wakati joto la kisiasa
likiendelea kukua hapa nchini kuelekea 2015, jimbo la kawe lina mpambano
mkali sana wa ndani unaoendelea pia.
Mpambano wenyewe ni mbio za ubunge za jimbo hilo ambapo sasa kundi la
mbunge wa sasa halima james mdee linajipanga kuhakikisha linakamata
nafasi zote muhimu kuanzia tawi, kata mpaka jimbo ili kumrahisishia
ushindi mdee katika kura za maoni,
lakini kwa upande wa pili mwanasiasa kijana jerry muro anayetarajia
kuacha kazi tbc mwakani ili kuanza rasmi harakati zake ameshajipanga
vizuri kumng'oa mdee kwan kundi lake ni lile lililokuwa likiupinga
uongozi wa sasa wa jimbo la kawe chini ya katibu mbaga na mwenyekiti wa
vijana mfinanga..
Mtonyo wa ndani unasema jerry muro atakutana na vijana wake wanaojiandaa
kugombea bavicha jimbo, bawacha jimbo, wazee jimbo na chadema jimbo ili
kukamilisha mipango ya mwisho ya kumng'oa mdee.
Kijana gerald patrick, byamungu pamoja na sagati william wanatajwa kuwa
vinara wa mpango huu.