Hongereni sana.
Haya ndio mawazo tunayoyataka kwa vijana kama sie.
Ila mwambie Boss kwamba atengeneze website,na pia awe na Official email sio hiyo ya Kindergarten.
Angalua hata website yenye page moja au mbili tu ambayo hata Laki tatu hazifiki.
Maana maeneo mnayo deal na mnayoelekea ni maeneo ya VIP na VVIPs,.Sasa wenzetu wanatabia ya kujua ni namna gani kazi yenu mnafanya na maelezo ya ziada.Yaani kama mkiwa vizuri basi mtapenya sana.
Huo ni ushauri tu,maana hii ndio Bongo,anaweza kuja mmoja akafanya zaidi yenu na kuwa maarufu kuliko nyie kisha nyie ndio mkaja kushtuka.
Mfano mmoja nikupe,kwa kumbukumbu zangu Mfumo wa Mobile Money ulianzishwa na Celtel(Airtel),lakini wakawa hawajajiandaa kisha wakasitisha,wakaja Voda na Tigo wakafanya balaa la mapinduzi ya kasi sana.Leo Airtel wanaibuka hawana jipya tena watu waliishakamata soko zamani sana na wao kurudi kwenye ushindani inakuwa ngum,kwa tafsiri fupi imekula kwao.
Sasa na nyie lazima muweze kutumia fursa,msikwepe gharama za kuweka sawa ofisi yenu,maana akitokea mtu ku beat hapo itabidi mtumie gharama mara mbili.
All the best
Ni mtizamo tu.