Jeh, ananiigizia ama anamaanisha??

Jeh, ananiigizia ama anamaanisha??

Badilisha mpango mkuu alafu heshima ndoa ya mwenzako atakama unampenda umbali kati yenu ni nafasi ya ww kuzitoa hisia za kimapenzi kati yenu mfanye kama rafiki. Maybe is cute but know that is already married punguza mawasiliano naye jiweke mbali naye ili utengeneze AMANI ya ndoa yake
 
Pole na hongera; zingatia umri wako unasogea naamini wazazi wako wanasubiri wajukuu, usiwangushe tafadhali.
Huyo ni mke wa mtu sasa na wewe tafuta mke wako.
 
Kazi kwelikweli acha kupoteza muda na mke wa Mwanaume mwenzio tafuta wako.
 
Dah.. Kuna kaukwel flan hapaa
Ijiandae na ky kabisa mkuu ameshakwambia wazi hawezi wacha kuolewa kisa wewe. Sasa mwanzo ulitembea na mchumba wa mt sasa mke ujue. Utavalishwa dera shauri yako
 
Fb hatari sana,Yaani wachumba za watu wanaleta mazoea.Kuna mmoja naye nilimpokea Msamvu kama wewe Ulivyompokea Ubungo.Akili za Wanawake/Mabinti wanazijua wenyewe.Unamla Papuchi huku anamkandia Mchumba wake.....tena anasema kabisa "jamaa hanipatii kama wewe".
Hahaha.. Fb raha Sanaa, AF kung'oa wachumba sio kazi ngumu km mitandao mingine..
 
Umenena mkuu..

Kipato cha ' Boda 'hakiwezi lingana na kile cha wale waliobatizwa jina LA ' Wasiojulikana '

Njia pekee ya kufuta machozi yetu kwa kutupotezea ndugu zetu mfano Ben saa8 ni kuwaadhibu wake zao tu..
Kuna ka ukweli hapa
Kwan wangap wanasomesha na wanaachwa kama kawaida tu.
Akili za wanawake wanazijua wenyewe.
Inaonekana jamaa kipato chake hakikumridhisha huyo mdada
Upepo wa hela wa mtoa Uzi n mdogo kuliko wa mchumba
 
Aisee maisha hayo ndio uliochagua, kama kweli Moyo wake upo na ww kule upo mwili bas asingekubal kuolewa yule kaka,

Pole sana ww utabak kuwa mchepuko wake.
 
Amani ya Bwana iwe nanyi..

Nakumbuka ilikuwa ni mwaka Jana, miezi ya mwanzoni kabisa, niko zangu Page ya EaTV Facebook, nikitoa maoni yangu km ilivyo desturi yangu..

Moja ya reply yenye kukwaza ilikuwa ni ya mdada flani, basi na mie skutaka kuwa mnyonge, nilijikuta natumia lugha Kali zaidi hadi mdada wa watu akaamua kunifata inbox na kuniuliza, ' Bro tatizo ni ugumu wa maisha ama nini, mbona unashindwa kuwa mstaarabu..'

Aisee ilinibidi nicheke sanaa, kwani sikutegemea km angenambia alichoniambia. Basi nkamuomba samahani , akajibu nisijali..na maisha yakaendeleaaa..

Tukawa Mara moja moja tunachat, tukazoeana hadi tukachange namba za simu..

Kwa Facebook, hakuwai ku-upload picha yake. So nilikuwa nikichat na mtu nisiyemjua kwa sura. Na mie kwa kufaham apendelei sana maswala ya picha, sikutaka kumkera kwa kumuomba omba anitumie pcha zake..

Hatimae hisia za mapenzi zikatuteka, kuna siku alinitumia pcha yakee.. Nami nkaishia kuguna tu kwani niliamini ananitania tu, nitaamini km ni yeye kweli siku tukikutana..

