikiwemo mtandao wa Global Witness kwa rushwa ya $1bn , zaidi ya shilingi trilioni2 huko Nigeria kwa vigogo wa serikali hiyo ili kufanikisha biashara zake. Nani ataamini kama ukiukwaji huu wa sheria hii hapa kwetu haujafanyika kwa nguvu ya rushwa?Utawala bora upo wapi hapa?
# Nataka majibu kuhusu ufisadi huu, maana mkutano wa Januari nilihoji kwenye Kamati ya walipokuja watu wa Fair Competition Commission(FCC), nikawahoji kwann ufisadi ulitokea, wakashindwa kujibu na kuahidi wangejibu kwa maandishi baadae leo tunaelekea nusu mwaka hawajajibu.
# Niliwandikia barua rasmi TRA kutaka maelezo ya ufisadi huu kwa mujibu wa sheria ya Haki, Kinga na Mamlaka ya Bunge ya mwaka 2002, kifungu10, kutaka wanipe taarifa ya kwanini jambo hili limetokea, leo ni mwezi zaidi umepita bila majibu. Na hata Nilipochangia bungeni Januari mwaka huu, Waziri wa Nishati alijibu akikiri tatizo bila kutoa majibu ya kwanini sheria hii imevunjwa. Nataka Serikali hii inieleze kwanini ufisadi huu umetokea na wahusika hawachukuliwi hatua?
# Mwisho naomba nihoji idara ya Utumishi, kwani mkoa wangu wa Singida nimepewa chati ya madeni ya walimu tangu 2013 mpaka 2017, walimu wanadai zaidi ya 2.4bn.kwanini madeni haya hayalipwi kwa wakati? kuna uhusiano mkubwa sana kati ya ufanisi wa walimu na stahiki zao.hawa ni watumishi maskini lakini bado wanaidai serikali kwa miaka bila kulipwa. kwanini?
# Ukweli ni kwamba kuchelewa kuliwapa watumishi madeni yao kwa miaka ni dhuruma. kuna kila sababu sasa watumishi wanapochelewa kulipwa madeni yao serikali ianze kuwalipa na riba kwa miaka ya kuchelewa kwani wanalipwa wakati thamani ya deni lao imeshashuka. kama serikali ikichelewa kulipa madeni ya wakandarasi hata kwa miezi inalipa na riba kwanini ikichelewa kulipa madeni ya watumishi kwa miaka isilipe na riba? hii ni dhuruma kwa watumishi maskini wa nchi hii.