Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Kumekuwa na matukio mfululizo ya watu kutekwa, na watu tunaoaminishwa na serikali yetu iliyoko madarakani kuwa watu hao ni watu wasiojulikana, matukio ambayo yameongezeka sana katika utawala huu wa awamu ya tano, matukio ambayo hapo siku za nyuma hayakuwepo.
Swali kubwa tunalojiuliza wananchi, je watu hao wasiojulikana, je wana "connection" yoyote na vyombo vya dola, hususani na Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa?
Jibu ambalo naweza kulitoa ni kuwa watu hao tunaoaminishwa kuwa ni watu wasiojulikana ni watu WANAOJULIKANA vizuri sana na vyombo vya dola, hususani na Jeshi letu la Polisi na Usalama wa Taifa.
Nasema hivi nikiangalia namna ambavyo watu wanatekwa, watu wanashambuliwa, huku kitendawili hiki cha watu wasiojulikana kikiwa hakijatatuliwa.
Najua kuwa wajibu mkubwa namba moja wa Jeshi letu la Polisi ni kuwalinda Raia wake na Mali zao.
Sasa inapotokea raia wanaishi kwa hofu kubwa, wasijue ni lini na saa ngapi na wao watatekwa na watu wasiojulikana, ni dhahiri hapo kuwa Jeshi letu la Polisi linaposhindwa kuwabaini watu hao wasiojulikana, basi Jeshi hilo la Polisi, limeshindwa katika wajibu wao namba moja wa kuwalinda raia wake na mali zao na hivyo ni wajibu wa Rais wa nchi awatumbue viongozi wakuu wa Jeshi hilo la Polisi nchini.
Iwapo pia Rais wa nchi haonyeshi dalili yoyote ya kuguswa na yanayoendelea nchini, wananchi tunapata picha kuwa matukio yote yanayotokea nchini yana "baraka" zote za uongozi wa juu hapa nchini
Ni jambo lililothibitishwa kuwa kutokana na "staili" ya utekaji waliofanyiwa mwandishi wa habari Eric Kabendera na hili la hivi majuzi la Tito Magoti kuwa Jeshi letu la Polisi nchini "linahusika" aidha directly au indirectly na matukio ya kutekwa kwa hao niliowataja.
Zipo sababu za kueleza kuwa nimejiridhisha kuwa vyombo hivyo vya dola vinahusika moja kwa moja na utekaji huo.
Tukiangalia matukio yote hayo mawili namna yalivyotekelezwa ni lazima wananchi washuku kuwa vyombo hivyo vya dola, yaani Jeshi letu la Polisi na Usalama wa Taifa, ni vigumu vyombo hivyo vya dola, kujiweka kando na matukio hayo ya utekaji.
Jeshi letu la Polisi linajua taratibu za kumkamata mtu ambaye wanamshuku kuwa ni mhalifu, zikiwemo kujitambulisha kuwa wewe ni askari na uonyeshe kitambuisho chako cha kazi na yule unayemkamata unamweleza sababu za kumshuku kuwa ametenda uhalifu gani wa jinai na pia ni lazima wakati unamkamata uwajulishe jamaa zake wa karibu ni katika kituo kipi cha Polisi ambako unampeleka mtuhumiwa huyo na unawaeleza pia ndugu wa mtyhumiwa huyo kuwa wanaruhusiwa kumteua mwanasheria wao atakayewawakilisha katika kutoa maelezo Polisi.
Ni jambo la ajabu kuwa taratibu zote hizo za kisheria ingawa zinaeleweka wazi na Jeshi letu la Polisi, lakini taratibu zote hizo za ukamataji wa mtuhumiwa zilikiukwa katika kuwakamata watuhumiwa Eric Kabendera na hili la majuzi la Tito Magoti.
Vile vile kujichanganya wanakojichanganya Jeshi letu la Polisi katika kutoa Maelezo ya watu hao wanaowakamata ndiko kunaashiria kuwa Jeshi hilo la Polisi ni "part and parcel" ya watu hao wasiojulikana.
Maoni yangu hayo nayatoa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 18(1) ambayo inasema "mtu yoyote yuko huru kutoa maoni yake katika chombo chochote cha habari na mawasiliano yake hayapaswi yaingiliwe kati na chombo chochote kile" mwisho wa kunukuu.