Jerry Muro: Utoto huu wa mbunge Nassari na Lema, Watanzania tuwe wakali. Tutapoteza taifa

Ushauri tu kwa Jerry ni kwamba Watanzania si wajinga kama unavyofikiri. Wewe ulivyotuma zile video za traffic wakipokea rushwa katika barabara ya Tunduma, kuna mtu alisema video hizo zilikuwa feki?? You need to be a bit intelligent. Unajishushia heshima kwa maneno yako ya ovyo ovyo siku hizi. Huna watu wanaoweza kukushauri?
 
Ningelikuwa sikufahamu toka enzi ya Kolila Sec School ungenishika masikio vizuri sana.

Uzuri nakuelewa sana tu, kwa mwenendo huu unachokitafuta utakipata tu.

Usemaji wa CCM naona inakufanya ujitoe akili hata ile uliyonayo, Ubunge wa Hai unaoutamani naona unaanza kuujengea misingi.

Safi sana u have good plan Bro.....

Ni muda wa kila mtu kupambana na hali yake.
 
Trump2 Muro kasema ukweli, tatizo upinzani umekosa dira, basi ni utoto, kulialia tu, kulalamika, kutokujenga ajenda wala dira, basi vurumai tupu, wengine tunasikitika kwa Chademakwanza kutokutoa upinzani wa kweli wenye policies and strategies za kuiongoza nchi! Wamefikia kufanya haya! Raia wanasikitika kweli kweli...
 
Muro dogo acha kutetea kila uozo, unatusikitsha sana sisi wanayanga, hapo ndo naamini we ukua mtu sahihi kwa nafas ile. Mwache mnyeti ajitete yy. Udhaifu wa picha au sauti auwez kukutoa hatiani ukidhibitishwa kua ulihonga. Acha haya mambo jery unajipa aibu sana.
 
Tangu Jerry Muro aanze kuleta mabandiko yake humu JF sijawahi kuona hoja ya kizalendo kutoka kwake zaidi ya kuinyesha itikadi na mapenzi yake kwa Chama na watawala. Yaani Jerry haoni hoja yoyote kwenye madai ta Lema na Nassari! Huyo jamaa ni hatari!

Vv
 
Pole pole umemuona jery muro anataka nafasi yako shauri yako maana haieleweki yupo wapo soka anataka yeye sasa anajileta uku kwenye siasa haya karibu ila jipange kumbuka watu wa siasa tofauti na watu wa soka

Watu wasiasa wengi waelewa wa mambo zana za mbumbu kuwa kwenye siasa zepita uku siyo jangwani mwana chama hata kusoma ajui anapiga kelele anasikilizwa uku siyo kiongozi jipange
 
Jerry Muro amesahau kuweka namba ya simu mwishoni mwa andiko lake ili tumchangie au wakuu wampe nafasi za uteuzi
 
Haya mabandiko ya Jerry nawashauri wale wenye akili zenu msiwe mna-comment chochote.
Waache wenyewe kwa wenyewe wasifiane. Huyu naona anatafuta kazi ya Polepole kwa nguvu sana, bahati mbaya sana hana ushawishi katika hoja zake. Mchunieni ataacha kuandika hizi ngonjera.
 
Muro unaeleweka vema2 mbona sema umegusa yaupinzan ndomana wao hawaguswagi wakatafakar bali hukurupuka nakuanza kutukana watu wa namna hii ole wako uwape nchi uone kama watakubali kukosolewa ndomana hata chama chao nimarufuku kwenda mahakaman ukienda ww sii mwanachama.ndicho chama pekee kinafanya huo upunguan hapa tanzania na Afrca.
Mkuu, yawezekana una hoja, lkn uandishi wako umenifanye nishindwe kujusoma, huna coma wala full stop.

Vv
 
NDUGU Jerry! Usifikirie kwamba kila mchezo ni wa mpira.
kuna michezo mingine siyo ya kubwabwaja kijingakijinga kama ulivyozoea.
Hii ni Siasa hai.
kama unaomba ukuu wa Wilaya au Mkoa tafuta njia nyingine sio hiyo uliyoichagua.
INAONESHA TAYARI UMESHAKUWA NA ELEMENT ZA UPUMBAVU WA AKILI !!
waache wafanye kazi yao ,ww ambayehujuwi kitu kaa kimya JERRY MURO.
 
