Nimecheka sana. Imenikumbusha movie niloangalia jana inaitwa "Reload" kuna wanawake wana wivu wa kufa mtu. Kuna mmoja huyo kila akiona gari ya mumewe anamwambia dereva wake waifuatilie. Kuna siku wamefuatilia mpaka hotel mumewe katoka na kabinti kwenye gari wacha mama akachimbie mkwara. Siku nyingine kaona gari ya mumewe kaifuatilia (huwa yeye ana dereva afu it seems ni mama wa nyumbani ila ndo mwenye pesa ambazo hubby wake anatumbua) kakuta kumbe gari yao (Vogue) inaendeshwa na mwanamke na si mumewe. Alichokifanya ni kumdaka yule dada, ambaye inaonyesha alikuwa anaenda ku book chumba hotel na alikuwa ni staff wa kampuni yao, na kumwamuru ampe dereva wake funguo afu akampandisha nyuma wakakaa wote akiwa anampa mkong'oto mpaka wamefika nae home kwao. Kachukua mkanda kaendelea na shughuli ya kumtandika. Mume baada ya kusaka kimada wake anakuta gari ya wife imepaki hotel akajua kimeshanuka. Kukimbia home kakuta kimada yuko hoi. Eti anajitetea huyu ni just co worker. Wife anasema eeh ngoja nimfunze adabu ili aogope other people's property (sikujua ana maana ya mume au ile vogue aliposema other people's property). Ni movie nzuri inaonyesha jinsi gani wanawake tuko possessive na tunavyopenda ku deal na the other woman na si wapenzi wetu.