Jee Karume ageukwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jee Karume ageukwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngekewa, Dec 25, 2009.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Vuai alisema Rais Jakaya Kikwete, alitoa wazo na changamoto ya dhana nzima ya kuanzishwa kwa mazungumzo ya muafaka na hajashindwa kusimamia dhamira hiyo.

  "Nia ya kuwepo kwa mazungumzo ya kuleta muafaka wa kisiasa kati ya CCM na CUF yameanzishwa na Rais Jakaya Kikwete, alisema hayo huko Dodoma katika mkutano wa Bunge kwa kumuagiza katibu wa CCM kukutana na mwenzake wa CUF,” alisema Vuai.

  Vuai alilazimika kutoa ufafanuzi huo, kufuatia kauli iliyotolewa na mkurugenzi wa chama cha CUF uhusiano wa kimataifa, Ismail Jussa aliyesema kwamba Rais Kikwete ameshindwa kusimamia mazungumzo ya muafaka.

  Jussa alisema mazungumzo ya sasa ya kuleta maridhiano ni kwa ajili ya Wazanzibari tu na kamwe wasihusishwe watu kutoka Tanzania Bara.

  Vuai alisema kauli iliyotolewa na Jussa haina nia njema ya kuleta maelewano na kujenga mahusiano mazuri ya CCM na kambi ya upinzani.
  "Kauli ya kusema CCM haihusiki na mazungumzo ya maridhiano ya kisiasa Zanzibar yaliopo sasa ni sawa na kauli za uchochezi. CCM ni moja na mwenyekiti wake taifa ni Rais Jakaya Kikwete,” alisema Vuai.


  Haya ni maneno ya kada mkubwa wa CCM na upande mwengine Kada mkubwa waCUF juu ya maelewano ya Karume na Maalim Seif.
  Bado najiuliza iwapo jitihada hiyo ni ya Karume au ya Rais Kikwete kama malumbano hayo yanavyoonyesha. Na jee hii kwa upande wa CCM inakaaje hasa tukitilia maanani maneno ya Karume kuwa kuna watu hata upande wa CCM ambao hawaridhishwi na jitihada zake?
  Makada wakubwa Pakacha, Mwiba na Junius mnasemaje?
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Ni vema kujua kuwa wananchi wa Zanzibar pamoja na kumchagua rais wao humchagua rais wa muungano vilevile. Aidha rais wa sasa wa Zanzibar ni Makamu Mwenyekiti wa CCM. Upande Mwingine Maalim alikutana na rais wa Zanzibar baada ya baraka za baraza la CUF.
   
 3. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Huyo Vuai na wenzake kama Shamhuna, Khatibu ni watu wanaopigania tonge ziende tumboni.Si watu wenye kusimamia uzalendo wa kizanzibari, hapo anajipendekeza kwa JK akijua mwakani anaweza kupatia ajira.

  Sisi wazanzibari wala hatushangazwi na kauli ya watu wa namna hii.Sema ni watu hatari kwenye jamii
   
 4. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Naam Swadakta ndugu Mzanzibara! Suwala hapa ni kuwa jee Wazanzibari humchaguwa Rais wa Muungano kwa Ridhaa au La! Halafu Vuai anaposema JK alisema kule Dodoma anasahau kuwa JK huyo huyo alisema mengine kule Pemba?
  Sisi Twajua kuwa Muungwana ni Vitendo sasa tumuulize Vuai ni nani muungwana hapa kati ya Karume na JK?
   
 5. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Maalim amekutana na Rais wa Zanzibar kutokana na baraka za Baraza Kuu la CUF. Lakini Rais wa Zanzibar amekutana na Maalim katika capacity yake ya Urais wa Zanzibar na siyo mwamvuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala CCM (ambako yeye Rais wa Zanzibar ni Makamo Mwenyekiti). Mimi naunga mkono watu kama kina Jussa na waliyosema katika hadhara ya REDET. Na Tumwachie Karume katika ulingo wake kama Rais wa Zanzibar aen delee na hizi juhudi mpya za kusaka suluhu. CCM na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Rais Kikwete) wasitie mikono- wakae chonjo kwa wakati huu. Tuangalie juhudi za sasa zitatufikisha wapi.
   
 6. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  karume hana muafaka wowote anaotaka bali mda wake umeisha anatafuta jinsi ya ku prolong nguvu zake za kisiasa na pia kuhakikisha mtu ambaye hamtaki yeye hashiki madaraka
   
 7. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Ni kweli Karume anamaliza muda wake lakini hili la nini anaweza kufanya hivi sasa ni suwala la kujadiliwa. Mara zote kwenye uchaguzi wa vyama vingi viongozi walio madarakani ndio wanaoweka foundation ya uchaguzi unaofuata na tukilikumbuka hilo na namna ushindi wa CCM unavyopatikana Zanzibar it si matter of concern (msimamo wa Karume)
   
 8. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2009
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Huyu bwana (Karume) alipoingia madarakani alinyang'anya mali nyingi za (ahli bayt/washika dau/wapambe/homeboys/wanamtandao...name them) wa Dkt Salmin.....Sasa anaona zamu yake inakaribia,,anadhani kwa kufanya hivyo alivyofanya Maalim (nae sidhani kama atapata ulaji) atamsamehe kitu ambacho sidhani
  Deep down inside,,sidhani kama Karume anacho hicho anachotaka watu wadhani kwamba anacho (Zanzibar mpya)
  Tena huyu (karume na familia yake) ndio kanyang'anya mali za watu kweli kweli mpaka wanamuita majina ya ajabu ajabu..wala sidhani kama atathubutu kuendelea kuishi visiwani baada ya uchaguzi wa mwakani..
  Mkuu mzee mwanakijiji plzz kama una kijisehemu huko kijijini kwako tayarisha bei na lawyer,,,mteja yupo njiani
   
Loading...