NIMEANGALIA VIDEO YA LEMA NA MWENZAKE, NA NIMESOMA MAELEZO YA MURO. MURO HAJAKOSEA ILA SISI WANAMAGEUZI TUNA SHIDA YA KUELEWA HARAKA. HATUNA UWEZO WA KUJIONGEZA, HAIINGII AKILINI USHAIDI WALIOSEMA WANAO MIMI BADO SIJAWAELEWA KAMA WANAO MWINGINE WAUTOE ILI SAIDI WANACHAMA WAO TUWAELEWE. RAKINI KWA MAINGIZO HAYA WANATUPA WAKATI MGUMU JAMII

Hata darasani sio wote wanaoelewa kile mwalimu anafundisha, kwa hilo wala sikushangai
 
Anaandika Jerry C. Muro
Dar es Salaam, Tanzania
October mosi, 2017

Nimetazama mkutano na waandishi wa habari wa Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nasari ambao alimualika pia Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Godbless Lema, nikaishia kuvuna hasira kubwa sana. Na kwa hili kwa kweli naomba watakaokasirika wanisamehe.

Mimi ni kijana ninayefanya kazi za upigaji wa picha na utengenezaji wa vipindi na makala mbalimbali (Audio Visual Production). Kwa mara ya kwanza baada ya Mhe. Rais Magufuli kuwapokea madiwani walioamua kuondoka CHADEMA na kuhamia CCM pale Sheikh Amri Abeid Arusha niliposikia kuwa Nasari anasema anaushahidi usio na mashaka na ambao ameupata kwa vifaa maalum alivyovipata nchini Uingereza nilivutiwa sana kwamba nguvu ya teknolojia sasa itamaliza ubishi juu ya biashara ya kununua wanasiasa ili wahame upande mmoja kwenda mwingine.
Tatizo lako Jerry na ccm wengine elimu zenu ndogo sana. Mara nyingi kwa wakwe huwa mnasema mnaeleimnu ya course.Kupata access ya media ahakukufanyi wewe kujiita expert sana . KWa akili yako unadhani kutoka uingereza au lah, kuwa na ubora wa mwisho kabisa au ah kunaondoa hoja kwamba magufuli anahitaji kukaza mwili haswa. Lazima aonyeshe kwa vitendo kuwa hataki rushwa hata ya tuhuma tuu.Itashangaza km wewe na yeye mtapanda jukwaani kuwatetea km vile nyie ni takukuru. Ni ngumu watu wenye njaa zisizioisha km wewe kukubaliana na mimi.Njaa zenu haziwapi time ya kujifunza vitu na kujua.Ni km wapiga deme wa stand.Kwa vile hamjui thamani ya vitu mnavyoharibu au kuchezea ni rahisi kujiita kila majina mengine ni kufuru.Ila bado mtajiiita watoto wa mjini.Waulize wenzio walijiita wa mjini miaka na miaka ila leo bado mji una wenyewe.Wenye kujua kufanya kazi, na wasiojidanganya
Nilikatishwa tamaa na Nasari akiwa na mwenzake Lema waliposema hawatatoa ushahidi huo kwa yeyote isipokuwa wakikutana na Rais, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ama viongozi wa juu waliokuwa wanawataja. Niliona hawa ni wababaishaji kama kawaida yao.
Ndio unataka sema nini hapa wewe?Wababaishaji km ulivyozoea?Au km ccm walivyozoea kufanya mizaha? Ulizoea nini?Umethibitisha vipi kuwa hapakuwa na rushwa?Umesikiliza maneno ya huyo mkuu wa wilaya?.hata jinsi anambembeleza jamaa inajisema yenyewe kwamba ccm imeishiwa kweli kweli, ktk kutaja dau mdomo unakuwa zege haswa. haalfu sijui km amekaa mjini muda mrefu huyu mkuu wa wilaya.Km mkabila fulani huko ambapo,hata kutongoza wanawake huwa wanapata advantage ya ujinga na umasikini
Leo nikabonyezwa kwamba kuna mkutano wa waandishi wa habari na uthibitisho unatolewa, nimefuatilia mwanzo mpaka mwisho na nimeogopa sana, nimeogopa kwa sababu naona tunakokwenda sasa watanzania wote tunafanywa watoto.

