Jela miaka 30 kwa kulawiti

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
Monday, November 16, 2009 10:00 AM
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala ya jijini Dar es Salaam, imemuhukumu mfanyabiashara Mohamed Yusuph (27), mkazi wa Kariakoo kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka 11.
Jela miaka 30 kwa kulawiti

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala ya jijini Dar es Salaam, imemuhukumu mfanyabiashara Mohamed Yusuph (27), mkazi wa Kariakoo kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka 11.



Hukumu hiyo imetolewa katika mahakama hiyo na Hakimu Janeth Kinyage wakati upende wa mashitaka wa kesi hiyo ulikuwa ukiongozwa na Mwendesha Mashitaka, Mkaguzi wa Polisi, Mussa Gumbo.


Mwendesha Mashitaka Mkaguzi wa Polisi, Bw. Musa Gumbo alimtaka Hakimu kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo katika jamii.


Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, mahakama iliamuru mshitakiwa huyo kufungwa kifungo cha maisha kutokana na uzito wa kosa lake.


Lakini baada ya mshitakiwa kuomba apunguziwe adhabu kutokana na matatizo yake ya kiafya mahakama iliamuru akatumikie kifungo cha kwenda miaka 30 jela.


"Muheshimiwa hakimu naomba nipunguziwe adhabu hiyo kwa kuwa hali yangu ya kiafya sio nzuri muheshimiwa" aliomba mtuhumiwa mbele ya mahakama


Hakimu Janeth Kinyage alisema, ametoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka ambao unamtia hatiani mshitakiwa.


Awali ilidaiwa kuwa Februari 21, mwaka jana, katika maeneo ya Feri, mshitakiwa alimlawiti mtoto wa miaka 11 [jina linahifadhiwa] na kumsababishia maumivu makali mwilini na kumuharibu maumbile.


Hivyo kutokana na ushahidi uliosikilizwa na hakimu kuuridhia na ushahidi wa kidaktari mtuhumiwa anakwenda kutumikia kifungo hicho jela.


http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3555234&&Cat=1
 
Hii ni kali kweli.
Hawa majaji wakienda kule Zenj sio nchi nzima watakuenda jela kila mmoja miaka 30 ???
 
Back
Top Bottom