Je, wewe ukikutana na mwanamke huyu utafanya nini?

Rahajipe

Senior Member
Joined
Oct 29, 2012
Posts
165
Reaction score
63
Heri ya PASAKA wana JF wote na hususani wana MMU!

Yawezekana wewe unayesoma hii mada upo mzima ki mwili, ila ki hali upo taaban sana kutokana na nijirusho ya weekend ndefu iliyopita.
Wana MMU, naomba kwa hadhali kubwa tusaidiane kutoa mawazo yanayotokana na uzoefu tulionao katika maisha yetu ya kila siku.
Binafsi mimi ni mtu nipo huru kwa maana ya kwamba (SINGLE) Nimewahi kuishi na mshika dau tukashindwana na kila mtu akageukia njia aliyotokea! Kutokana na mazingira ya hali hiyo jinsi yalivyoniumiza na kujikuta nikiwa kama naanza maisha upya, sipendi sana kuwapa kipaumbele hawa washika dau wenzetu ( wanawake) kwa maana kuwa sasa naishi kama DUME LA NYANI.

KILICHOTOKEA!
Siku ya Jumapili baada ya kumaliza kipindi kigumu sana cha kusafirisha mwili wa marehemu rafiki yangu aliyefariki ghafla siku ya Ijuma Kuu! Basi usiku niliamua kutafuta sehemu yoyote yenye kelee nikae nipate msosi kisha nisogeze masaa halafu nikalale.

nilikaa Kaunta na nikaagiza kinywaji changu! watu walikuwa wengi na walikuwa wanacheza Muziki kana kwamba kufa hakupo. Wakati nimekaa hapo, wanawake kama wanne kila mmoja kwa wakati wake walikuwa wakinikonyeza na mimi sijibu lolote! Baadae alikuja dada mmoja akakaa karibu yangu! aliagiza bia moja akainywa kama vile kwa hasira fulani! Walitokea jamaa kama wawili wakawa wanamtaka kwenda kucheza nao ila kila mmoja kwa wakati wake.

Yule dada alikuwa aking'aka kwa hasira na kuwaambia " HIVI KILA MNAYEMUONA HAPA MNAFIKIRI AMEFUATA UPUUZI WENU HUO? HEBU NIACHENI NIPUMZIKE ZANGU!" Niligeuka nikamwangalia kisha nikaangalia jamaa aliyekuwa anamgasi nikakaa kimya.

Dada alipomaliza bia yake aliondoka taratibu pasipo kusema na mtu, na mimi baadaye nilimaliza kinywaji changu nikatoka na kupanda usafiri wangu na kuondoka.

Baada ya dakika chache nilipofika mbele, kumbe na yule dada alikuwa anaelekea njia hiyo hiyo. Nilisimama kwa tahadhari kutokana na kwamba kweli alionekana kuvurugwa akilini.

"............ Aaaah, jirani yangu wa Kaunta kumbe na wewe uaelekea huku?!" niliposema hivo alisimama na kuniaangalia!! ........ Aaah, kumbe ni wewe ulikuwa umekaa pembeni mwangu?"
Ndiyo! Nilimjibu huku nikimwambia........ samahani kama naweza kukusogeza kidogo, japo hakukataa ila aliseme siishi mbali ni hapo mbele kidogo. alipanda na tulipofika nilimshushaila kabla ya kuagana nilimwambia kama hutaojali naomba namba yako kwano nimependa sana behavour yako.

Wala usitie shaka naomba simu yako nikuandikie! Binti aliniandikia na kuniambai usiku mwema.

