Jenerali Ulimwengu: Tumerudi nyuma miaka 50 kwenye demokrasia, Kikwete apelekwe mahakamani

Jeneral ni mnafiki, kwa nini hakuusema ukweli uo akiwa rais, je Ulimwegu hajui km JK anakinga, au angaongea kufurahisha umma, wa wannanchi, jambo la msingi hapa, nyie wazee tuachieni nchi yetu, mlicho kifanya kinatosha ezi wa mali za nchi hii.
Hujaelewa hoja ya Ulimwengu. Na kama wewe ni kijana basi Taifa hili huenda lilikuwa bora zaidi wakati wa hao akina Ulimwengu kuliko litakavyokuwa wakati wa vijana wa namna yako. Vijana wanatakiwa kutumia akili zao katika kutafakari na kuchambua mambo kuliko kuwa waitikiaji wa vibwagizo vya vyama au watawala.
 
Kiwete alishamaliza sehemu yake ya mchakato wa Katiba hiyo mpya, sehemu iliyobakia imaliziwe na VIngozi waliopo madarakani sasa hivi. Mchakato ulikuwa Poa tu, kilichobakia sasa hivi ni kupiga kura tu ya kuibaliki. Kwani ilikuwa ni lazima kila kitu amalize yeye? Si wengine wapo, na waendelee basi?

REjea Link hii kwa taarifa zaidi>>>>>>>>>>Tathmini:Mchakato wa katiba ya TZ - BBC Swahili
Kikwete aliharibu mchakato mzima kwa kutumia vikao vya chama chake kutengeneza kitu walichokiita eti katiba pendekezwa. Ule ulikuwa ni ujinga wa hali ya juu. Nadhani mahali pa kuanzia ni pale ilipoachia kamati ya Warioba. Katika uchafu wote uliofanyika awamu ya nne, huu wa katiba mpya haustahili kuvumiliwa.
 
Kuna mhadhiri mmoja aliwahi kutuambia darasani kuwa " Kwa mtu mwenye njaa Mungu kwake ni Mkate (chakula). Ukikutana na mtu mwenye njaa ukamuonesha njia kuwa kulia inakwenda kwa Mungu na kushoto inakwenda kwenye chakula, ujue kuwa huyu mwenye njaa ataenda kilipo chakula"
Wanasiasa wafanye kazi ya kuwaondolea wananchin shida za kupata mahitaji ya msingi. Demokrasia ije kadiri maendeleo ya watu kiuchumi yanavyokuwa.
Usichokijua ni kwamba ni vigumu sana kujenga uchumi na kupata maendeleo kama hakuna demokrasia. Kama hakuna demokrasia huwezi kuhoji mipango hovyo ya serikali kuhusiana na uchumi. Kama hakuna demokrasia, watawala wanaweza kufuja fedha za umma bila ya kuhojiwa.

Hata huu upuuzi wa uhaba wa sukari umechangiwa na ufinyu wa demokrasia. Wataalam na watu mbalimbali walikuwa wanajua kuwa hatua ya Rais kuzuia uagizaji ingesababisha upungufu lakini hawakuweza kumzuia Rais kutekeleza maamuzi yake kwa sababu ya hofu, kwa sababu ya upungufu wa demokrasia ambao ulifanya vyombo vyenye mamlaka kuhusiana na biashara ya sukari kuzimwa na maamuzi ya Rais. Baadaye wajinga wengi wakalazimika kuendelea kusifia maamuzi yenye makosa, japo dhamira ilikuwa nzuri, badala ya kuonesha makosa ya serikali.
 
Ila Magufuli lazima ajiangalie sana maana anakokwenda atapotea haraka mno, kutotenda haki na kufikiri unajua kila kitu ni kujitakia majanga. Busara ya kiongozi yeyote ni kusikiliza kwa makini wengine wanasemaje na si wewe tu kusema kuibuka na kuonea watu hata wasifanye mikutano ya ndani ya ofisi zao hii ni dalili mbaya kwa kiongozi yeyote, ajipime na atafakari kwa umakini mkubwa
 
Demikrasia ni mchakato ambayo unapitia njia zake kulingana na mazingira.

