Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,948
- 74,430
Ibara ya 46(2) – Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (kama ilivyofanyiwa marekebisho)
"Iwapo Rais anaonekana kuwa hawezi kutekeleza majukumu ya kazi ya Rais kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili, basi Baraza la Mawaziri linaweza kupeleka taarifa kwa Jaji Mkuu ambaye atamwagiza Daktari Mkuu wa Serikali au jopo la madaktari walioidhinishwa kumfanyia uchunguzi. Kama ripoti ya madaktari itathibitisha kuwa Rais hawezi kutekeleza majukumu yake, basi itatolewa taarifa rasmi na Jaji Mkuu, na nafasi ya Rais itachukuliwa kwa mujibu wa Katiba."
Maelezo ya ziada:
- Mchakato huu unalenga kuhakikisha kuwa Rais ambaye hawezi tena kutekeleza majukumu kwa sababu ya maradhi (ikiwemo ya akili) anaondolewa kwa njia ya kikatiba.
- Ni lazima Baraza la Mawaziri liwasilishe taarifa hiyo kwa Jaji Mkuu.
- Jaji Mkuu ndiye mwenye mamlaka ya kuanzisha uchunguzi wa kiafya dhidi ya Rais kupitia kwa Daktari Mkuu au jopo la madaktari.
Maradhi ya afya ya akili ni ya kawaida kumtokea binadamu yeyote na sababu zake ziko wazi na hazibagui mtu.
Jee kwa katiba yetu hii na baraza letu hili la mawaziri lililojaa wajumbe wanaoogopa kusema ukweli, kujipendekeza na kushauri huku wakipima upepo wanaweza kufanya kazi hiyo ya kumwagiza Jaji Mkuu atimize wajibu wake kuagiza Rais apimwe?
Tunajua, Rais kuna kipindi anapitia wakati mgumu kama binadamu hadi akaingiwa woga na kuchanganyikiwa. Na kwa mamlaka makubwa aliyo nayo akatoa maagizo hatari ambayo hata watu wake wa karibu hawayaafiki au kupokea ushauri toka kwa watu wabaya bila kujitambua.
Binafsi nimepata mshangao wa majibu ya siku za karibuni kwenye masuala nyeti, issue ya Gwajima, handling ya sakata la ugaidi kwa Lissu katika siku hizi kuelekea uchaguzi nk.
Binadamu ukijihisi mwili maumivu unapima maradhi kama malaria, lakini ukiamua mambo isivyo kawaida au pressure za no reform no election zikikuelemea basi wenzako wanakupeleka kupima afya ya akili ili upumzike.
Kwa manufaa ya nchi na wahusika uchunguzi ufanywe.
