atufigwege_jr
Member
- Oct 6, 2026
- 5
- 3
Nadhani wengi mtakubaliana na mimi kwamba ukienda kwenye miji mingi, utakutana na watu wengi wanaopitia changamoto za afya ya akili kuliko unavyoweza kutarajia.
Lakini kuna jambo huwa linanipa maswali.
Fikiria mtaani kuna makopo kibao yaliyotapakaa. Lakini kuna mtu ambaye kila siku akiamka asubuhi, kitu cha kwanza anachofanya ni kuwahi mjini kwenda kuokota makopo. Yaani ana ratiba, ana malengo na anaamka mapema kuliko watu wengi wenye kazi za ofisini.
Wakati huohuo, mtaani kwenu kuna kijana mwenye akili timamu, hana kibunda, hana kazi, lakini kila siku yupo kwenye kijiwe akijadili maisha ya watu wengine, mpira na mipango mikubwa ya maisha ambayo haijawahi kuanza.
Sasa hapa ndipo ninapojiuliza,
Huyu wa kwanza anaamka kila siku kwenda kutafuta makopo ili apate cha kula. Huyu wa pili anaamka kila siku kwenda kijiweni kutafuta story, huku maisha yake yakiwa palepale.
Swali langu ni hili: Ni nani hasa anayehitaji kujitathmini zaidi kati ya hawa wawili?
Je, ni yule ambaye jamii inamwona kama amepoteza mwelekeo, au ni yule ambaye jamii inamwona yuko sawa, lakini miaka inakatika bila hatua yoyote ya kubadilisha maisha yake?
Tusihukumu watu kwa mwonekano tu. Lakini pia tusitumie kicheko kukwepa maswali kuhusu maisha yetu wenyewe.
Je, kuwa na akili timamu bila mwelekeo ni bora kuliko kuwa na changamoto za afya ya akili huku ukijituma kutafuta riziki?