Kutaka kujenga demokrasia kwa sasa inayofanana na demokrasia ya nchi za Magharibi ni kama kuanza kumlazimisha mtoto ambaye hajaanza hata kutambaa aanze kukimbia.

Huwezi kujenga demokrasia kama inayotendwa kwa sasa katika nchi za Magharibi wakati kuna wananchi kwa mamilioni katika vijiji vingi nchini ambao hawana hata mahitaji ya lazima(basic needs).

Demokrasia ya nchi za Magharibi ni kama elimu ambayo ina mpangilio wake na kwa maana hii, huwezi kuanza kumfundisha mtoto elimu ya sekondari wakati hata ya shule za msingi hajapitia.

Tatizo letu kwa sasa ni kuanza kuiangalia Tanzania kwa kutumia jicho la nchi za Magharibi wakati kuna maeneo mengi nchini ambayo hata elimu kwa wananchi ni majanga achilia mbali mlo wa siku na malazi (shelter).

Nchi za Magharibi zilipitia mifumo ya udikteta kwa njia ya tawala za kifalme kabla ya kufikia demokrasia waliyonayo kwa sasa ambayo wanataka tuitende wakati mazingira yetu hayaruhusu kwa sasa.

Tanzania ya sasa inahitaji kiongozi ambaye ni dikteta kwa maslahi ya wananchi wengi na siyo nchi yenye demokrasia kwa maslahi ya wachahe.

Mazingira ya Tanzania ya sasa hayaruhusu demokrasia kwa faida/maslahi ya wananchi wengi. Kutaka kulazimisha demokrasia ya aina hii ni kupalilia mfumo ambao matokeo yake ni kuwepo kwa makundi mawili makubwa ambayo ni kundi la wachache wenye nacho ambalo litazidi kuongezewa na kundi la pili ni kundi la wengi wasionacho ambalo litazidi kupunguziwa.
Hiyo ni nadharia potofu. Tafiti mbalimbali za kitaalam zinaonesha kuwa maendeleo hupatikana kwa urahisi zaidi pale ambapo kuna demokrasia kuliko palipo na udikteta. Kuifikia demokrasia ya kweli siyo lazima uchukue miaka karne nyingi kama unavyotaka kuwahadaa watu. Nchi kama Botswana, ni Taifa changa kuliko letu, lina maendeleo zaidi ya mara 10 ya Tanzania. Lina misingi imara ya demokrasia kuliko sisi. Kuna mataifa kama Singapore, walikuwa sawa kama sisi miaka ya 60 lakini leo hii maendeleo yao ya kiuchumi na kidemokrasia, kwa kadiri ya taarifa za UNDP, Tanzania kuweza kuwafikia walipo leo kwa mwendo wetu huu wa kobe, itachukua zaidi ya miaka 250.

Kinachochelewesha maendeleo ya Afrika ni misingi duni ya utawala wa kidemokrasia. Watawala wanawaburuza watu na kuwanyima watu wenye uwezo kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa nchi zao.
 
Kama huyu ni profesa bora tu nisiende shule maana naona ndiko kuna shamba la wasioelewa.
 
Kikwete ndio adui wa nchi hii... Hata Rais Magufuli anapata shida sana sbb ya Kikwete.. Refer Rais Magufuli alimweleza live JK amemwachia mzigo sana kila kitu HEWA TU... !! Mh. Rais Magufuli ndio maana alimchana live JK, hadi KATIBA MPYA ni HEWA sbb hela ndefu sana imetumika, na KATIBA MPYA HAKUNA.. hiyo ni KATIBA HEWA nayo..!!

JK ameharibu sana sehemu nyingi..!! Ndio maana Mh. Rais Magufuli anafanya safisha safisha ya SERIKALI, KUTUMBUA MAJIPU... The Govnt was IN VERY BAD SHAPE..!!

JK kazi kucheka cheka na kupiga madeal tu...!!

Kutumbua majipu kwa magufuli kulikuwa ni kuondoa masalia ya Lowasa.
Mbona huo utumbuaji hakufika kwenye madini? Utalii?
 
Hahaaaaaa nyumbu hamfaidiki na mambo kwa sababu mnapenda kusikia serikali ikishambuliwa tu. Fankuuuro.