Tunaigeuza nchi kuwa ya maigizo na sinema, tunaleta mzaha na taharuki badala ya kujielekeza katika ujenzi wa taifa letu ambalo kwa kweli linahitaji mikono na akili zetu ili litokea hapa lilipo.
Sijaona mtu kama wewe. Sidhani km ulichoandika hapa kina maana kihivyo.The first assumptions ni kwamba wewe ndie una akili sana, pili ni kwamba wewe ndie pekee unaweza jua kweli na uongo, pili unaonyesha kuwa Nassari na Lema ndio wanfanya watu watoto na sio wewe na wengine wenye njaa kali kuliko fisi na akili km wapiga debe wa stand.Hata siti isiyokalika wanataka mtu akae na kulipa hela mengine watajijua wenyewe
Sasa twenda kitaalamu.
Picha zilizotolewa na Nasari zinaonesha zimerekodiwa na kamera ya kificho na kwa hakika aliyekuwa anarekodi anaoneka kabisa ama alitumia kalamu zenye kamera ambazo zinapatikana madukani popote Dar es Salaam hata mikoani ama katumia kamera zilizopandikizwa kwenye vishikizo vya shati.
Hivi vifaa vya kawaida sana na kila anayehitaji anaweza kuvipata, wafanyabiashara wengi wanavyo na huvitumia pale wanapofanya makubaliano na watu mbalimbali ili wasije wakawageuka baadaye. Hata bei yake ni ndogo, mimi nina kalamu yangu nilinunua kwa shilingi 23,500 na inarekodi vizuri.
Unajibu hoja au unaanza udaslam?Kuwa ni vya kawaida?Kawaida ni relative wewe kanjanja. Ni kawaida mjini kula mikate hadi kuichoka ila sio kawaida kila mtu. your guess ni kalamu,ila kuna zaidi ya kalamu. Na hizo kalamu ni nyingi na bei zanatofautiana km ilivyo smartphones. Kuna elfu kadhaa hadi milions kadhaa.Kwa udogo wa akili yako unataka huo upunmbavu wako uwe kweli. By the way hata ikiwa cheap kunaondoa vipi ushahidi kuwa mkuu wa wilaya alikuwa anachezea office?Ajira za serikali zinakuwa rushwa ,tena ya kuua democrasia?
Ama laa aliyerekodi anaweza kuwa ametumia simu ya mkononi.
Matokeo yake ni kuwa ubora wa picha dhaifu sana na sauti haisikiki kabisa kwa uthibisho wa kila kinachozungumzwa. Lakini pia eneo lililotumika kurekodi kuna mwangwi mwingi sana kiasi kwamba ngumu kujua sauti ya aliyekuwa anazungumza.

Kibaya zaidi kwa sababu ya kutumia vifaa dhaifu hata picha zilizorekodiwa hazioneshi sura ya mtu zaidi ya kuonesha traki suti na mikono na kwa kupitapita inaonesha sura ya mtu ambayo ni vigumu kujua ni nani kutokana na mwanga hafifu.
Sasa una unaanza guesswork hujui ni simu ,hujui ni kalamu km yao ya 23,000 ila bado unataka potezea watu muda wakusikilize,wakuamini, wakufutie makosa yako ya logic na weledi. Zaidi ya ubora wa camera pia mwanga una matter, kupiga picture za spy, kuna mara inaweza kuwa shida kupata target ktk mazingira rafiki km mlengwa ndie anayamua wapi pa kukaa
Mbinu hii hutumika lakini hutumika kwa weledi unaokuwezesha kutokuwa na mashaka na Yule unayemrekodi.
Kwa sisi tunaofanya kazi za Audio visual production kuchukua picha Fulani ukaipandikizia sauti ni jambo rahisi sana na mchezo huu unafanywa sana na watengeneza sinema na movie.
Ni umbea tuu unakusumbua na elimu zenu za course. Kufanya editing ya studio hakumaanishi ni mtaalamu wa kuchukua video. ushahidi gani unataka mkuu wa wilaya kaonekana na jinsi anaongea kishamba km katoka kishapu siku hiyo hiyo na gari a mjomba.Ulitaka umwone mpiga picture?Pengine hujui mazingira ya kuoata picture hadi ya mpigaji na maana ya siri
Unaweza kuchukua sauti ya Juma ukaipandikiza kwenye picha ya Hamis.
Sasa nataka kumwambia hivi Nasari, taharuki aliyoitengeneza kwa watanzania kwa kutegemea ataonesha vipicha hivyo vilivyopigwa na simu ya mchina ama vikamera vya kalamu ni utoto mkubwa sana. Hao anaosema ni akina Mnyeti na Mkurugenzi na Katibu Tawala wa Meru hakuna mahali wanapoonekana kwa uhakika kwamba wamesema unachodai, lakini pia hata hizo sauti zao hazisikiki kwa uthibitisho wa uhakika kuwa wasemaji walikuwa wanasema nini.
Kwa akili za CCM mnadhani kutoonekana pesa ikitolewa ,ndio ushaidi, ila mnasahau alichoongea cha kuonyesha kuwa ajira za serikali ya ccm zinatolewa kwa namna hiyo ni uvunjifu wa katiba.Ajira hazikupaswa kutolewa kwa ubaguzi,achilia mbali kuwa chambo ya kubadili watu dini,chama, au chochote. Pia Chadema walipaswa mlinda mtu wao, kwa vile angepokea rushwa asingekuwa salama takukuru, mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni wahalifu. Pia kufikia kupokea hela kungehatarisha usalama wa anayetaka pewa rushwa.Asingekuwa na sababua ya kukataa kwa kiasi cha kumridhisha huyo mkuu wa wilaya. Kwa kaili yako hukuona huyo dogo alivyokuwa nakwepa kufikia kupewa hela,ndio maana alikuwa akiongeza dau, na kuwapa kesho ingawa wao waikuwa wakikomaa aandike hapo hapo hata stationery hapo nje.CCM makenge kweli kweli, kwanza hawana hela, pili hawajui issue za siri km hizo sio za kupeleka stationery, tatu wana mtetezi km wewe.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari Nasari anafanya janja ya nyani eti anapandisha sauti za hizo video halafu anazima na kuzungumza yeye kwamba wamesema hivi na hivi na hivi. Utoto na ujinga wa hali ya juu.

