ameline
JF-Expert Member
- Jan 8, 2013
- 2,292
- 1,152
[h=3]HILI SUFURIA UKILITAZAMA SUPU ILIYOPIKWA HUMO HUWEZI KUITAMANI,LAKINI....[/h]
[h=3]KUTANA NA KITU CHA MTURA[/h]
Hapa imepikwa supu ya hatarii yenye mchanganyiko wa makongoro,utumbo,mkia,ulimi n.k
Sufuria huwekwa mezani kama hivi na watu hulizunguka kuchagua unachotaka
Hapo unasimama unachagua kipande unachokitaka unakatiwa katiwa na kuwekewa supu kwenye kibakuli huku ikiwa ni ya motoooo.
Baada ya nusu saaa tu sufuria linawezakuwa jeupeeee mzigo umekata.
[h=3]KUTANA NA KITU CHA MTURA[/h]
Mtura ni chakula maarufu sana mkoani Arusha.Ni utumbo ule unaoitwa utumbo wa maziwa unaoshwa vizuri na kufungwa halafu ndani kuwekwa vipande vidogo vidogo vya nyama.Nyama hizo zinakuwa zimetiwa pilipipili,ndimu,mboga mboga na viungo mbali mbali inategemea.Halafu unafungwa na kuchomwa.
Ukiiva ndio unaliwa na salad kama hivyo na ndizi hata chipsi.Karibuni sana Arusha jaman, msisite kunitafuta ili niwapeleke zinakopatikana huduma hizi.....