Mwenye akili timamu afungue clip anayoongea Rais mstaaf Ben ataelewa. Ameainisha upumbavu wenu wa kulalamika na kulaumu hovyo na kutaka msikilizwe na kukubaliwa kila jambo. Kawapasha vizuri majukumu ya viongozi na wananchi wakiwemo mababy wasusaji. Msifikiri maendeleo yanakuja kwa kupiga domo na uonekane live. Fankuuuro
 
Usichokijua ni kwamba ni vigumu sana kujenga uchumi na kupata maendeleo kama hakuna demokrasia. Kama hakuna demokrasia huwezi kuhoji mipango hovyo ya serikali kuhusiana na uchumi. Kama hakuna demokrasia, watawala wanaweza kufuja fedha za umma bila ya kuhojiwa.

Hata huu upuuzi wa uhaba wa sukari umechangiwa na ufinyu wa demokrasia. Wataalam na watu mbalimbali walikuwa wanajua kuwa hatua ya Rais kuzuia uagizaji ingesababisha upungufu lakini hawakuweza kumzuia Rais kutekeleza maamuzi yake kwa sababu ya hofu, kwa sababu ya upungufu wa demokrasia ambao ulifanya vyombo vyenye mamlaka kuhusiana na biashara ya sukari kuzimwa na maamuzi ya Rais. Baadaye wajinga wengi wakalazimika kuendelea kusifia maamuzi yenye makosa, japo dhamira ilikuwa nzuri, badala ya kuonesha makosa ya serikali.
Demokrasia isiyo ondoa umasikini kwa kasi ipumzike kwanza kwani tuisha ionja na tujua ifanyavyo kazi. Sasa tunataka rais mkali ambaye anauthubutu wa kuwambia wananchi fanyeni kazi za uzalishaji mali shambani na viwandani hata katika sekta zisizo rasmi.
Nyie mnaotaka kuishi kwa porojo mtawajibika. Lazima mjue Mh Magufuli si Mh Kikwete kila mtu anambinu zake za kuongoza. Mfano Mh Kikwete hakuwa na uwezo wa kumpa mtu makavu lakini huyu anaweza hana rafiki ilimradi imethibitika umeharibu. Huu si udikteta na dikteta huwa hapimwa kwa haya msemayo. Huyu hutaka kila sheria iliyotungwa ifanye kazi yake pale kosa tajwa linapokuwa limefanyika. Hivyo vyombo husika vinapowahoji watu kwa makosa wanayotuhumiwanayo wajue ndio utekelezaji wa demokrasia kwa kuzingatia utawala wa sheria.
 
Ssawa kwa sababu huyo alikuwa fisadi mkuu kama mlivyomuainisha kwetu sasa kuacha virusi vyake ni sawa na kuacha maradhi na faida tunaziona.
Msomi ndio anavyo takiwa kila kitu akianike
Fungua clip ya Rais Mstaafu Ben Mkapa ndio utajijua ni nyumbu wa gredi gani Fankuuuro
 
Hata ikibidi watu wachapwe viboko hadi tukae sawa. Wanataka kujenga nchi kwa madili. Mtu wa TRA anakaa mezani anapiga dili ya mamilion kwa siku ati unatakiwa ufate taratibu ya kumuondoa? Fankuuuro kama mimi ni Rais nawatwanga risasi tu tuu fankuuuro
 
Ingekuwa demokrasia na uhuru wa habari umefinywa, angeweza kweli kuyazungumza hayo aliyoyazungumza??
 
Wapi huko wanakula democrasia??

Mwaka Jana mlizungusha mikono kwa miezi 3, mliambulia nini??

Arusha iko chini ya chadema mmebadilisha nini?? Kazi kulialia tu.

Mbona unakimbilia conclusion? Mimi sipo chadema wala sishabikii chama chochote cha siasa. Nilikua mstari wa mbele kusupport Magufuli wakati wa campaign simply coz niliona anafaa kuliko Lowassa, sasa hivi amepewa kichwa, kupinga anachokifanya hainifanyi kua cdm, inanifanya kua mtanzania nayetaka maendeleo, hata cdm yapo mengi wakiboronga napondea vilevile.

We tatizo lako umekosa counter~arguments unatafuta pa kujifariji kua you are right. Endelea kumtumikia mtakatifu. Simchukii Magu, ningependa kuona anaitransform Tanzania ikue kimaendeleo kwenye nyanja zote, kuua uhuru kutatugeuza libya muda si mrefu.
 