Mhe. Nasari na mwenzako Lema, tupeni huo ushahidi usio na mashaka, hizi takataka mnazotaka kupanda ndege kuja kuzileta kwa Kamishna Mkuu wa TAKUKURU ni upuuzi na usanii wa kupigiwa mfano, na I wish ningekuwa mimi ndio Kamishna Mlowola mkikanyaga tu ofisini kwangu nawakamata na kuita vyombo vya dola ili muthibitishe madai yenu.
Jery jerry ,wewe ni kanjanja kweli kweli. Alichofanya Nassery ni shaihi zaidi kuliko kuweka hiyo sauti km video.Ni kwamba anatoa maelezo ambayo hata documentary na taarifa za habari zikifika studio huwa zinawekwa maelezo ya maandishi au maneno ili kufikisha ujumbe uiofichika.Angefanya kwa kuedit mngekuja na sababu tofauti.Jerry ujinga wenu ni bahati ya ccm ,ila ni balaa kubwa zaidi. Ushiahidi waliotoa ni mkubwa sana ,badala ya kupoteza muda kujaribu upuuza ni bora ungejiwekeza ktk kuuzuia.Wananchi wanaelewa sana tuu.Na km unataka zaidi , basi huko kwingine ni kwa takukuru na sio kwa raia kufanya uchunguzi. Km takukuru hawawezi ona cha kufanya hapa?Na km wewe na wao wanajiona ni mahakama na kumaliza shauri kipumbavu km unavyoshauri.Ni wazi mnahitaji kutolewa kwa viboko hapo mlipo na sio kwa mazungumzo.Mwehu sio rahisi kumshawishi kwa mazungumzo atapoteza muda tuu
Kwa sababu nina hakika mnajua mnafanya, fanyeni siasa za kileo jamani. Siasa za kuwafanya watanzania watoto ama wajinga sio leo.
Unaongea km mtu aliyeshindwa jibu swali hadharani, ni majibu ya kukata tamaa kw akukosa ushawishi.I wonder unatafuta nini ktk hizi njia. Kwa akili yako wanakupenda sana hao waunaowafanyia kazi? Waulize nduguzo wanavyoumia kwa vile wewe unafanya kazi upande wa shetani ili ule leo tuu ,na ndugu zao wenye kila uwezo waangamie.
Hizo video zenu zinaweza kutengenezwa na mtu yeyote, tunataka utuoneshe video kama zile alizozionesha Jerry Muro alipowapiga wale askari wa barabarani wanapokea rushwa. Picha iwe clear na ambayo mtu akiona anapata uhakika kwamba ile ni hela. Ama tunataka kuona video kama ile ya yule askari aliyepokea rushwa kwa watalii kule Zanzibar.
Kwani ulitaka zinazo jitengeneza zenyewe?Una shida ya akili Jerry. Video zinatengenezwa na mtu kwa kutumia camera.
Nilitarajia kumuona DC Mnyeti akigawa hela kama mlivyodai, nilitarajia kuwaona madiwani wakipokea hiyo hela kama mlivyotuaminisha. Badala yake mnatuletea picha za mashati ya watu na sauti za kupandikiza.
Hakuna hata diwani mmoja mliyemuonesha hapo, na ningekuwa mimi ni diwani ningewafungulia mashitaka ya kunichafua. Ili mkathibitishe hiyo rushwa nilichukua wapi.
Kama ushahidi ndio huu, Nasari anastahili kukamatwa mara moja ili taharuki aliyeijenga kwa jamii aithibitishe. Ama achukuliwe hatua.
Ulitaka jamaa apokee hela ili nae awe ktk list ya wahalifu?Una kili ndogo sana jombaaa. For your info Takukuru walipaswa anzia hapo.Mazungumzo yapo wazi, kila mtu alifuatwa kw amuda wake. Mbaya jamaa kajieleza jinsi alivyowalaghai wengine na pia alichowaahidi hakijatimia kwa vile ccm imefilisika ndio maana inatumia vitu vidogo km ajira, na miradi ya umma. sishangai hata wasanii wema kaanika ccm iliwakopa.Na wewe kumbe unakopwa.Umechoka sana, na hapo umejiweka kitazini siku unawatosa, wanakupiga pini na kufufua ile kesi yako.And this time around hakuna wanasheria watakuhurumia tena
Na kwa kweli mimi sielewi, hivi kweli tunajenga nchi kwa mtindo huu? Kwani Diwani ama mwanachama wa chama cha siasa kuhamia chama kingine tatizo nini? Mbona wanasiasa wanahama kila siku? Wapo wanaokwenda Chadema akina Sumaye, Lowassa, Mgeja, Masha, Ester Bulaya na wengine wengi. Hawa ni wakubwa wakubwa tu. Halikadhalika wapo wanaohama Chadema na kwenda CCM wengi tu wakiwemo hao madiwani kuna shida gani?
Manaake tunatengeneza mazingira kwamba chama kinachostahili kuhamwa ni CCM tu, Chadema hapana.
