Jery Muro wa TBC anusurika kupata kichapo mjini Mtwara kutokana na sakata la gas.

UTENDE

Senior Member
Jan 20, 2013
126
64
Jery Muro wa TBC amenusurika kupewa kichapo majira ya mchana leo tar.15.05.2013 kutokana na issue ya gas. Kama mujuavyo huyu jamaa anaendesha kipindi chake cha rasilimali gas TBC, leo alikuwepo mjini Mtwara kuchukua maoni kwa wanamtwara juu ya msimamo wao ktk ujenzi wa bomba la gas kutoka Mtwara kuelekea dar. Chanzo cha mtafaruko baina ya wananchi na Jery Muro ni pale Jery alipojaribu kuonesha kuiunga mkono serikali kuendeleza nia yake ya kutaka kujenga bomba la gas huku akijaribu kusema wanamtwara wakubali tu kwan watanufaika km wanavyonufaika wananchi wa Kilwa kupitia mradi wa SONGAS kwa kusanya kodi ya mrahaba wa 0.3%. Bila police kufika mapema kumwokoa story zingekuwa tofauti kbs.
 
na hakome huku ni kazi kwa kwenda mbele na tunasubiria siku ya ijumaa taarifa ya wizara ya nishati na madini GAS KWANZA
 
Jerry ana matatizo makubwa sana, nashaanga wanaomwona shujaa. Nimesoma nae Loyola, Kisarawe Lutheran Junior Seminary na Chuo kikuu cha Dar kabla hajadisco. Dogo yuko cheap sana. Juzi jumapili tulikuwa wote Bagamoyo maeneo ya Adem kiujumla dogo ni kimeo balaa
 
Fafanua ni kimeo kwa mantiki ipi? Kusema tu umesoma nae haitoshi bila kueleza mapungufu gani umeyaona kwake.
 
Huyu Jery Muro ni mnafiki sn kwa kweli, yaani hoja ya walala hoi wa Mtwara na Lindi anajifanya haioni kbs! Na anafanya hivi kwa maslahi yake binafsi na mafisadi waliomtuma kwa lengo la kumislead watanzania na kuhalalisha wizi wao kupitia ujenzi wa bomba la ga, ambapo hata gharama zake wame DOUBLE. Ieleweke kuwa wanaoumia na gharama za mradi huu si wanakusini tu bali ni walipa kodi wote wa kitanzania.
 
The Big show please tupe Habari kamiri nakuaminia Kamanda.Vipi uko Mtwara au umesepa.
 
Wangemtandika basi tu, wamechelewa mpaka polisi wamemwokoa, akawape habari waliomtuma.
GAS KWANZA.
 
Huyu bwana nae aliingizwa mkenge na TBCCM,amejipunguzia hadhi yake aliyokuwa nayo baada ya kushinda kesi, hao hao waliomtesa wqmemteka kifikra, njaa ni mbaya sana....
 
Tatizo la kutojua limit yake.

Yeye kama mwandishi wa habari anapaswa kuripoti anachojibiwa na watu na sio kufanya propaganda za maajabu kwa favor ya wananchi ama serikali.

Na kwa huu uchonganishi wa kidini unaoendelea nchini, tutakapoanza vita vya wenyewe kwa wenyewe ataishia kukosa shavu la kuripoti ccn na dw. Manake atakapotoa maoni binafsi sijui watampa shaba ya wapi!
 
ufffffffffffffff!!!!!!!!!!!
 
Swala siyo kushabikia muro kupigwa swala ni watanzania wote kulaani elementi za vurugu zinazoendelea nchini؛
 
Jerry ana matatizo makubwa sana, nashaanga wanaomwona shujaa. Nimesoma nae Loyola, Kisarawe Lutheran Junior Seminary na Chuo kikuu cha Dar kabla hajadisco. Dogo yuko cheap sana. Juzi jumapili tulikuwa wote Bagamoyo maeneo ya Adem kiujumla dogo ni kimeo balaa

We mwenyewe unaonekana kimeo maana umekuwa naye sehwmu nyingi mpaka last week mlikuwa wote.. So mmeambukizana ukimeo
 
Murro anatumika vibaya, anapaswa kuwa makini sana maana hapa Mtwara anaandaliwa mtego ambao akinaswa atafanyiwa kitu mbaya sana ambayo hataisahau mishani mweka ampaka aniaga dunia. awe makini.
 
Hapa Ntwara ijumaa kutakuwa hakukaliki....vimesambazwa vipeperushi kuutarifu umma usijishughulishe na suala lolote liwe la kiabishara, kijamii n,k mpaka bajeti ya wizara ya Nishati na madini itakapomalizika.......na endapo itasema gesi inatoka basi vurugu kubwa itatokea.............hofu.
 
Swala siyo kushabikia muro kupigwa swala ni watanzania wote kulaani elementi za vurugu zinazoendelea nchini؛

Tunatakiwa kuangalia tulipojikwaa na si tulipoangukia mkuu....wenye nchi(wananchi) washakataa bomba mafisadi wanalazimisha je nani chanzo cha vurugu hapa?
 
Back
Top Bottom