Mathayo 6: 25. Kwa sababu hiyo ninawaambia ninyi: Acheni kuhangaika
+ juu ya nafsi zenu kuhusu kile mtakachokula au kile mtakachokunywa, au juu ya miili yenu kuhusu kile mtakachovaa.
+ Je, nafsi haimaanishi zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi?
+ 26 Waangalieni kwa makini ndege
+ wa mbinguni, kwa sababu hawapandi mbegu au kuvuna au kukusanya ghalani; na bado Baba yenu wa mbinguni huwalisha wao. Je, ninyi si bora kuliko wao?
+ 27 Ni nani kati yenu kwa kuhangaika anaweza kuongeza kipimo cha mkono mmoja kwenye uhai wake?
+ 28 Pia, katika lile jambo la mavazi, kwa nini mnahangaika? Jifunzeni kwa mayungiyungi
+ ya shamba, jinsi yanavyokua; hayafanyi kazi, wala hayasokoti;
29 lakini ninawaambia ninyi kwamba hata Sulemani
+ katika utukufu wake wote hakupambwa kama moja la haya.
30 Basi, ikiwa Mungu huivika hivyo mimea ya shambani, ambayo ipo hapa leo na kesho hutupwa ndani ya jiko, je, yeye hataona ni afadhali zaidi awavike, ninyi wenye imani kidogo?
+ 31 Kwa hiyo msihangaike
+ kamwe na kusema, ‘Tutakula nini?’ au, ‘Tutakunywa nini?’ au, ‘Tutavaa nini?’
32 Kwa maana vyote hivi ndivyo vitu ambavyo mataifa yanafuatilia kwa tamaa. Kwa maana Baba yenu wa mbinguni anajua mnahitaji vitu hivi vyote.
+33 “Basi, endeleeni kuutafuta kwanza ufalme na uadilifu wake,
+nanyi mtaongezewa hivi vitu vingine vyote.
+ 34 Kwa hiyo, msihangaike kamwe juu ya kesho,
+ kwa maana kesho itakuwa na mahangaiko yake yenyewe. Unatosha kila siku ubaya wake.