unaongea marudio km vile wengine hawajui walichosema.Akina Lema na Nassery waliweka wazi kwamba hao jamaa wana haki ya kuondoka,Ila kupewa rushwa na kutoa sabbau za uongo kwamba wanadhulu kwa vile wanataka muunga rais mkono ni stupidest reason. Wananchi wameshaelewa ila sio wewe kanjanja. in fact nimejifunza sana,ingawa sio mara ya kwanza kukutana na wakuu wa wilaya na kuona jinsi wengi walivyo,ila huyu kaniacha kinywa wazi.Anaenda ongea dili huku akionekana wazi hajui hata anaweza honga bei gani, huku akijianika kwamba hana uwezo kihivyo,ila anachokiita ushawishi.hata dogo mwenyewe kaona na kumweka kati
Wakihama wamehongwa, wamenunuliwa.
Sasa hebu angalia, mkutano wa kuangalia ushahidi wa rushwa ya kuwanunua madiwani yameanza kuzungumzwa na mengine ya miradi, anashambuliwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo.
Wao wana video,wewe una tumbo na keyboard.Kwa hiyo sio wanasema ila wanasema na inaonekana
Sasa wote tunajua hapa kuwa kutokana na changamoto anazokumbana nazo Nasari kwenye Jimbo amebaki kupambana na Mkuu wa Wilaya, anaona kabisa hataweza kurudi. Kwa hiyo kamfanya Mkuu wa Wilaya ndio adui yake, halikadhalika sote tunajua kuwa Mhe. Lema nae anaugomvi na Mkuu wa Mkoa Bw. Gambo sasa wanadhani watatumia tuvideo hutu kuwadhohofisha. Childish!!!!!
Usichojua ni kwamba changamoto za kuletwa na ccm zinamuimarisha, watu wa meru wanazidi ichukia ccm.Kwa taarifa yako Lema hana ugomvi na Gambo ila Gambo ndie ana ugomvi na Lema. Acha umbea km unajidai wewe ni mwanahabari.Ndio maana magazeti yenu hayana thamani sana km ilivyo vitabu vya maprofessor wenu hata vikipigiwa upatu hakuna wa kununua mizaha.Muulize Kitila km kauza vitabu vingapi pamoja na ccm kumpigia debe sana.Hata ccm wenyewe wangenunua tuu wangetosha muondolea njaa
Na niseme ukweli watumishi wa serikali katika mkoa wa Arusha mnagombanishwa bila sababu, maana hawa jamaa wanasema nyinyi ndio mnaowapa taarifa, naamini wanawasingizia.
Nimalizie kwa kusema tukiendelea kulea michezo hii ya kitoto ya Lema na Nasari tutakuja kujuta.
Umeweka umbea kisha unautumia kuhitimisha ujinga
Hii nchi imejengwa kwa juhudi kubwa za mababu zetu, who is Nasari aje kuibomoa, who is Lema?
Yaani mmefikia mahali pa kutengeneza sinema za kuwavuruga wananchi, mnatengeneza movie za kulivuruga taifa. Mimi naamini vyombo vya dola havitaacha hili lipite hivi hivi.
Wewe ndie ungejiuliza who are you?Wao ni waheshimiwa wabunge, na ni wabunge wa kuchaguliwa na sio wateuliwa au walamba viatu km wewe na hao wakuu wa mikoa watu wa kuja tuu ktk wilaya za watu kisha wanajaribu ziharibu
Ndugu Nasari pambana na hali yako kwenye Jimbo, kama ulipoteza muda wa kuhudumia wananchi wa Arumeru Mashariki ukidai unakwenda kusoma ili ukatengeneze sinema hii ya kukubeba kisiasa unakosea sana.
hali yako ndio hiyo ktk jimbo lake.Yako umeimaliza? huduma ya watu mojawapo ni hii ya kuwaambia kwanini waliwapigia kura watu juzi tuu leo wanawasaliti.
Unatafuta huruma ya wananchi. Unataka sinema hii ndio ikupe ushindi?
Nitashangaa sana kama vyombo vya dola vitaachia hili jambo lipite. Zipo nchi zilizofanya mageuzi makubwa ya uchumi na maendeleo kwa ujumla ililazimu watu kama hawa wapotezwe kabisa, maana kuendelea kupoteza muda na watu wa aina hii ni sawa na kuchezea shilingi chooni.
Unashawishi mauaji mkuu. Mungu akuhurumie sana.Ni hiyo njaa yako tuu imefikia mhali haiwezi rudi nyuma.
Haiwezekani watu wale wale kila siku wanaleta taharuki nchini, halafu wanachekewa tu.
Taharuki mnafanya nyie na matendo yenu,sio hao wanaoyafunua n akuyaweka wazi. Km mnatengeneza mkanda wa kuweka hadharani na mnaweka vipande,kwanini kipande kingine kikiwekwa hadharani hamtaki?nyie ndio mnafanya maigizo.
Nimesoma Majibu ya Mhe Mnyeti, yeye amesema vizuri sana kuwa amechangia Harusi ya Diwani kama alivyoombwa na Muhusika na kama alivyoombwa kuchangia matibabu ya Mhe Lissu, na Amekwenda mbali zaidi kwa Kusema Katika matukio ya filamu hii ambayo producer alikuwa Lema na Director alikuwa Nasari ni filamu ya kuokota matukio ya kazi anazofanya kama Mkuu wa Wilaya.