Jenerali amsema lakini wasomi wengi wanaujua lakini hawausemi. Ni lazima wasomi wasimame na kusema ili watu wafahamu.
Watu wetu wengi hawafahamu na hii imekuwa advantage kwa wanasiasa.
Mfano mtu mmoja alisema leo hela imopotea sana kiasi watu wanashidwa kujua waipateje. baadhi ya wenye magari wamepaki! Mtu mmoa akasema hajui kabisa hela inapoteaje! Huko Mtwara kuna wananchi wanauliza maana ya simu feki ni nini! Haiingii laini au?
Kanuni moja ya mwana TANU ilisema "nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.."
Wapo wanachi wasiojua mengi mfano kwa nini wabunge huwa wanabishana bungeni. kwa nini wanasiasa wanaandamana! nk.
Sasa wanachi hawaambiwi ni kwa nini badala yake kwa ulafi wa wanasiasa ambao ni wasomi huwahadaa wanachi kwa misemo kama " watanzania si wajinga" lakini hawawaambii ukweli. Jenerali amesema na wengine waseme ili watu wafahamu. Mwalimu alisema "watu wapaswa kufahamu"
 
Safari ni ndefu. Kila kitabu na zama zake. Magufuli has diferent priorities. And democracy is not. Ufisadi na uwajibikaji are.

Sijui kama mwananchi anayelala njaa, matibabu ni shida, anasikia kila siku hadithi za ufisadi wa pesa za umma, utam-convince kwamba tunahitaji demokrasia. Wengi katika nchi yetu tuna-msupport Magufuli si kwamba hatuoni kwamba anaminya uhuru wa kikatiba (rejea kufukuzwa wabunge wa upinzani), lakini ukweli ni kwamba tumechoshwa na wanasiasa wanaohangaikia matumbo yao wakisahau waliowachagua. What is democracy if it cant guarantee my ability to bring food on the table for my family?

Katika taifa lolote Maskini adui yake ni Tajiri (hata kama utajiri umepatikana kwa uhalali uliotukuka) lakini asiyenacho anaamini amekosa kwa sababu Tajiri kamkosesha. Leo Magufuli ametangaza kwamba watu wa million 40 washushwe wapewe million 15....wengi tumeshangilia. Unajiuliza ni kwa nini?

Essentially Magufuli is exploiting our fatigue na hawa wanasiasa wanaochumia matumbo yao. Ndo maana leo ukiongea kwamba demokrasia inaminywa...I can gurantee ......very few will sympathise with you on the street! Maana anajua nyinyi ndo mnafaidi keki ya taifa. Unadhani kwa nini miaka hiyo tulisupport Ujamaa wa Nyerere alivotaifisha mali za wahindi na wangine? kwa sababu tuliamini hawa matajiri/wahindi ndo wachawi wa shida zetu. Kulikuwa na ukweli? Historia itatoa hukumu.

In all wanasiasa wajifunze ku-align agenda zao na shida za wananchi. Na ndicho Magufuli amefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Na akiendelea hivi, I tell you atatuongoza for a foreseeable future.

Kaka yangu Zitto anasema kwamba atafia demokrasia na Magufuli atafia ufisadi.

Hakika kwa wananchi tulio wengi. Magufuli ndo mshindi. Maana hata mimi na shida zangu..nimeaminishwa kwamba Mkurugenzi wa NHC anayepata million 40 ndo adui yangu. Ingawa kiuhalisia hata angenyimwa mshahara, I doubt kama maisha yangu yangebadilika.

Hoja za wanasiasa wetu ziakisi shida na changamoto za wananchi. Ndugu yangu wa Kakonko (wilaya ya mwisho kwa umaskini Tanzania)...I am sure priority yake siyo freedom of expression. Ni kuhudumia chakula familia yake au kupeleka mtoto shule (kununua uniform)....Magufuli amelitambua hilo mapema. Na lugha yake inaakisi hivyo.