BIG RESULTS NOW!!
Kesho yake nilikwenda kibaruani, mida ya saa tatu hivi alinitumia ujumbe mfupi. "Mzima wewe!" nilimjibu kuwa ni mzima na nimefurahi kupata salaam zake. Nilimwuliza, vp mbona jana ulikonekana kuwa na hasira kupita kiasi, tatizo nini?!!
Aliguna na kuishia kuguna "Mmmmh" kisha alikata simu! baadae alinitumia ujumbe wa SMS kuwa........... "Nina mengi sana yanayonisibu, laiti kama ningeweza kaburini nikamuamsha baba yangu akayaona, nahisi ningekuwa na amani maisha yangu yote"
Kwangu hameno hayo yalikua mazito sana!! Nilimuomba tutafutane walau nipate kumsikia ana kwa ana labda nimpe ushauri!
Alisema ningependa kupata mtu kama huyo lakini wewe ni mume wa mtu haitawezekana kwani nitaona kukaa na wewe nafanya kile ninachofanyiwa.................!!
Ndipo nilipomwambia, tatizo unajiuliza swali na unajipa jibu mwenyewe, kwa hali hiyo ni ngumu kupata jibu yakini.
Nilimwambia usijali panga muda wako mimi napatika hata saa nane za usiku, sifungwi na mtu!! Ok, kama hivyo labda tuonane mida ya jioni!

Kweli mida ya saa moja alinitumia ujumbe na kuniuliza wapi nilipo, nilimwelekeza na akaja.

Nilimuagizia kinywaji kama cha jana yake lakini alikataa na kusema yeye si mnywaji bali ilitokea tu! Baada ya hapo tuliingia kwenye MADA na nilipomuuliza kwa kina alijikuta akifunguka mambo yake ya ndoa ya ndani sana! huku akisema......... "Nimekuona mstaarabu sana ndiyo maana nimejikuta nikitokwa maneno mfululizo, labda unaweza kunipa ushauri".

Kwakweli, nilihisi kutokwa na machozi!! Binti si mdogo wala si mkubwa kwa umri, bali ni mtu anayejitambua, kujiheshimu na nimtafutaji mzuri kwani ameweza kumlea mmewe kwa miaka zaidi ya minne akiwa hana kazi, Jamaa alivyopata kazi amefungua miradi na mwanamke mwingine na bado anaweza kulala hata siku tatu bila kuja home!!

Mdada huyu amejitwisha mzigo wa kusimamia ujenzi wa nyumba yao ambayo ipo kwenye hatua za mwisho kwa hela yake anayoitafuta!! Wakati mwingine jamaa huwa anamlazimisha eti waende wote kwenye miradi yake aone, wakati huo huo akijua kuwa hajamshifrikisha kwa lolote.

Lakini kubwa ambalo nimejifunza kwa huyu dada, ni uvumilivu na ujasili wa ajabu japokuwa wengine wanaweza kuuita umbumbumbu hasa kwa wanawake wengi wa kizazi hiki kama alivyo yeye!

Hadi kuamua kuleta uzi huu ni kitendo cha juzi ambacho nilikishuhudia mwenyewe! Kwani jamaa baada ya kulala nje ya nyumba yake hata bila taarifa, ilipofika usiku alimtumia ujumbe mkewe na kumbwambia....... "I luv u honey........" leo umepika nini?

Yule dada alimjibu............. I luv u 2222222" na kumwambia sema chochote unachotaka kula mume wangu nikuandalie!!!!!!!

Jamaa alipendekeza chakula anachotaka kisha akaomba awekewe bia kadhaa nyumbani ili akija azikute!!!!
na binti wa watu bila kinyonyo alimjibu ............ "Worry not"

Picha hii nimeishuhudia mwenyewe na ni storry ndefu sana ila nimejaribu kuifupisha.

Je, wewe kama ungekutana naye ungempa ushauri gani?? Nauliza hivyo kutokana na ukweli kuwa baada ya kukaa naye na kumfanyia canceling kubwa tumejikuta tukiwa karibu sana kiasi kwamba ananiona kama baba, mama, kaka na mpenzi wake! haswa mara baada ya kumaizi kuwa hata mimi ni mmoja wa wahanga wa mapenzi.

TAFAKARI SANA KABLA YA KUCHANGIA.
 