Uchaguzi umekwisha 2015, badala ya kujenga nchi sisi kila siku kutiana hamaki tu.

Wasalamu katika UZALENDO
Jerry C. Muro
Dar es Salaam
Tanzania
 
Anaandika Jerry C. Muro
Dar es Salaam, Tanzania
October mosi, 2017

Nimetazama mkutano na waandishi wa habari wa Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nasari ambao alimualika pia Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Godbless Lema, nikaishia kuvuna hasira kubwa sana. Na kwa hili kwa kweli naomba watakaokasirika wanisamehe.

Mimi ni kijana ninayefanya kazi za upigaji wa picha na utengenezaji wa vipindi na makala mbalimbali (Audio Visual Production). Kwa mara ya kwanza baada ya Mhe. Rais Magufuli kuwapokea madiwani walioamua kuondoka CHADEMA na kuhamia CCM pale Sheikh Amri Abeid Arusha niliposikia kuwa Nasari anasema anaushahidi usio na mashaka na ambao ameupata kwa vifaa maalum alivyovipata nchini Uingereza nilivutiwa sana kwamba nguvu ya teknolojia sasa itamaliza ubishi juu ya biashara ya kununua wanasiasa ili wahame upande mmoja kwenda mwingine.

Nilikatishwa tamaa na Nasari akiwa na mwenzake Lema waliposema hawatatoa ushahidi huo kwa yeyote isipokuwa wakikutana na Rais, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ama viongozi wa juu waliokuwa wanawataja. Niliona hawa ni wababaishaji kama kawaida yao.

Leo nikabonyezwa kwamba kuna mkutano wa waandishi wa habari na uthibitisho unatolewa, nimefuatilia mwanzo mpaka mwisho na nimeogopa sana, nimeogopa kwa sababu naona tunakokwenda sasa watanzania wote tunafanywa watoto.

Tunaigeuza nchi kuwa ya maigizo na sinema, tunaleta mzaha na taharuki badala ya kujielekeza katika ujenzi wa taifa letu ambalo kwa kweli linahitaji mikono na akili zetu ili litokea hapa lilipo.

