Jeh, ananiigizia ama anamaanisha??

Jeh, ananiigizia ama anamaanisha??

FirstClass

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2016
Posts
1,141
Reaction score
1,448
Amani ya Bwana iwe nanyi..

Nakumbuka ilikuwa ni mwaka Jana, miezi ya mwanzoni kabisa, niko zangu Page ya EaTV Facebook, nikitoa maoni yangu km ilivyo desturi yangu..

Moja ya reply yenye kukwaza ilikuwa ni ya mdada flani, basi na mie skutaka kuwa mnyonge, nilijikuta natumia lugha Kali zaidi hadi mdada wa watu akaamua kunifata inbox na kuniuliza, ' Bro tatizo ni ugumu wa maisha ama nini, mbona unashindwa kuwa mstaarabu..'

Aisee ilinibidi nicheke sanaa, kwani sikutegemea km angenambia alichoniambia. Basi nkamuomba samahani , akajibu nisijali..na maisha yakaendeleaaa..

Tukawa Mara moja moja tunachat, tukazoeana hadi tukachange namba za simu..

Kwa Facebook, hakuwai ku-upload picha yake. So nilikuwa nikichat na mtu nisiyemjua kwa sura. Na mie kwa kufaham apendelei sana maswala ya picha, sikutaka kumkera kwa kumuomba omba anitumie pcha zake..

Hatimae hisia za mapenzi zikatuteka, kuna siku alinitumia pcha yakee.. Nami nkaishia kuguna tu kwani niliamini ananitania tu, nitaamini km ni yeye kweli siku tukikutana..

Niwe mkweli tu, mwanamke huyu alionesha kunipenda sana, mipango ya kuja Daslam ikaanza. Katika kipindi chote hiki, binafsi skuwai muamini kwa lolote japo nilikuwa nikimkubalia tu..

Kuna siku aliniambia km utani tu, ' Jmosi uje ubungo unipokee....sawaa ??' Hahah nkamkubalia huku nkijua utani tu, maana ingekuwa kweli ningeombwa nauli kwanza.. Basi bana, Jmosi hii hapa, Mara text inaingia jiandae uanze kusogea. Tumekaribia..

Basi nikasogelea gari na hatimae nkamuona mgeni wangu. Hakika ni yulee yulee wa kwenye picha. Nikajisemea moyoni ' Sitongoz tena ad siku narudi mavumbini, nitamuoa huyu huyu..'

Nifupishe story..
Niliishi nae vizuri sana, kwani alipanga aondoke bda ya siku mbili, ila tulijikuta tanamaliza week na sehemu. Kila alipotaka kuondoka alishindwa..

Ukweli kumuhusu yeye..
Ni mchumba wa mtuu, japo anaishi kwao bado. Anadai jamaa alimsomesha University. Atafunga naye ndoa km fadhira kwa alichomfanyia. Hawezi kumuacha kisa Mimi..

Ukweli kunihusu..
Sikuwa na mke, mtoto wala mchumba. Nadhani ni moja ya facts zilizomfanya anipende zaidi. Password za simu zangu nilimfundisha, simu zangu zilikuwa ni km zake tu..

Kilichofanya niombe ushauri..
Kwa week mbili nilizoishi nae, alibahatika kubeba ujauzito wangu. Ilimtesa sana, hakuhitaji ushauri tofauti na kutoa. Niliumia sanaa kwani sikuwa na mtoto. Alidai akijifungua inaweza fahamika, ukoo ungemshangaa kwa kumsaliti aliyemsomesha.. Kwa hiyo kimbilio n kutoa tu..

Alipotoa ujauzito wangu na mawasiliano tukapunguza japo yeye hunitafuta Mara kwa Mara..

Leo mwenzangu anandoa na jamaa yakee, lakini Mimi kila nikmwambia habari za kuoa anahuzunika sana, anaishiwa raha na mwisho ananisihi nisifanye hvyo kwani moyo wake upo kwangu kule kuna mwili tu..

Kwa kweli nashindwa kumwelewa kabisa huyu Mwanamke..


Funzo
Wanaume ifike mahali km umeamua kumsaidia mtoto wa kike, umsaidie tu. Sio kusaidia ili bdae umuombe ktu flani..
 
Weeee.... Ili ninyi mjipatie taratibu siyo...?? Mimi nafikiri mwanamke huyo angetumia busara kuliko kuitoa mimba... Suala la yeye kukupenda na kukuwekea zuio la kuoa ni ujinga, kama anataka uishi naye angeonyesha ujasiri wa kuikataa ndoa siku yake ya ndoa.... Oa Mkuu achana naye
 
Wanaume ifike mahali km umeamua kumsaidia mtoto wa kike, umsaidie tu. Sio kusaidia ili bdae umuombe ktu flani..

Mkuu ulimuuliza kabla jamaa hajamsomesha walikubaliana nini, au uchumba ndio ulianza baada ya kumpeleka shule.??

Mkuu endelea na mipango ya kuoa kama unayo, achana na huyo Malaya atakuletea ukimwi tu.
NOTE: Ogopa sana maamuzi atayofanya aliyemsomesha siku akijua, keep out of reach of children
 
Humo hakuna mke bali kuna kahaba, kama angekuwa mke asinge fanya huo ujinga wa kituoa mimba
 
Ngoja jamaa aje na full magazine kama Yule wa Kenya ndo utaelewa
 
Mke wa MTU ni sumu , hi kitu bado watu hawaelewi tafsiri yake???
 
We jamaa mapenzi yamekufanya uwe mpumbafu..
Hivi mwanamke mwenye ujasiri kwa KUTOA MIMBA YAKO bado unajidanganya eti anakupenda zaidi ya jamaa anayetaka kumuoa..

Wewe ujue kuna kitu anakitaka kutoka kwako either ni show zako au kitu kingine....

Huyo mwanamke wewe mpige chini akaolewe na aliyemsomesha wewe tafuta wako
 
Unaamin kweli kaolewa ??? Yaan nikweli alikutumia picha za harusi yake .


Umewahi Pima afya baada ya ye kuondoka???
 
Fb hatari sana,Yaani wachumba za watu wanaleta mazoea.Kuna mmoja naye nilimpokea Msamvu kama wewe Ulivyompokea Ubungo.Akili za Wanawake/Mabinti wanazijua wenyewe.Unamla Papuchi huku anamkandia Mchumba wake.....tena anasema kabisa "jamaa hanipatii kama wewe".
 
Back
Top Bottom