Hao waumini/wafuasi wa kanisa hilo watawanywe kwenye branch nyingine za TAG na hizo hela walizo pata wagaiwe maskini na watoto yatima!Jengo la Kanisa la TAG Kariakoo mkabala na s/msingi Uhuru,limeuzwa kwa Mpemba mmoja. Mchungaji wa kanisa hilo alipohojiwa alisema wameuza kwa lengo la kujipanua zaidi. Limeuzwa kwa Tsh 850 milioni. Majengo ya ibada yanapouzwa kwa wafanyabiashara si jambo zuri,hata kama lengo ni kujipanua,basi wangegeuza eneo hilo kuwa kitega uchumi chao kama kanisa. Kuna waumini wengi wataumizwa na uamuzi huu,na la mwisho ni uhakika mdogo wa kupata eneo lingine kariakoo kwa pesa hiyo.
Si ajabu hela hiyo ikatafunwa kabla ya kutimiza malengo yaliyokusudiwa.
source; Mtanzania ya jumapili ya tarehe 6/12/2009.
Labda walijadili Kanisani kwao na kufikia muafaka wa kuliuza. Makanisa yana viongozi na viongozi wanaongoza watu, na watu ni sisi tulio hapa duniani.
Mwisho, nafikiri si vema kuweka conclusion kuwa hela za mauzo zitatafunwa bila ya kueleza na/au ambatanisha sababu yakinifu.
Labda walijadili Kanisani kwao na kufikia muafaka wa kuliuza. Makanisa yana viongozi na viongozi wanaongoza watu, na watu ni sisi tulio hapa duniani.
Mwisho, nafikiri si vema kuweka conclusion kuwa hela za mauzo zitatafunwa bila ya kueleza na/au ambatanisha sababu yakinifu.
Waumini wameongezeka na kijikanisa kile ni kidogo tena sana, kuna kelele nyingi mno, ibada haziendi kwa amani, kikao cha baraza la wazee walibariki kuuzwa kwa kanisa lile na waumini wakaunga mkono , kwa pesa hizo zote limepatikana eneo lingine katikati ya mji penye utulivu na pesa ile itaanzishia ujenzi wa nyumba mpya ya BWANA, kanisa si mali ya mtu binafsi , ni nyumba ya bwana.....hizo hadithi zingine kua pesa italiwa so and so, aah sio lengo la kuuzwa hilo eneo.
mnastaajabia hilo. Mbona kuna mengisana ulaya yanageuza kuwa majumba ya starehe au biashara.
Mnastaajabia hilo. Mbona kuna mengisana Ulaya yanageuza kuwa majumba ya starehe au biashara.
Nadhani wazee wa kanisa na waumini walihesabu na kuona pesa ni nyingi na watajenga banda la milioni tano hala yoooote iliyobakia wataitolea maelezo kwamba imefanyika kazi ya Bwana.
Jamani nyie Mungu anaona na anakaa kimya ktk hekima zake akisubiri siku ya hukumu kuwapasha ukweli wa kila hatua bofyo mnazopiga sasa.
Kama kanisa lilikuwa dogo na watu wakaongezeka si wangewapunguzia waumini wapya ktk makanisa mengine ya TAG!!!! au huko waendako si mbali na kariakoo ambapo wana waumini kedekede? naomba kujulishwa pls
yeye si mwanasiasa kwamba anatumikia umma wa w TZ wote, yeye ni kiongozi wa kiroho na anawajibika moja kwa moja kwa umma wa kanisa. ana haki yakukataa kuhojiwa kwa malengo asiyo yafahamu, taarifa za uuzwaji wa eneo hilo zimekua zikitolewa mara kwa mara kwenye ibada pale UHURU. Kwa waumini wa pale kila mtu anaelewa taratibu zote ambazo mchungaji alizichukua katika kukamilisha mpango huo.Mchungaji alipoulizwa zaidi amegoma kutoa maelezo. .
kabla hawajauza tayari waliishapata eneo jipya la kujenga kanisa lao, hizi habari hutolewa pale kanisani, na kwakweli waumini wengi wameelewa dhamira safi ya zoezi hilo.unajua kitakacho wasumbua hao jamaa ni wapi wakajenge hilo kanisa na kweli itakuwa rahisi kwa muumini wa hilo kanisa kulifata lili[po hilo kanisa jipya?
hapo kwa kweli wamechemsha kama walikuwa wanaona hilo kanisa ni dogo basi angalau wangepageuza kuwa sehemu ya biashara kwa kwenda kuchukua mkopo benk huku wakijenga kanisa lingine
kwa hiyo fedha na njaa za wachungaji wetu pamoja na wazee wa kanisa akyaMungu tutasikia tu, haya ni kama yale ya Mtikila anapiga kelele mwisho wa siku anaenda kwa RA kuomba fedha za kanisa aibu sana kwa hawa wachungaji