Sasa twenda kitaalamu.
Picha zilizotolewa na Nasari zinaonesha zimerekodiwa na kamera ya kificho na kwa hakika aliyekuwa anarekodi anaoneka kabisa ama alitumia kalamu zenye kamera ambazo zinapatikana madukani popote Dar es Salaam hata mikoani ama katumia kamera zilizopandikizwa kwenye vishikizo vya shati.
Hivi vifaa vya kawaida sana na kila anayehitaji anaweza kuvipata, wafanyabiashara wengi wanavyo na huvitumia pale wanapofanya makubaliano na watu mbalimbali ili wasije wakawageuka baadaye. Hata bei yake ni ndogo, mimi nina kalamu yangu nilinunua kwa shilingi 23,500 na inarekodi vizuri.

Ama laa aliyerekodi anaweza kuwa ametumia simu ya mkononi.
Matokeo yake ni kuwa ubora wa picha dhaifu sana na sauti haisikiki kabisa kwa uthibisho wa kila kinachozungumzwa. Lakini pia eneo lililotumika kurekodi kuna mwangwi mwingi sana kiasi kwamba ngumu kujua sauti ya aliyekuwa anazungumza.

Kibaya zaidi kwa sababu ya kutumia vifaa dhaifu hata picha zilizorekodiwa hazioneshi sura ya mtu zaidi ya kuonesha traki suti na mikono na kwa kupitapita inaonesha sura ya mtu ambayo ni vigumu kujua ni nani kutokana na mwanga hafifu.

Mbinu hii hutumika lakini hutumika kwa weledi unaokuwezesha kutokuwa na mashaka na Yule unayemrekodi.
Kwa sisi tunaofanya kazi za Audio visual production kuchukua picha Fulani ukaipandikizia sauti ni jambo rahisi sana na mchezo huu unafanywa sana na watengeneza sinema na movie.

Unaweza kuchukua sauti ya Juma ukaipandikiza kwenye picha ya Hamis.
Sasa nataka kumwambia hivi Nasari, taharuki aliyoitengeneza kwa watanzania kwa kutegemea ataonesha vipicha hivyo vilivyopigwa na simu ya mchina ama vikamera vya kalamu ni utoto mkubwa sana. Hao anaosema ni akina Mnyeti na Mkurugenzi na Katibu Tawala wa Meru hakuna mahali wanapoonekana kwa uhakika kwamba wamesema unachodai, lakini pia hata hizo sauti zao hazisikiki kwa uthibitisho wa uhakika kuwa wasemaji walikuwa wanasema nini.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari Nasari anafanya janja ya nyani eti anapandisha sauti za hizo video halafu anazima na kuzungumza yeye kwamba wamesema hivi na hivi na hivi. Utoto na ujinga wa hali ya juu.

Mhe. Nasari na mwenzako Lema, tupeni huo ushahidi usio na mashaka, hizi takataka mnazotaka kupanda ndege kuja kuzileta kwa Kamishna Mkuu wa TAKUKURU ni upuuzi na usanii wa kupigiwa mfano, na I wish ningekuwa mimi ndio Kamishna Mlowola mkikanyaga tu ofisini kwangu nawakamata na kuita vyombo vya dola ili muthibitishe madai yenu.

Kwa sababu nina hakika mnajua mnafanya, fanyeni siasa za kileo jamani. Siasa za kuwafanya watanzania watoto ama wajinga sio leo.

Hizo video zenu zinaweza kutengenezwa na mtu yeyote, tunataka utuoneshe video kama zile alizozionesha Jerry Muro alipowapiga wale askari wa barabarani wanapokea rushwa. Picha iwe clear na ambayo mtu akiona anapata uhakika kwamba ile ni hela. Ama tunataka kuona video kama ile ya yule askari aliyepokea rushwa kwa watalii kule Zanzibar.

Nilitarajia kumuona DC Mnyeti akigawa hela kama mlivyodai, nilitarajia kuwaona madiwani wakipokea hiyo hela kama mlivyotuaminisha. Badala yake mnatuletea picha za mashati ya watu na sauti za kupandikiza.
Hakuna hata diwani mmoja mliyemuonesha hapo, na ningekuwa mimi ni diwani ningewafungulia mashitaka ya kunichafua. Ili mkathibitishe hiyo rushwa nilichukua wapi.
Kama ushahidi ndio huu, Nasari anastahili kukamatwa mara moja ili taharuki aliyeijenga kwa jamii aithibitishe. Ama achukuliwe hatua.

