Jerusalem: Vurugu mpya zaibuka katika mji wa Jerusalemu Mashariki

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Sep 25, 2018
1,114
3,768
Baada ya Mpango wa Kusitisha Mapigano kati ya Israel na Hamas kufanikiwa chini ya upatanishi wa Misri,kuna vurugu mpya Zimeibuka kati ya Polisi wa Israel na Waandamanaji wa Kipalestina.

Hiyo inakuja ikiwa kila upande ukidai kushinda vita hivyo. Kundi la Hamas limewataka raia wote wa Palestina kuitumia siku ya leo ya Ijumaa kusherehekea ushindi huo.

Kuanzia Mitaa ya Gaza Mpaka mji unaozozaniwa wa Jerusalemu Mashariki,wapalestina wamekuwa wakipiga kelele za MUNGU MKUBWA huku wakielekea kwenye Msikiti wa AL-AQSA.

Wakati huohuo,vyombo vikuu vya habari nchini Iran Kama IRNA vimedai Wapiganaji wa Hamas wameyashinda majeshi dhalimu ya Utawala haramu wa Wazayuni. Iran imedai itaendelea kuunga mkono mapambano ya wananchi madhulumu wa Kipalestina mpaka pale watakapo fanikiwa kuufutilia mbali Utawala dhalimu na haramu wa Wazayuni.

Chanzo: DW Swahili leo Jioni.

EWE MTANZANIA MZALENDO,SHIRIKI KATIKA SHINIKIZO LA KUWATAKA WATAWALA WA NCHI HII KULETA MCHAKATO WA KATIBA MPYA YENYE UHURU NA UWAJIBIKAJI KWA RAIA NA VIONGOZI DHALIMU.
 
Sa mtu umepoteza watu 230+ na majumba miundimbinu, maji barabara majengo marefu mwenzako kapoteza watu 22 na minir damages unatoka kuahangilia eti umeahinda tukisema kuna watu na viatu tunaonekana tuna gubu
vita ya kagera watanzania wengi walikufa lakin tulishinda vita muda huu israel kama mpole baada ya juhudi za kulimaliza kundi la hamas kwa kuvunja nyumba kufeli
 
Na umesahau wamemaliza na stock ya missile za iron dome ,hardly 2$ billion dollars
 
Yaani wamekufa wanachama wa hammas 150 na viongozi wao na miundo mbinu mingi imeharibiwa na mahandaki ya hammas kama km 100 zimebomolewa na roketi zao 4000 zimezuiliwa wameshinda nini sasa hapo huu utani sasa juzi waislamu wanapiga kelele na kuiombea Palestine inaonewa kwa kichapo inachopewa na Israel

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Sio siri hawa jamaa ni vichaa

Yani badala ya kushangilia vita imeisha wao wanawaza ushindi, sijui ni nani kawadanganya wameshinda maana maisha ya watu wao 232 yamepotea.
Na kwa huu ujinga wao hawatakaa wafanikiwe.Akili yao inaona pafupi Sana.Wameshinda nini Sasa? Walikuwa wanadai nini na wamepata nini?
 
vita ya kagera watanzania wengi walikufa lakin tulishinda vita muda huu israel kama mpole baada ya juhudi za kulimaliza kundi la hamas kwa kuvunja nyumba kufeli
Hiv unaielewa vita ya kagera wewe?....Tanzania tulishinda so kama Palestine unapigwa unashangilia Sisi tuliingia mpaka entebe kwa maana mji mkuu wa uganda hiyo haistishi tukapitiliza mpaka ikulu wapalestina wamepigwa kipigo cha mbwa koko yaani Israel anapiga mpaka anakosa kwa kupiga jinsi Palestine ilivyochakaa....uwege unasoma historia mkuu acha kufananisha wapumbavu wa Palestine na jeshi la ukombozi la tanzania
 
Baada ya Mpango wa Kusitisha Mapigano kati ya Israel na Hamas kufanikiwa chini ya upatanishi wa Misri,kuna vurugu mpya Zimeibuka kati ya Polisi wa Israel na Waandamanaji wa Kipalestina.

Hiyo inakuja ikiwa kila upande ukidai kushinda vita hivyo. Kundi la Hamas limewataka raia wote wa Palestina kuitumia siku ya leo ya Ijumaa kusherehekea ushindi huo.

Kuanzia Mitaa ya Gaza Mpaka mji unaozozaniwa wa Jerusalemu Mashariki,wapalestina wamekuwa wakipiga kelele za MUNGU MKUBWA huku wakielekea kwenye Msikiti wa AL-AQSA.

Wakati huohuo,vyombo vikuu vya habari nchini Iran Kama IRNA vimedai Wapiganaji wa Hamas wameyashinda majeshi dhalimu ya Utawala haramu wa Wazayuni. Iran imedai itaendelea kuunga mkono mapambano ya wananchi madhulumu wa Kipalestina mpaka pale watakapo fanikiwa kuufutilia mbali Utawala dhalimu na haramu wa Wazayuni.

SOURCE : DW Swahili leo Jioni.

EWE MTANZANIA MZALENDO,SHIRIKI KATIKA SHINIKIZO LA KUWATAKA WATAWALA WA NCHI HII KULETA MCHAKATO WA KATIBA MPYA YENYE UHURU NA UWAJIBIKAJI KWA RAIA NA VIONGOZI DHALIMU.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Mkuu unatumia SIM gani kuandika hi habar yako....tuanzie hapo....🥱
 
Sa mtu umepoteza watu 230+ na majumba miundimbinu, maji barabara majengo marefu mwenzako kapoteza watu 22 na minor damages unatoka kushangilia eti umeshinda tukisema kuna watu na viatu tunaonekana tuna gubu
Unajuwa hivi vikundi kwao ushindi au kushindwa ni ile hali ya kupoteza wapiganaji wao au uwezo wa kurusha makombora yao sasa kufa 240 kwao sio issue kwa maana ni nani hao 240 kwa kauli ya Nentanyau alisema hatasimama mpaka ahakikishe kadhoofisha hamas viongozi wao na uwezo wao kurusha makombora kutoa mizizi sasa hilo hakuweza mpaka vita wanasimamisha makombora yanarushwa tu kwa hiyo Netanyau kaenda kinyume na kauli yake Hamas bado wapo sana tu waliokufa wengi ni raia wa kawaida. kama walikuwa wanarusha makombora alfu 3 kwa siku ukawapiga kila siku ili wasiweze kurusha hayo makombora siku zinaisha bado makombora yanaenda tu hapo kuna kitu umekosea ila kipimo ingekuwa walianza na alfu 3 baada ya kipigo wakawa 500 tu unasema yes operation imekuwa na mafanikio lakini haikuwa hivyo kwa goal was not achieved.
 
Wakitaka kujua stock imeisha washambulie tena mbona wao ndio waliomba po
netanyau alisema atahakiki maandaki yote ya roketi yanaharibi sasa akaona kila akishambulia gaza anaishia kuuwa watoto na akina mama huku roketi zikimiminwa kama maji hapo ndo akaomba poo na kuipa lawama iran ha ha ha
 
Back
Top Bottom