Sasa kuminya demokrasia kunamsaidiaje katika kufikia lengo lake la kuondoa umaskini wa sisi Watanzania maskini tulio wengi? Don't you see that he is creating an unnecessary distraction for his own well-intended efforts to fight poverty and corruption? Isitoshe, criticism ingeweza kumsaidia kuona "gaps" katika kufikia malengo ya uongozi wake. Evidently, his current obsession with controlling dissent is a dead-end strategy, because it is a practice his development partners don't share, and will almost certainly try to stop. Hapo atajikuta anajaribu kupigana na kilamtu anayemzunguka. In the end, he will lose, for a simple reason that he can't succeed without the support of his both local and international partners, who are overwhelmingly opposed to undemocratic governance.

Simple, huwezi kuendelea kama taifa peke yako, au kwa kutengeneza maadui ndani na nje ya nchi, huku ukiendelea kuishiwa marafiki kwa kasi. Ndani tu ya muda mfupi ambao ameingia madarakani, rafiki yetu na "brother" wetu kiuchumi kwa muda mrefu, Kenya, anaanza kugeuka kuwa adui. Mshirika wetu Marekani amefikia mpaka kutunyima baadhi ya misaada. Umoja wa Ulaya wanashirikiana na sisi kwa tahadhari kubwa zaidi sasahivi. Ndani ya nchi, vyama vya upinzani wananuia kupambana naye vikali. Hakika, kama asipobadilika, hafiki mbali.
 
Jeneral ni mnafiki, kwa nini hakuusema ukweli uo akiwa rais, je Ulimwegu hajui km JK anakinga, au angaongea kufurahisha umma, wa wannanchi, jambo la msingi hapa, nyie wazee tuachieni nchi yetu, mlicho kifanya kinatosha ezi wa mali za nchi hii.
Wewe si mfuatiliaji wa makala za JU ambaye amezungumza mambo haya ya katiba mara nyingi sana. JU anajua kuwa JK ana kinga ndo maana anapaswa kulaumiwa kwa kutomaliza suala la katiba. Katiba ya Warioba ingepita JK angekuwa Lupango. Sasa jipime; wewe na JU nani mnafiki?
 


Jenerali Ulimwengu akiwa kwenye kongamano la kigoda cha mwalimu Nyerere chuo kikuu cha Dar es Salaam, amesema pamoja na hatua nzuri anazochukua Rais wa sasa, Mheshimiwa John Magufuli ambazo zimepongezwa lakini ukiangalia picha kubwa ni kwamba tumerudi nyuma kama miaka 50 kwenye demokrasia.

Ulimwengu amesema ni kutokana na kufinya uhuru wa kujieleza na hususan kwa kufinya uhuru wa wawakilishi wa wananchi ndani ya bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Ulimwengu ameendelea kwa kusema katika hili hamna kifimbo cha uchawi cha kujinasua isipokuwa mchakato wa katiba ambao ulichukua fedha nyingi kisha ukaachwa njiani na Mheshimiwa Kikwete.

Mwandishi huyo wa habari na mchambuzi wa masuala ya kisiasa ametaka Raisi mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete kufikishwa mahakamani kwa kosa la kuisababishia serikali hasara baada ya kutokuufanikisha mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.

Jenerali Ulimwengu alisema katika kipindi cha mchakato wa katiba mpya, fedha nyingi ambazo zilitokana na kodi za wananchi zilitumika katika shughuli mbalimbali lakini katiba mpya haikupatikana.

“Katika kipindi hiki tumeona viongozi mbalimbali waliopita wakichukuliwa hatua kwa kuisababishia serikali hasara… Kikwete anapaswa kufikishwa mahakamani kuelezea zile pesa za mchakato wa katiba zitarudi vipi,” alisisitiza.

Akijibu hoja hiyo, mwenyekiti wa mdahalo huo, Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa amesema wakati wa mchakato huo yeye hakuwa mshauri wa rais hivyo hawezi kulijibia suala hilo.

“Mimi sikuwahi kuwa mshauri wa raisi wala mshauri wa chama juu ya mchakato huo, ila niliombwa kutoa maoni kama wananchi wengine,” alisema Mkapa na kuongeza kuwa wasomi wanapaswa kufanya uchambuzi makini kabla ya kutoa hoja kwani kuna baadhi ya hoja hutolewa lakini sio muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Tunakupongeza jenerali kwa kuwa mkweli na kujiondoa kwenye kapu la wanao jipendekeza
 
Back
Top Bottom