Na kwa kweli mimi sielewi, hivi kweli tunajenga nchi kwa mtindo huu? Kwani Diwani ama mwanachama wa chama cha siasa kuhamia chama kingine tatizo nini? Mbona wanasiasa wanahama kila siku? Wapo wanaokwenda Chadema akina Sumaye, Lowassa, Mgeja, Masha, Ester Bulaya na wengine wengi. Hawa ni wakubwa wakubwa tu. Halikadhalika wapo wanaohama Chadema na kwenda CCM wengi tu wakiwemo hao madiwani kuna shida gani?
Manaake tunatengeneza mazingira kwamba chama kinachostahili kuhamwa ni CCM tu, Chadema hapana.

Wakihama wamehongwa, wamenunuliwa.
Sasa hebu angalia, mkutano wa kuangalia ushahidi wa rushwa ya kuwanunua madiwani yameanza kuzungumzwa na mengine ya miradi, anashambuliwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo.

Sasa wote tunajua hapa kuwa kutokana na changamoto anazokumbana nazo Nasari kwenye Jimbo amebaki kupambana na Mkuu wa Wilaya, anaona kabisa hataweza kurudi. Kwa hiyo kamfanya Mkuu wa Wilaya ndio adui yake, halikadhalika sote tunajua kuwa Mhe. Lema nae anaugomvi na Mkuu wa Mkoa Bw. Gambo sasa wanadhani watatumia tuvideo hutu kuwadhohofisha. Childish!!!!!

Na niseme ukweli watumishi wa serikali katika mkoa wa Arusha mnagombanishwa bila sababu, maana hawa jamaa wanasema nyinyi ndio mnaowapa taarifa, naamini wanawasingizia.
Nimalizie kwa kusema tukiendelea kulea michezo hii ya kitoto ya Lema na Nasari tutakuja kujuta.

Hii nchi imejengwa kwa juhudi kubwa za mababu zetu, who is Nasari aje kuibomoa, who is Lema?
Yaani mmefikia mahali pa kutengeneza sinema za kuwavuruga wananchi, mnatengeneza movie za kulivuruga taifa. Mimi naamini vyombo vya dola havitaacha hili lipite hivi hivi.

Ndugu Nasari pambana na hali yako kwenye Jimbo, kama ulipoteza muda wa kuhudumia wananchi wa Arumeru Mashariki ukidai unakwenda kusoma ili ukatengeneze sinema hii ya kukubeba kisiasa unakosea sana.

Unatafuta huruma ya wananchi. Unataka sinema hii ndio ikupe ushindi?
Nitashangaa sana kama vyombo vya dola vitaachia hili jambo lipite. Zipo nchi zilizofanya mageuzi makubwa ya uchumi na maendeleo kwa ujumla ililazimu watu kama hawa wapotezwe kabisa, maana kuendelea kupoteza muda na watu wa aina hii ni sawa na kuchezea shilingi chooni.

Haiwezekani watu wale wale kila siku wanaleta taharuki nchini, halafu wanachekewa tu.

Nimesoma Majibu ya Mhe Mnyeti, yeye amesema vizuri sana kuwa amechangia Harusi ya Diwani kama alivyoombwa na Muhusika na kama alivyoombwa kuchangia matibabu ya Mhe Lissu, na Amekwenda mbali zaidi kwa Kusema Katika matukio ya filamu hii ambayo producer alikuwa Lema na Director alikuwa Nasari ni filamu ya kuokota matukio ya kazi anazofanya kama Mkuu wa Wilaya.

Uchaguzi umekwisha 2015, badala ya kujenga nchi sisi kila siku kutiana hamaki tu.

Wasalamu katika UZALENDO
Jerry C. Muro
Dar es Salaam
Tanzania
Mhhhhhh duuuh unaomba kazi ccm kwa nguvu kweli kweliii mpaka aibu
 
katika yote uliyoandika kuna sehemu nadhani umeghafika hasa unaposema
(WAPOTEZWE)

kauli hii hukupaswa kuitoa kwani kama ingetumika na wale waliokupinga wakati ule ulipokamatwa kwa makosa mbalimbali, tusingekuwa na wewe tena.

nasisitiza AMANI!!! AMANI!!! AMANI!!! AMANI!!!!! YA TAIFA LETU TULILOPEWA NA MUNGU KAMA URITHI WETU TUIDUMISHE.
Hata Lissu walianza hivi hivi.Eti kuliko mtu mmoja azuie taifa kwenda mbele bora apotezwe. Tuliona kilichotokea.
 
Back
Top Bottom