Jerusalem embassy act of 1995

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Wadau Jerusalem Embassy Act of 1995 ni Sheria iliyopitishwa na Serikali ya Marekani tarehe 23 Oktoba 1995.

Madhumuni ya kuipitisha Sheria hjyo ni kuanzisha na kugharamia mpango wa kuhamisha Ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.Utekelezaji wa Sheria hiyo ulipangwa uwe umekamilika mwaka 1999.

Vitu vya muhimu kwenye Sheria hiyo.

1.Marekani kuutambua mji wote wa Jerusalem kuwa makao makuu ya Taifa la Israel.

2. Ilipitishwa na idadi kubwa sana ya Maseneta na Wajumbe wa Baraza la wawakilishi.
Maseneta 93 vs 5
Baraza la Wawakilishi 374 vs 37
4. Ilipitishwa na mkutano wa 104 wa Bunge la Marekani ( Congress)
5. Sheria hiyo Ilianza kutumika rasmi kuwa kuanzia tarehe 8 Novemba 1995
6. Utekelezaji wa Sheria hiyo ulitakiwa uwe umekamilika mei 31,1999.
7. Sheria hiyo haikutekelezwa na Marais watatu John Bush, Bill Clinton na Barack Obama.
8. Kabla ya Baraza la Congress kupitisha Sheria hiyo Waziri Mkuu wa Israel Yitzak Rabin na Meya wa Jiji la Jerusalem Ehud Olmet walitembelea Marekani kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya miaka 3,000 tokea Mfalme Daudi alipoutangaza Mji wa Jerusalem kuwa Makao makuu ya Taifa la Wayahudi.
9. Utekelezaji wa Sheria hiyo ukiwahi kusitishwa na Marais waliokuwapo kwa sababu za kiusalama.
10. Sheria inatambua haki ya kuabudu kwa watu wa dini zote katika Jiji hilo.
11.Rais Donald Trump alianza utekelezaji wa Sheria hiyo kwa kuutambua mji wa Jerusalem kuwa Mji mkuu wa Taifa la Israel tarehe 6 Desemba 2017
NB: Tokea 2010 Serikali ya Marekani imeshafungua Ofisi tatu za Kidiplomasia katika Jiji la Jerusalem.
Serikali ys Israel tayari imeshatenga eneo rasmi la ujenzi wa Ubalozi huo wa Marekani Jijini Jerusalem katika eneo linaloitwa Talpiot.
 
Ndiyo maana kwenye Uzi ule watu walimlaani Trump, na USA kwa hatua hiyo.

Niliandika kuwa, Hiyo issue ilikuwa tayari ipo na hata Trump mwaka 2016 alisema ataitekeleza akawa anasubiria budget ipitishwe.
 
Back
Top Bottom