MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Kurudishwa kwa Prof. Muhongo na pia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliachim Maswi kumezua maswali ambayo yanahitaji majibu mbadala!
Nisingepata maswali kama wangerudishwa na Serikali ya Rais Kikwete kutokana na historia yake kiutendaji lakini ninapatwa na maswali baada ya kurudishwa kwenye nafasi za juu za kisiasa katika serikali ya Rais Magufuli ambayo inajipambanua na nimeiona ni no-nonsense, results-driven government.
Kwa alichokifanya Rais Magufuli na historia aliyonayo ndani ya serikali, uteuzi wa Prof. Muhongo na Maswi unatoa picha nyingine kwenye kadhia ya Tegeta Escrow Account.
Wakati wa sakata la Tegeta Escrow account, Kumbukumbu zinaonyesha Prof. Muhongo aliwahi kusema hawezi kujiudhuru na kama ikitokea hivyo basi nchi itatikisika.Kwa maana nyingine, alikuwa amebeba bomu kubwa la kisiasa ambalo alikuwa tayari kuripua iwapo atashinikizwa kujiudhuru hata hivyo inaonekana alishauriwa na watu wa ‘’kitengo’’, akajiudhuru ili kulinda heshima ya serikali kwa matarajio ya baadaye.
Hata aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliachim Maswi aliwahi kusema hahusiki na sakata hili bali alifanya kazi kama alivyoshauriwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema.
Maswi baada ya kusafishwa na tume ya maadili, aliteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara huku Prof. Muhongo akijikita kutafuta nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea Urais na ubunge kwa tiketi ya CCM.
Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema alikiri hata ndani ya Bunge, kuwa ni kweli kuwa alitoa ushauri kwa mamlaka ya juu ili kuidhinisha fedha kutolewa na kwa maana hiyo yuko tayari kubeba msalaba wa Prof Muhongo na Maswi. Kwa sasa amerudi kwenye kazi yake ya Ujaji.
Mpaka sasa tunachofahamu ni kuwa, pesa zilichukuliwa lakini hatufahamu nani aliyechukua na kuweka kwenye ‘’mifuko ya lambo’’ na lumbesa katika Benki ya Stanbic, lakini kikubwa zaidi, hizo pesa zilienda wapi?
Uchunguzi wa sakata hili mpaka sasa ‘’haujamalizika’’ lakini waliowajibika kisiasa wamerudishwa katika nafasi za juu nchini.
Kwa yanayofanyika kwa sasa, kuna hatari na uwezekano tulikuwa tunacheza ngoma ya kisiasa ambayo hatufahamu mapigo yake achilia mbali wapigaji wake.
Hizi teuzi zinaacha maswali mengi bila majibu!
Ama kweli usilolijua...