Niwe mkweli tu, mwanamke huyu alionesha kunipenda sana, mipango ya kuja Daslam ikaanza. Katika kipindi chote hiki, binafsi skuwai muamini kwa lolote japo nilikuwa nikimkubalia tu..

Kuna siku aliniambia km utani tu, ' Jmosi uje ubungo unipokee....sawaa ??' Hahah nkamkubalia huku nkijua utani tu, maana ingekuwa kweli ningeombwa nauli kwanza.. Basi bana, Jmosi hii hapa, Mara text inaingia jiandae uanze kusogea. Tumekaribia..

Basi nikasogelea gari na hatimae nkamuona mgeni wangu. Hakika ni yulee yulee wa kwenye picha. Nikajisemea moyoni ' Sitongoz tena ad siku narudi mavumbini, nitamuoa huyu huyu..'

Nifupishe story..
Niliishi nae vizuri sana, kwani alipanga aondoke bda ya siku mbili, ila tulijikuta tanamaliza week na sehemu. Kila alipotaka kuondoka alishindwa..

Ukweli kumuhusu yeye..
Ni mchumba wa mtuu, japo anaishi kwao bado. Anadai jamaa alimsomesha University. Atafunga naye ndoa km fadhira kwa alichomfanyia. Hawezi kumuacha kisa Mimi..

Ukweli kunihusu..
Sikuwa na mke, mtoto wala mchumba. Nadhani ni moja ya facts zilizomfanya anipende zaidi. Password za simu zangu nilimfundisha, simu zangu zilikuwa ni km zake tu..

Kilichofanya niombe ushauri..
Kwa week mbili nilizoishi nae, alibahatika kubeba ujauzito wangu. Ilimtesa sana, hakuhitaji ushauri tofauti na kutoa. Niliumia sanaa kwani sikuwa na mtoto. Alidai akijifungua inaweza fahamika, ukoo ungemshangaa kwa kumsaliti aliyemsomesha.. Kwa hiyo kimbilio n kutoa tu..

Alipotoa ujauzito wangu na mawasiliano tukapunguza japo yeye hunitafuta Mara kwa Mara..

Leo mwenzangu anandoa na jamaa yakee, lakini Mimi kila nikmwambia habari za kuoa anahuzunika sana, anaishiwa raha na mwisho ananisihi nisifanye hvyo kwani moyo wake upo kwangu kule kuna mwili tu..

Kwa kweli nashindwa kumwelewa kabisa huyu Mwanamke..


Funzo
Wanaume ifike mahali km umeamua kumsaidia mtoto wa kike, umsaidie tu. Sio kusaidia ili bdae umuombe ktu flani..
Jamaa akiwa nae kitandani anajua anapendwaa kumbe hamna lolote.
Huyo ni malaya, Kama amependana na Wewe hajakuona ni hatari Kabisa huyo.
Yaani kwa Comment tu ya Facebook, ameolewa wiki nzimaa?
Mwenyezi amsamehe kwa Usaliti alioufanya na anaoendelea nao.
Lakini na Wewe unaye fanya hayo na mpenzi wa Mwanaume mwenzio, Fikiri Kama ungefanyiwa Wewe.
Sio vizuri hata kidogo.
Hakuna kitu kinauma Kama kuchukuliwa mpenzi.
 
Hao Wanawake mnao wapata Facebook huwa mnapima afya zao kabla ya Kufanya mazoezi?
Angalieni wasije wakawafanya mkose amani na furaha ya kuwepo duniani.
Ukimwi bado upo.
Nyie chiachieni tu, ukiona mtu yuko hivo akili yako inapaswa kuchemka kwakujiuliza maswali mengi.
Kama amefanya hivi na Mimi, keshafanya hivi na watu wangapi?
Ulimpa mimba, Maana yake uliuza mechi. Umeshapima afya yako mkuu?
Sasa hivi hawajulikani hata.
Wengine mnachukua wauza papuchino wa FB mnajiona mmepatiiiia.
 
Back
Top Bottom