Duh aisee kuna watu wana roho za tofauti sana hapa duniani na hawa

wanaume me hawaachi kunishangaza hivi inakuwaje na mtu mwenye upendo wa dhati

hivyo na still unachepuka..........na siku huy mwanaume kwa mfano akigundua mkewe ana mchepuko nje

hakutakalika siku hiyo kuna muda roho yangu huwa inaniuma sana I wish I just wish...........
 
Noo kaka mwanamke yupo sawa haswa kwenye swala la uvumilivu ila je swala hilo alishaliweka bayana kwa mumewe au ndugu wa karibu juu ya tabia zake hizo(mumewe)????
 
..

....Endelea kuwa na moyo wa chuma katika hayo mahusiano ...kwani kuhasi na kuchanya ni kama pua na mdomo !!!!
 
Duh aisee kuna watu wana roho za tofauti sana hapa duniani na hawa

wanaume me hawaachi kunishangaza hivi inakuwaje na mtu mwenye upendo wa dhati

hivyo na still unachepuka..........na siku huy mwanaume kwa mfano akigundua mkewe ana mchepuko nje

hakutakalika siku hiyo kuna muda roho yangu huwa inaniuma sana I wish I just wish...........

Kwa kweli hii story ni somo tosha sana kwa pande zote mbili!! iwe kwa mwanamke au mwanamme. Kwangu mimi nasema hivi kama walau katika ndoa za sasa 100 tungekuwa na wanawake hata 5 tu wa hivo, hakika ndoa zingekuwa tamu.

Ushauri jitahidi sana kumpa moyo kwa kuwa ameshakuamini, jifanye kuwa wewe umevaa joho tu! Kwani siku akiamua kuchepuka atakuwa kama trela lililokatika kwenye mlima Kitonga.

Haya Dada yangu Heaven waalike na wenzako kutoa ushauri hapa.
 
Noo kaka mwanamke yupo sawa haswa kwenye swala la uvumilivu ila je swala hilo alishaliweka bayana kwa mumewe au ndugu wa karibu juu ya tabia zake hizo(mumewe)????

Hukuwa na lazima ya ku-quote uzi wote..!!
 
Amekuamini msaidie ila Chunga bamsap wake asijekukurarua akijua unampelekea moto mamsap wake
 
Je, wewe kama ungekutana naye ungempa ushauri gani?? Nauliza hivyo kutokana na ukweli kuwa baada ya kukaa naye na kumfanyia canceling kubwa tumejikuta tukiwa karibu sana kiasi kwamba ananiona kama baba, mama, kaka na mpenzi wake! haswa mara baada ya kumaizi kuwa hata mimi ni mmoja wa wahanga wa mapenzi.

TAFAKARI SANA KABLA YA KUCHANGIA.
Huyo Jamaa siku akikudaka hatakuwa na uvumilivu ambao mke wake anao....lazima akufanye HAMNA...si unajua Mwizi Akiibiwa?

Nikirudi kwenye Avator yako....napata wasiwasi na cancelling uliyompa!
 
Mimi nikushauri wewe mleta maada nliwahi kukutana na stuation kama hiyo. Nasikitika sana kwani ndoa ilishajeruhiwa vya kutosha ila mimi nikaimalizia kabisa so sad i feel guilty halafu nashindwa kuifufua tena.
 
wewe ni mtunzi mzuri wa hadithi jitahidi soko lipo
 
Siku zote mwanamke ni mtu mmoja mvumilivu sana hata aumie kiasi gani, kikubwa kama ana watoto ajibidishe amalizie hiyo nyumba wanayojenga wahamie kwani watoto kama anao watakuwa ndo furaha yake hata kama nafasi ya mume ipo, kama wako ni wako tu hata akichukuliwa na king'asti miaka 5, pole sana kwa huyo dada
 
nasikia kaharufu ka uzaid ya ukaribu inanukia kwa mbali...kila mtu anajanga lake la mapenzi...uvumilivu upo inafika hatua kwakwel unanyoosha mikono...
 
mi nashauri uendelee kukaa mbali hivyo hivyo ka mdomo na macho ili ulimi wako usijefuta MATONGOTONGO Na hatimaye ......mwanamke akikukubali hautokiiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom