Jela kwa kufanya mapenzi na mwanafunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jela kwa kufanya mapenzi na mwanafunzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mchapaji, Mar 26, 2010.

 1. Mchapaji

  Mchapaji Member

  #1
  Mar 26, 2010
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  MWANAMKE Sophia Philemon [44] ambaye ni mama wa watoto watatu, amehukumiwa kwenda kutumikia kifungo cha miaka saba jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mwanafunzi chini ya miaka 18.Mwanamke huyo mkazi wa wilayani Moshi vijijini alifanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Langasani mwenye umri wa miaka 15 bila kutambua anatenda kosa kisheria.

  Hukumu hiyo takatifu, ilitolewa jana na Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi John Nkwabi wa Mahakama ya Mkoa Kilimanjaro, John Nkwabi baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashitaka.

  Nkwabi alisema ameridhika na ushahidi uliotolewa akiwemo na mwanafunzi huyo umeithibitishia mahakama pasipo shaka yoyote na mahakama imeridhika na ushahidi huo.

  Nkwabi alisema kitendo alichokifanya mwanamke huyo cha kumlazimisha kijana huyo kufanya nae tendo la ndoa ni kosa chini ya kifungu namba 138B (1) (d) cha kanuni ya adhabu kinachosimamia makosa ya kimapenzi kwa watoto baada ya sheria hiyo kufanyiwa marekebisho mwaka 2002.

  Awali hati ya mashitaka ilionyesha kuwa, Februari 28, mwaka jana, saa 1:00 usiku, huko katika kambi namba tisa katika nyumba za sukari wilayani Moshi vijijini, mshitakiwa alimlazimisha mwanafunzi huyo kufanya naye mapenzi katika chumba anachoishi na mumewe.

  Ilidaiwa kuwa muda huo mwanafunzi huyo alikuwa ametoka dukani alikokuwa ametumwa na wazazi wake na mwanamke huyo alimwita na kumshawishi aingie ndani ya nyumba yake anapoishi na mumewe na baadaye kumlazimisha kufanya naye tendo la ndoa.

  Sophia ni mke wa mtu na ni mama wa watoto watatu ambao wawili wa kike na mmoja ni wa kiume.
   
 2. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ndugu Mchapaji,

  Karibu katika jamvi, kwani hii ni post yako ya pili. napenda kukutaarifu ya kuwa kabla ujaweka bandiko lako jaribu kupitia kwanza mabandiko ya wenzako. Mada uliyoitundika hapa ilishatundikwa jana.

  Tafadhali fanya utafiti kabla hujatenda jambo.

  Karibu sana.
   
Loading...