Jeff Lea: Simba hamfiki mbali kwa ulinzi ule

Mapenzi yanatuzidia, ni kweli wachambuzi wengi wabongo ni weupe, ila katika hili kuna ukweli, hasa ukiwa ni mtizamaji mzuri wa mpira.
Simba tuna tatizo pale nyuma.

Mpira sio mchezo wa chumbani, unachezwa hadharani na kila mtu anaona.

Nawashauri ndugu zangu game zijazo tutizame hili jambo kwa makini kuna mambo mtang'amua

Sent from my COR-AL10 using JamiiForums mobile app
Nasoma comments zangu mwenyewe nafsi inaniuma, ni km nililichuria chama langu pendwa..

Kule sauzi tulifedheheka ila naimani wakiweka akili saww, kila jambo linawezekana
 
Yuko sahihi, mara nyingi ninapotizama mpira kwenye vibanda hasara, huwa nawaambia watu, tuna tatizo la marking hasa kwenye robo yetu.

Utakuta Kapombe kaenda, kachelewa kurudi, mtu yuko nyuma ya mabeki wawili wa kati peke yake. Mipira ya faulo na kona ndio kabisa, tunategemea mpigaji kichwa akosee au golikipa atusitiri, hakuna mtu na mtu.

Hili kama tusiporekebisha bado kazi tunayo.

Sent from my COR-AL10 using JamiiForums mobile app
Makosa yametugharimu saana haya.
 
Makisa yametugharimu saana haya.
Mimi sikupenda sana simba ipangwe na Kaizer Chiefs kwa sababu ya timu kufanana sana aina ya mpira zinaocheza hata kasi pia na set pieces niliamini wangetupa wakati mgumu sana.

Tungepangwa na CL Belouzdad au MC Alger sasa hivi tungekuwa tunachekelea Semi final.

Ila ndiyo hivyo maombi ya wengi yalikuwa Kaizer Chiefs.
 
Ndio basi tena, kuamgalia msimu ujao sasa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom