PostGE2025 Jenista Mhagama kuzikwa Desemba 16, Ruanda - Mbinga

PostGE2025 Jenista Mhagama kuzikwa Desemba 16, Ruanda - Mbinga

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Ratiba rasmi ya mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Joakim Mhagama, imetangazwa, ikionyesha utaratibu wa maombolezo na ibada zitakazofanyika kuanzia Desemba 12 hadi Desemba 16, 2025.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Bunge la Tanzania, maombolezo yameanza leo nyumbani kwake eneo la Itega Jijini Dodoma, ambako mwili wa marehemu uliwasili kwa ajili ya kuagwa na familia pamoja na waombolezaji.

Soma pia: Jenista Mhagama, Mbunge wa Peramiho afariki dunia


Kesho, Desemba 13, ibada kuu ya kumuaga marehemu itafanyika katika Kanisa Katoliki Kiwanja cha Ndege Jijini Dodoma, ikihudhuriwa na waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali. Baada ya ibada hiyo, mwili utasafirishwa kuelekea Songea kwa ajili ya kuendelea na shughuli za kuaga.

Siku ya Desemba 14, maombolezo yataendelea nyumbani kwa marehemu katika eneo la Makambi, Songea Mjini. Jioni ya siku hiyo, mwili utapelekwa Kanisa Katoliki Matogoro kwa ibada nyingine kabla ya kurejeshwa nyumbani.

Mnamo Desemba 15, shughuli za kuaga zitaendelea Peramiho, Songea Vijijini, kupitia ibada itakayofanyika katika Kanisa Katoliki la Peramiho, kisha waombolezaji wa eneo hilo watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kabla ya mwili kurejeshwa nyumbani kwa marehemu.

Safari ya mwisho ya mwili wa Marehemu Mhagama itafanyika Desemba 16, ambapo utapelekwa katika Kijiji cha Ruanda wilayani Mbinga kwa ajili ya mazishi. Maziko yanatarajiwa kufanyika kijijini hapo kwa mujibu wa utaratibu uliopangwa na familia pamoja na kamati ya mazishi.
 
Ni muda sasa tume ya uchaguzi itangaze tarehe ya uchaguzi mdogo, watu wa peramiho wasikose uwakilishi
 
Back
Top Bottom